Hivi mkuu ni nini kipo nyuma ya hii picha yako kila ukifanya ku-reply hapa unaituma?Tulia tu hatuna tbs tuna wajinga fulani hivi wapiga diliView attachment 2024983
Mkuu hat nakosa hata cha kukujibu labd nikujibu tu kikawaida ni utaratibu tu niliojiwekea maana nikisema nikupe maelezo kwa kina nitapoteza maan ya uzi wa mdauHivi mkuu ni nini kipo nyuma ya hii picha yako kila ukifanya ku-reply hapa unaituma?
Nadhani huyo ni moja wapo ya mental cases zilizovamia JF hivi karibuniHivi mkuu ni nini kipo nyuma ya hii picha yako kila ukifanya ku-reply hapa unaituma?
Wanajipanga na uchaguzi kwanza. Hata mwaka haujaisha tangu tufante uchafuzi mkuu lakini tayari wanaaanda ujao tenaHakuna kiongozi anayefikiria mambo magumu kama haya!
Viongozi wengi wamekuwa brainwashed wanachofikiria zaidi ni chaguzi zijazo na teuzi basi!
Sio kweli maana hiyo mitumba inauzwa bei kubwa kuliko hata taulo za Urafiki kutoka kiwandani. Issue sio umaskiniSioni mantiki ya malalamiko ya waswahili kwa sababu sisi Tunapenda bidhaa za bei rahisi pengine ni kulingana na uwezo wetu.
Nchi ambayo bado mitumba hata ya taulo, vyupi nk ni dili ni nchi masikini na yenye Watu wasiojitambua. Kuwauzia bidhaa feki haiepukiki
Ni lini ulinunua tishet 60000?au kadet 75000?bidhaa original zipo ila hatuzimudu bei na mfanyibiashara anaangalia walaji wanataka nini kulingana na uwezo wao.
As long as tbs imejaa watu wa Chama fulani maarufu. The rest mtajuana wenyewe.Kwenye vipodozi ndio kabisa. Madukani vipo vipodozi feki na hatarishi kabisa kwa afya ya binadamu.
Sisi tunapooenda sokoni tunakutana na bidhaa tunaamini vimepolita kwenye mamlaka sa ukaguzi na uchunguzi. Unataka mnunuzi atembee na Xray scanner??Tatizo ni wanunuzi
Vibaya mnoo😅😅 Hata iwe ya bei kubwa majanga ni yale yaleUpande wa nguo ndio shida
Nguo unanunua leo ukifua TU tayari ishafubaa wale wazee wa kadeti nadhan tunaelewana hapa
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Business is all about demand and supply forcesMara kadhaa, watu mbalimbali wamekuwa wakihoji uwezo wa TBS katika kuhakikisha ubora wa viwango vya bidhaa wanazopewa Watanzania.
Kuhusu TBS, mara kadhaa, tumeuliza:
1) Je, haina utalaam?
2) Haina maadili?
3) Au haina vifaa?
Leo, kila mahali, zimezagaa bidhaa duni kabisa kutoka China. Bidhaa za China zisizo na ubora, ni balaa kubwa kwa uchumi wa Afrika.
Kwa upande mwingine, wanaouhujumu uchumi wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla ni wafanyabiashara. China, bidhaa zenye ubora ni zile zinazotengenezwa na makampuni ya Ulaya na America, yaliyowekeza nchini China, ambazo soko lake kubwa huwa ni huko huko Ulaya na America. Makampuni mengi ya China, yanayomilikiwa na Wachina, ndiyo yanayotengeneza bidaa duni za kuiga, ambazo soko lake ni Afrika. Bidhaa hizi ni janga kwa uchumi na ustawi wa Afrika, ni bidhaa zinazoua uchumi wa Afrika.
Wafanyabiashara wa Tanzania, ndio wanaoenda kununua bidhaa kwenye makampuni hayo ya wachina yanayotengeneza bidhaa duni, na kuzileta Tanzania. Bidhaa hizi ni za viwango duni sana, na zinaua uchumi wa Tanzania na Afrika, huku zikiitajirisha China. Huu ni wizi wa wazi unaofanywa na Serikali ya China kwa Waafrika. Huu ni wizi wa kidola. Kwa nini nchi ya China iruhusu makampuni yanayotengeneza bidhaa fake? Kwa nini iruhusu bidhaa hizi duni kusafirisgwa kuja Afrika? Ina maana Serikali ya China imeruhusu uharamia huu dhidi ya Afrika?
Jambo la kusikitisha, siku hizi, karibia maduka yote yamejaa hizi bidhaa duni toka China. Kwenye baadhi ya miji, unazunguka maduka yote, hakuna duka hata moja ambalo lina bidhaa kutoka mataifa mengine.
Ushauri kwa wafanyabiashara, baadhi yenu agizeni bidhaa toka mataifa kama Japan, Singapore, Hong Kong, Malaysia, UK, Germany, US, au bidhaa zilizotengenezwa nchini China kwenye makampuni ya kutoka Ulaya na America, hakika mtapata wateja wengi, waliochoshwa na hizi bidhaa duni za makampuni ya Kichina.
Serikali iamke, idhibiti ubora wa bidhaa toka China. Serikali iangalie uwezo wa TBS kiutaalam na kiutendaji. Kwa utendaji wake wa sasa taasisi hii ya TBS haina maana yoyote kwa Watanzania.
Sasa hivi siyo kadeti tu, hata mashati.Upande wa nguo ndio shida
Nguo unanunua leo ukifua TU tayari ishafubaa wale wazee wa kadeti nadhan tunaelewana hapa
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app