Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,022
- 10,189
Ela zamani ilikuwa inatumwa Posta kwa njia ya EMO inachukua wiki au kwa EMS inachukua siku moja akiingiza muamala asubuhi na mapema jioni au kesho yake unapigiwa simu unakwenda kuchukua mkwanja kama una simu ya mezani au unakwenda posta unakuta kikaratasi cha kuchukulia mkwanja (hii ni mpaka miaka ya 90 mpaka mwanzoni mwa 2000.Watu wa kale mlipata sana shida!!!! Kwaio pesa ilikua inatumwa kwa bus
Hali ya barabara ilivyoanza kuwa nzuri ndipo baadhi ya makampuni ya Mabasi yakaanza kutoa huduma ya kutuma fedha na vifurushi kwa kuwa mtu akituma leo anapokea siku hiyo hiyo au kesho yake kutokana na bus limefika muda gani, hii tumekwenda nayo mpaka 2010 hivi kwa baadhi ya maeneo maana huduma za kutuma fedha kwa simu zimeanza 2007/2008 na kwa baadhi ya watu walianza kupitia bank transfer mara baada ya mifumo ya kibenki kuboreshwa kwa uanzishwaji wa ATM maana kumbuka mpaka mwaka 2000 bank nyingi zilikuwa zinatumia vitabu, kabla ya hapo information za mteja zilikuwa zinapatikana kwenye kitabu na bank ukitoa wanaandika na kugonga mhuri na ukienda nje ya tawi lako lazima wafanye mawasiliano na tawi lako ndo unahudumiwa
Ila wewe wa juzi juzi mkuu nadhani umepata akili za utambuzi umekuta Tipopesa, Airtel na Mpesa zinapeta