TCRA kulazimisha laini moja tu kwa kila mtandao kwa Raia si sahihi!

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Juzi nikiwa katika viunga vya bunge na baadhi ya maafisa wa serikali, kuna jambo la ajabu sana nilisikia eti ule uvumi ulio kuwepo mwanzo kwamba raia hata ruhusiwa kusajili laini zaidi ya moja ni uhalisia.

Nikajiuliza lengo hasa ni nini?

Kama nina laini 100 na zote nimesajili kwa vidole tatizo lipo wapi?

Akili vs matope?

TCRA imesema lengo la kusajili kwa vidole na vitambulisho vya NIDA ni kukabiliana na ujambazi na uhalifu, sasa swala la laini moja linatoka wapi?

Nilimweleza mbunge mmoja, anatokea mkoa Kagera kwamba ajaribu kuishauri Serikali kuachana na issue ambazo hazina manufaa na zinaloleta usumbufu na maisha magumu kwa wananchi.

Mnataka wote tuwe na maisha ya gerezani?

409B8D98-733F-43A3-AADB-10851EB3770D.jpeg

AC7B5EDA-6EBB-4443-AAEB-DE086C11D8ED.jpeg

00FC6EDB-3175-4D62-B939-DDD128D8E70C.jpeg
 
Mnaokomenti msilishwe maneno ya hovyo serikali ishalitolea ufafanuzi Jambo hili ni kuwa uwe na laini moja kwa mtandao mmoja.

Nyie ropokeni tu hapa kwa kumfuata mtoa mada mnaendekeza ukilaza haingii akili hata kama viongozi wetu wameishiwa utafakari huku ni sawa na kuwatukana viongozi na wengine mnashabikia kwa kitu si kweli!!!

Hili taifa lina wananchi bendera fata upepo.
 
Mnaokomenti msilishwe maneno ya hovyo serikali ishalitolea ufafanuzi Jambo hili ni kuwa uwe na laini moja kwa mtandao mmoja.
Nyie ropokeni tu hapa kwa kumfuata mtoa mada mnaendekeza ukilaza haingii akili hata kama viongozi wetu wameishiwa utafakari huku ni sawa na kuwatukana viongozi na wengine mnashabikia kwa kitu si kweli!!! Hili taifa lina wananchi bendera fata upepo.
Na kwa bahati mbaya sana wananchi hao "bendera fata upepo" wanaujua upepo mmoja tu wa CCM.

Hivi uliliwaza hilo ulipokuwa unaandika maneno hayo, maanake inaonekana wewe ni CCM damu damu!

Hebu jaribu kuwahimiza wananchi hao waache hiyo tabia ya kuwa "fata upepo" - ukiweza hilo, nitaungana nawe katika yote uliyoandika hapo juu.
 
Mnaokomenti msilishwe maneno ya hovyo serikali ishalitolea ufafanuzi Jambo hili ni kuwa uwe na laini moja kwa mtandao mmoja.

Nyie ropokeni tu hapa kwa kumfuata mtoa mada mnaendekeza ukilaza haingii akili hata kama viongozi wetu wameishiwa utafakari huku ni sawa na kuwatukana viongozi na wengine mnashabikia kwa kitu si kweli!!!

Hili taifa lina wananchi bendera fata upepo.
Line za simu kwa sasa ni vibubu.Nina biashara tatu na sehemu ninayokaa mtandao mzuri kwangu ni Tigo na kila jioni nahitaji kuweka kipato changu kwenye account yake ili nisichanganye vibiashara vyangu na ili niwe na rekodi nzuri ambayo naweza kuipeleka mahali.

Kuna shida mahali.Serikali itueleze kwa uwazi hofu iko wapi,nini kinaweza kutokea mtu akiwa na line zaidi ya moja,ni yapi madhara ya kuwa na laini zaidi ya moja kwa uchumi wa nchi,usalama wa nchi n.k.Wakiwa wazi na tukaelewa itatuepusha na kupingana kusipo na sababu.

Israel ilikuwa na na mpaka leo ipo "collective punishment"Kijiji chenu kikitoa mtu mmoja akamdhuru Myahudi mjiandae makazi yenu kubomolewa.Inawezekana serikali kuna watu inataka kuwadhibiti,itusaidie maelezo ya kutosha ili tushirikiane nayo vilivyo.
 
Mnaokomenti msilishwe maneno ya hovyo serikali ishalitolea ufafanuzi Jambo hili ni kuwa uwe na laini moja kwa mtandao mmoja.

Nyie ropokeni tu hapa kwa kumfuata mtoa mada mnaendekeza ukilaza haingii akili hata kama viongozi wetu wameishiwa utafakari huku ni sawa na kuwatukana viongozi na wengine mnashabikia kwa kitu si kweli!!!

Hili taifa lina wananchi bendera fata upepo.

Hivi hauwezi kuhitaji kuwa na line mbili zenye plan tofauti kwenye mtandao mmoja? mfano line moja ya postpaid na line nyingine ya prepaid?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huenda hata mleta hoja hajaelewa/hakuelewa nini kilichosemwa au kuandikwa.

Soma tena ulichokituma wewe then tujadili.View attachment 1356946
Kwani mtu akiwa na laini zaidi ya moja za mtandao huo huo shida inatoka wapi as long as he is duly registered! ?

Kuna watu wanatumia devices tofauti tofauti kwa ajili ya mawasiliano na internet!

Unahitaji ku connect laptops, computers, simu zaidi ya moja nk.

Badala ya kwenda mbele katika kutumia fursa za utandawazi, magufuli yuko bize kuturudisha chattle enzi za ujima 987 BC!

Inafikirisha sana! Huyu mzee ana ajenda gani iliyojificha nyuma ya huu uovu wake wote?

He is extremely busy creating troubles all over the place!

Niseme tu kwamba, huyu mzee kama hana nia ovu, basi ana ushamba usiomithilika!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulieleta habari na wewe hukuilewa ni laini moja kwa mtandao mmoja, na sio laini moja tu
Kwa nini wanaweka ukomo huu?

Nikiamua kuwa na line moja ya internet tu, na line nyingine ya kuongea tu, hapo kuna tatizo gani?

Nikiamua kutenganisha line ya mambo ya biashara zangu na line ya mambo ya binafsi ili niweze ku reconcile mapato na matumizi kihasibu vizuri zaidi, tatizo liko wapi?

Kuna wakati jiji la Tokya Japan lilikuwa na line za simu nyingi kupita bara zima la Afrika.

Naona tunatamani kurudi huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom