TBT: Unakumbuka nini enzi ya Ngorika ikitamba?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,701
45,035
Wale wadau wa ruti ya Arusha Dar, unakumbuka nini enzi mabasi ya Ngorika yakitamba?

Ulishawahi kusafiri na kampuni hii? Kama kuna lolote tushirikishane, tukumbushane!

Karibuni
6e71d40e6d232bb7eaa82bfa07fe43ce.jpeg
 
My brother alikua anasoma Kibaha that time. Akimis ngorika au Buffalo hashuki Dar n'goo! Atadanganya lolote wazee wamuelewe hata kuzuga tumbo la kuhara.
Ukizingatia tulikua tunakaa mbali na mjini nauli kama elfu moja hivi, wazazi wanakua wapole tuu aondoke kesho yake. Hii siri nilikua naijua Mimi tuu
 
2010 nishawahi dandia ngorika moja pale Mombo nikiwa nakuja Dar ilikuwa inaendeshwa na mtu mwenye asili ya kiarabu kama sijakosea. Siku hiyo bus zilikuwa shida hivyo ikanilazimu nikae kwenye kitanda pale karibu na mlangoni na kwa dereva. Aisee jamaa alikuwa anaendesha gari balaa afu walikuwa wanapiga story na kondakta wake sasa unakuta inafika kipindi akawa anajisahau kabisa anaachia usukani mara apeane tano na konda wake. Nilipofika Ubungo nikasema ahsante Mungu kwa kufika salama ila nilijiapiza sitakuja kupanda ngorika tena
 
Hivi hii kampuni ya shabaha express imefia wapi, sitasahau ilipiga mzinga ikamuua mshkaji wangu
 
Hivi hii kampuni ya shabaha express imefia wapi, sitasahau ilipiga mzinga ikamuua mshkaji wangu
Kampuni Nyingi Zimekufa Kitambo
Royal Sumaye
Basi Zote Zilikuwa Engine Nyuma Kuna Kipindi Zilikuwa Tishio Hadi Kwenye Usafiri Wa Anga
Yaani Ilikuwa Ukiipanda Hiyo Bus Raha Sana
 
Asilimia kubwa za madereva wa mabasi ukikaa mbele au siti za mbele utatamani uhamishwe

Hiyo ya kuachia usukani niseme ni kawaida niliwahi kupanda simba ikapita Bagamoyo dereva anachat kabisa wasap wanagongeana na konda akaenda ingia kwenye shimo tulitoka Ubungo saa tisa lakini nilifika home Tanga saa saba za usiku
2010 nishawahi dandia ngorika moja pale Mombo nikiwa nakuja Dar ilikuwa inaendeshwa na mtu mwenye asili ya kiarabu kama sijakosea. Siku hiyo bus zilikuwa shida hivo ikanilazimu nikae kwenye kitanda pale karibu na mrangoni na kwa dereva aisee jamaa alikuwa anaendesha gari balaa afu walikuwa wanapiga story na kondakta wake sasa unakuta inafika kipindi akawa anajisahau kabisa anaachia usukani mara apeane tano na konda wake. Nilipofika ubungo nikasema ahsante Mungu kwa kufika salama ila nilijiapiza sitakuja kupanda ngorika tena
 
Back
Top Bottom