TBT: Unakumbuka nini enzi ya Ngorika ikitamba?

TBT: Unakumbuka nini enzi ya Ngorika ikitamba?

Nakumbuka Sana enzi hizo nikisafiri kutoka Moshi kwenda Dar kushangaa wakati wa likizo ya mwezi wa sita. Nilikuwa naipandia Machame road pale machine tools. Mwili wote ulikuwa unasisimka Kwa furaha na raha ya kusafiri kwenda mjini. Tulikula chips Mombo niliporudi bushi nilielezea nilivyokula chicken chips, Usiombe walitamani kusafiri na wao lakini basi tu
 
Macedonia
Armathaya,dothan,sidon,macedonia,nangai,
51840534_323579111629867_7713317071181267975_n.jpeg
 
Macedonia iyo
2010 nishawahi dandia ngorika moja pale Mombo nikiwa nakuja Dar ilikuwa inaendeshwa na mtu mwenye asili ya kiarabu kama sijakosea. Siku hiyo bus zilikuwa shida hivo ikanilazimu nikae kwenye kitanda pale karibu na mrangoni na kwa dereva aisee jamaa alikuwa anaendesha gari balaa afu walikuwa wanapiga story na kondakta wake sasa unakuta inafika kipindi akawa anajisahau kabisa anaachia usukani mara apeane tano na konda wake. Nilipofika ubungo nikasema ahsante Mungu kwa kufika salama ila nilijiapiza sitakuja kupanda ngorika tena
 
Mimi hii nilikua niita Ngorika mchafu... naipanda sana Moshi Dar, siku ilipata ajali wana wakapiga simu kama nipo hai, siku hiyo nilichelewa nikaikosa ikala mzinga ikaua rafiki yangu.
 
Ngorika ile Macedonia ilikuwa noma, kuna siku nilipanda Moshi kuja Dar, ilikuwa inakwenda kama Ndege, kuna Mzungu alinyanyuka akaenda kuchungulia Speed Meter, sikujua alimaanisha nn ?
 
Kuna ile nyingine Bennedict ilikuwa hatari, kuna siku niliipanda, kufika Moshi wakafaulisha abiria woote wa njiani tukabaki wa Arusha tuu, hapo ukaanza mchuano na buffallo wa nani atakuwa wa kwanza kuingia Arusha ilikuwa hatari mno hapo katikati na ngorika ikawa ya kwanza
 
Ngorika Chatco Hatco Kimotco Osaka Mberesero Chakito ni mabasi ya ukoo mmoja wazee Charles Temba Mberesero
Charles ni mtoto wa Mberesero, kuna Fransis amefariki nikiwa chuo yule mwenye zebra hotel. Ngorika ndio ya ukoo. Hayo mengine ni ya watoto mbali na kwamba wamegombana wakagawana. Kuna freys pia. Dada yao alisimamia akaanza upendeleo yule wa Tanga ndo vurugu yakapaki. Mfano kimotco ni ya marehem Fransis.
 
Back
Top Bottom