- Thread starter
- #21
Siyo kweli.Sioni mantiki ya malalamiko ya waswahili kwa sababu sisi Tunapenda bidhaa za bei rahisi pengine ni kulingana na uwezo wetu.
Nchi ambayo bado mitumba hata ya taulo, vyupi nk ni dili ni nchi masikini na yenye Watu wasiojitambua. Kuwauzia bidhaa feki haiepukiki
Ni lini ulinunua tishet 60000?au kadet 75000?bidhaa original zipo ila hatuzimudu bei na mfanyibiashara anaangalia walaji wanataka nini kulingana na uwezo wao.
Leo hii ukitaka vifaa vya umeme vya kutoka Japan, UK, Germany, Brazil, US, siyo rahisi kuvipata. Zimejaa takataka za China.
Kwangu mimi na wengi wenye kujitambua, ni aheri ninunue kitu kwa laki 2 kinachodumu miaka mitano kuliko ununue kitu toka China kwa sh laki 1, halafu kikadumu miezi 6.
Bidhaa za China, katika uhalisia ni aghali sana. Maana unaweza kununua kiatu sh 90,000 ukavaa miezi miwili tu, kimeachia sole, wakati Italy original 200,000 unakaa nacho miaka 6. Ioi ni aghali katika viatu hivyo viwili?