Katika taarifa ya habari ya Channel ten ya saa moja usiku leo, tarehe 21 Dec, kuna taarifa kuwa Condoms aina ya MELT ME toka INDIA ni feki na hazifai kutumiwa. Sote tunajua kuwa condom ndiyo kinga pekee iliyobaki baada ya A (kuacha ngono) na B (kuwa muaminifu) kukosa nguvu. Sasa kama condom zenyewe zinaingia feki, ni sawa na kufanya ngono zembe. Kupata HIV na magonjwa mengine na ngono ni nje nje. Ninachojiuliza hapa ni kuwa Tanzania tuna mkosi gani, hivi mjuzi zimeripotiwa ARV feki, leo Condo feki; Tutafika pale alipopasema JK - Tanzania bila Ukimwi inawezekana?