TBT: Unakumbuka nini enzi ya Ngorika ikitamba?

TBT: Unakumbuka nini enzi ya Ngorika ikitamba?

Asilimia kubwa za madereva wa mabasi ukikaa mbele au siti za mbele utatamani uhamishwe

Hiyo ya kuachia usukani niseme ni kawaida niliwah kupanda simba ikapita bagamoyo dereva anachat kabisa wasap wanagongeana na konda akaenda ingia kwenye shimo tulitoka ubungo saa tisa lakini nilifika home tanga saa saba za usiku
Kumbe we mtoto wa Tanga mashaallah Madame S
 
Nilikata ticket ya kwenda Arusha, lakini nilishukia Mkata.
Mwendo wao ulikuwa hatari. Koswakoswa nyingi. In short it was a risky travel.
Nilisubiria Sumry za Mbeya nikaendelea na safari yangu
Sumry! Yale yalikuwa majeneza yatembeayo, kuna siku mabasi yao matatu yalipata ajali, moja Mtwara, jingine Mikumi na huko Mbeya, hicho ndicho kilisababisha kifo cha Sumry, siku hizi mzee Sumry analima mahindi Sumbawanga.
 
Jamaa walikua noma nakumbuka Mbezi Luis wapiga debe walikua wanabet nani atakua wa kwanza kufika Kati ya Ngorika na Buffalo. Kuna siku niliingia A town saa saba mchana!
Saba mchana A town?
Kuna mRume ndago alishawahi kuingia Mbeya Saba mchana akitokea Dar. Km 850
 
Kuna chuma moja zilikuwa zinaitwa shabaha, kwa juu zilikuwa na muonekano kama wa ndege hizi za kupaa na mabawa yake, wacha kabisa
 
Kwa sie wahenga tunakumbuka zaidi Sawaya, Makundi, Mkwema, Mapande, etc
 
Sasa hivi watoto ni kama wamegawana magari, kila mmoja anamiliki brand yake.
 
Nakumbuka enzii hizo nasoma A level Tanga ilikuwaa lazim nipand hizoo chuma na bro flani ivi alikuwa ni agent so nilikuwa napata siti ya staff pale nakula story za bob dere na konda huku dereva aking'oa mihogo taratibuu kutoka moshi to jiji la mahabaaa

N:B Tangaa ntarud tenaa wallah PCB ilinibana sanaa those dayz nikashindwa kula mema ya nchi😋😋
 
Ndege hii nilikua naipanda sana...ile iliyokuwa imeandikwa macedonia ni hatari sana, mpinzani wake alikua Buffalo na Chakito longway....

Wamekula sana elf 50 kwa kuingia stand kama bus za kwanza
Ww kweli umeipita ile njia... Hizo ngoma zilikuwa hatr
 
Hivi kutoka dar-Arusha zilikuwa zinatumia masaa mangapi?maana kuna basi liliitwa kikondo Mbeya iliingia saa7 na nusu kutoka Dar!
 
Back
Top Bottom