Mara kadhaa, watu mbalimbali wamekuwa wakihoji uwezo wa TBS katika kuhakikisha ubora wa viwango vya bidhaa wanazopewa Watanzania.
Kuhusu TBS, mara kadhaa, tumeuliza:
1) Je, haina utalaam?
2) Haina maadili?
3) Au haina vifaa?
Leo, kila mahali, zimezagaa bidhaa duni kabisa kutoka China. Bidhaa za China zisizo na ubora, ni balaa kubwa kwa uchumi wa Afrika.
Kwa upande mwingine, wanaouhujumu uchumi wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla ni wafanyabiashara. China, bidhaa zenye ubora ni zile zinazotengenezwa na makampuni ya Ulaya na America, yaliyowekeza nchini China, ambazo soko lake kubwa huwa ni huko huko Ulaya na America. Makampuni mengi ya China, yanayomilikiwa na Wachina, ndiyo yanayotengeneza bidaa duni za kuiga, ambazo soko lake ni Afrika. Bidhaa hizi ni janga kwa uchumi na ustawi wa Afrika, ni bidhaa zinazoua uchumi wa Afrika.
Wafanyabiashara wa Tanzania, ndio wanaoenda kununua bidhaa kwenye makampuni hayo ya wachina yanayotengeneza bidhaa duni, na kuzileta Tanzania. Bidhaa hizi ni za viwango duni sana, na zinaua uchumi wa Tanzania na Afrika, huku zikiitajirisha China. Huu ni wizi wa wazi unaofanywa na Serikali ya China kwa Waafrika. Huu ni wizi wa kidola. Kwa nini nchi ya China iruhusu makampuni yanayotengeneza bidhaa fake? Kwa nini iruhusu bidhaa hizi duni kusafirisgwa kuja Afrika? Ina maana Serikali ya China imeruhusu uharamia huu dhidi ya Afrika?
Jambo la kusikitisha, siku hizi, karibia maduka yote yamejaa hizi bidhaa duni toka China. Kwenye baadhi ya miji, unazunguka maduka yote, hakuna duka hata moja ambalo lina bidhaa kutoka mataifa mengine.
Ushauri kwa wafanyabiashara, baadhi yenu agizeni bidhaa toka mataifa kama Japan, Singapore, Hong Kong, Malaysia, UK, Germany, US, au bidhaa zilizotengenezwa nchini China kwenye makampuni ya kutoka Ulaya na America, hakika mtapata wateja wengi, waliochoshwa na hizi bidhaa duni za makampuni ya Kichina.
Serikali iamke, idhibiti ubora wa bidhaa toka China. Serikali iangalie uwezo wa TBS kiutaalam na kiutendaji. Kwa utendaji wake wa sasa taasisi hii ya TBS haina maana yoyote kwa Watanzania.