TBS na Wafanyabiashara Hawawatendei Haki Watanzania

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Mara kadhaa, watu mbalimbali wamekuwa wakihoji uwezo wa TBS katika kuhakikisha ubora wa viwango vya bidhaa wanazopewa Watanzania.

Kuhusu TBS, mara kadhaa, tumeuliza:

1) Je, haina utalaam?
2) Haina maadili?
3) Au haina vifaa?

Leo, kila mahali, zimezagaa bidhaa duni kabisa kutoka China. Bidhaa za China zisizo na ubora, ni balaa kubwa kwa uchumi wa Afrika.

Kwa upande mwingine, wanaouhujumu uchumi wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla ni wafanyabiashara. China, bidhaa zenye ubora ni zile zinazotengenezwa na makampuni ya Ulaya na America, yaliyowekeza nchini China, ambazo soko lake kubwa huwa ni huko huko Ulaya na America. Makampuni mengi ya China, yanayomilikiwa na Wachina, ndiyo yanayotengeneza bidaa duni za kuiga, ambazo soko lake ni Afrika. Bidhaa hizi ni janga kwa uchumi na ustawi wa Afrika, ni bidhaa zinazoua uchumi wa Afrika.

Wafanyabiashara wa Tanzania, ndio wanaoenda kununua bidhaa kwenye makampuni hayo ya wachina yanayotengeneza bidhaa duni, na kuzileta Tanzania. Bidhaa hizi ni za viwango duni sana, na zinaua uchumi wa Tanzania na Afrika, huku zikiitajirisha China. Huu ni wizi wa wazi unaofanywa na Serikali ya China kwa Waafrika. Huu ni wizi wa kidola. Kwa nini nchi ya China iruhusu makampuni yanayotengeneza bidhaa fake? Kwa nini iruhusu bidhaa hizi duni kusafirisgwa kuja Afrika? Ina maana Serikali ya China imeruhusu uharamia huu dhidi ya Afrika?

Jambo la kusikitisha, siku hizi, karibia maduka yote yamejaa hizi bidhaa duni toka China. Kwenye baadhi ya miji, unazunguka maduka yote, hakuna duka hata moja ambalo lina bidhaa kutoka mataifa mengine.

Ushauri kwa wafanyabiashara, baadhi yenu agizeni bidhaa toka mataifa kama Japan, Singapore, Hong Kong, Malaysia, UK, Germany, US, au bidhaa zilizotengenezwa nchini China kwenye makampuni ya kutoka Ulaya na America, hakika mtapata wateja wengi, waliochoshwa na hizi bidhaa duni za makampuni ya Kichina.

Serikali iamke, idhibiti ubora wa bidhaa toka China. Serikali iangalie uwezo wa TBS kiutaalam na kiutendaji. Kwa utendaji wake wa sasa taasisi hii ya TBS haina maana yoyote kwa Watanzania.
 
mr bann

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
668
1,000
Tulia tu hatuna tbs tuna wajinga fulani hivi wapiga dili
SGN_11_26_2021_1637934876563.jpg
 
Iringakwanza

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
782
1,000
Mchina ni taifa muhimu sana kwetu bila mchina unazani hali ingekuwaje pale kariakoo mchina anakutengenezea simu ndogo inauzwa elfu 40 lakini wewe hiy simu utaweza kukaanayo zaidi ya miaka miwili
 
mr bann

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
668
1,000
Hivi mkuu ni nini kipo nyuma ya hii picha yako kila ukifanya ku-reply hapa unaituma?
Mkuu hat nakosa hata cha kukujibu labd nikujibu tu kikawaida ni utaratibu tu niliojiwekea maana nikisema nikupe maelezo kwa kina nitapoteza maan ya uzi wa mdau
 
Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,979
2,000
Sioni mantiki ya malalamiko ya waswahili kwa sababu sisi Tunapenda bidhaa za bei rahisi pengine ni kulingana na uwezo wetu.
Nchi ambayo bado mitumba hata ya taulo, vyupi nk ni dili ni nchi masikini na yenye Watu wasiojitambua. Kuwauzia bidhaa feki haiepukiki
Ni lini ulinunua tishet 60000?au kadet 75000?bidhaa original zipo ila hatuzimudu bei na mfanyibiashara anaangalia walaji wanataka nini kulingana na uwezo wao.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,603

Sio kweli maana hiyo mitumba inauzwa bei kubwa kuliko hata taulo za Urafiki kutoka kiwandani. Issue sio umaskini
 
yusufuj

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
279
500
Mara kadhaa, watu mbalimbali wamekuwa wakihoji uwezo wa TBS katika kuhakikisha ubora wa viwango vya bidhaa wanazopewa Watanzania.

Kuhusu TBS, mara kadhaa, tumeuliza:

1) Je, haina utalaam?
2) Haina maadili?
3) Au haina vifaa?

Leo, kila mahali, zimezagaa bidhaa duni kabisa kutoka China. Bidhaa za China zisizo na ubora, ni balaa kubwa kwa uchumi wa Afrika.

Kwa upande mwingine, wanaouhujumu uchumi wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla ni wafanyabiashara. China, bidhaa zenye ubora ni zile zinazotengenezwa na makampuni ya Ulaya na America, yaliyowekeza nchini China, ambazo soko lake kubwa huwa ni huko huko Ulaya na America. Makampuni mengi ya China, yanayomilikiwa na Wachina, ndiyo yanayotengeneza bidaa duni za kuiga, ambazo soko lake ni Afrika. Bidhaa hizi ni janga kwa uchumi na ustawi wa Afrika, ni bidhaa zinazoua uchumi wa Afrika.

Wafanyabiashara wa Tanzania, ndio wanaoenda kununua bidhaa kwenye makampuni hayo ya wachina yanayotengeneza bidhaa duni, na kuzileta Tanzania. Bidhaa hizi ni za viwango duni sana, na zinaua uchumi wa Tanzania na Afrika, huku zikiitajirisha China. Huu ni wizi wa wazi unaofanywa na Serikali ya China kwa Waafrika. Huu ni wizi wa kidola. Kwa nini nchi ya China iruhusu makampuni yanayotengeneza bidhaa fake? Kwa nini iruhusu bidhaa hizi duni kusafirisgwa kuja Afrika? Ina maana Serikali ya China imeruhusu uharamia huu dhidi ya Afrika?

Jambo la kusikitisha, siku hizi, karibia maduka yote yamejaa hizi bidhaa duni toka China. Kwenye baadhi ya miji, unazunguka maduka yote, hakuna duka hata moja ambalo lina bidhaa kutoka mataifa mengine.

Ushauri kwa wafanyabiashara, baadhi yenu agizeni bidhaa toka mataifa kama Japan, Singapore, Hong Kong, Malaysia, UK, Germany, US, au bidhaa zilizotengenezwa nchini China kwenye makampuni ya kutoka Ulaya na America, hakika mtapata wateja wengi, waliochoshwa na hizi bidhaa duni za makampuni ya Kichina.

Serikali iamke, idhibiti ubora wa bidhaa toka China. Serikali iangalie uwezo wa TBS kiutaalam na kiutendaji. Kwa utendaji wake wa sasa taasisi hii ya TBS haina maana yoyote kwa Watanzania.
Business is all about demand and supply forces
Chinese companies produce poor quality goods because there is a readily available market for them
Our institutions for quality control and fair competition e.g TBS, FCC are not doing their work properly
Consumers in general do not understand their rights
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
32,212
2,000
China kila bidhaa zipo.nzuri na mbaya ni wewe tu chaguo lako.
tbs wakikaza wafanyabiashara wengi watalia
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Upande wa nguo ndio shida

Nguo unanunua leo ukifua TU tayari ishafubaa wale wazee wa kadeti nadhan tunaelewana hapa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Sasa hivi siyo kadeti tu, hata mashati.

Mwezi uliopita nilinunua shati Morogoro. Shati lilikuwa jeupe, lenye mistari myekundu. Nikiwa nimevaa, muda wa mchana, mwenzangu niliyekuwa naye, akaniambia, una damu kwenye kwapa. Kumbe jasho lilipotoka kidogo tu kwapani, mistari myekundu ikaanza kusambaza rangi nyekundu kwenye sehemu nyeupe. Nilinunua sh 25,000. Mpaka leo sijalivaa tena, nadhani nikienda kijijini, nitawapa jamaa zangu litaweza kuwafaa kama shati la kuvaa kwenda shambani.

Kwa kweli bidhaa za China, kiasi kikibwa ni takataka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom