...TBS yakamata mipira ya kiume (condom) fake!

...TBS yakamata mipira ya kiume (condom) fake!

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
14,593
Reaction score
5,583
Serikali imewataka wananchi kuwa makini kutokana na uwepo wa condom fake za kiume zilizoingizwa KINYEMELA NCHINI TANZANIA tokea INDIA, condom hizo zinaitwa MELTME

SOSI: EATV
 
Tumezoea maneno yao. Kitu ambacho kimeingizwa nchini bila ya kutoa ten percent lazima kiwe fake wanakikosesha baraka zao. Subiri wiki ijayo utakisikia hizo ndio kondom bomba
 
sasa wanaposema zimeingia kinyemela sijui wanamaanisha nini?kazi hii ni ya TBS AU TFDA?

Hii ndiyo Bongo bwana! Eti: ''serikali imewataka wananchi wawe makini''! mambo ya ajabu haya!
sasa wananchi watajuaje kuwa 'MELT ME' kuwa ni fake? Watu wangapi wanaangalia EAST AFRICAN TV!
 
ARv fake condom fake nchi hii inaelekea wapi.Hii inaziirisha ni jinsi gani mipaka yetu ilivyo wazi.
 
viongozi wanalia, wananchi wanalia, taifa linaangamia. nafikiri kwamba hizo condom zilipitia TBS na kukaguliwa na mamlaka huska. sasa inakuwaje serikali hiyohiyo itutangazie kuwa ni feki na zimeingia kinyemela? nionavyo mimi mamlaka husika zinapashwa kuwajibika.
 
huu ni udhaifu wa taasisi zetu za ukaguzi na rushwa ,zimepitaje wakati pale kitengo cha tbs ,tfda na maofisa wapo pale watoe tamko kama zilirushwa juu kabla rungu halijawashukia
 
Fake Condoms+fake ARVs+fake makalio+fake waganga wa kienyeji wa kuongeza nguvu za kiume na mvuto wa mapenzi+fake guest houses+fake polisi+.....=?

The country is so unique with citizen of magic and leaders of high pathetic!!!!!!
 
Katika taarifa ya habari ya Channel ten ya saa moja usiku leo, tarehe 21 Dec, kuna taarifa kuwa Condoms aina ya MELT ME toka INDIA ni feki na hazifai kutumiwa. Sote tunajua kuwa condom ndiyo kinga pekee iliyobaki baada ya A (kuacha ngono) na B (kuwa muaminifu) kukosa nguvu. Sasa kama condom zenyewe zinaingia feki, ni sawa na kufanya ngono zembe. Kupata HIV na magonjwa mengine na ngono ni nje nje. Ninachojiuliza hapa ni kuwa Tanzania tuna mkosi gani, hivi mjuzi zimeripotiwa ARV feki, leo Condo feki; Tutafika pale alipopasema JK - Tanzania bila Ukimwi inawezekana?
 
Duh!tumekwisha,kama mimi napendaga sana kutumia kondomu!
 
lol..hili jina tu lenyewe..
 
nashangaa sijui kwa nini Jk pango lake haliishi pale magogoni tubadilishe mpangaji.
 
bora watuletee na ukimwi feki, labda tutapumua.!
 
Back
Top Bottom