TBS na Wafanyabiashara Hawawatendei Haki Watanzania

Zanaco

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,500
2,000
Japan, Singapore, Hong Kong, Malaysia, UK, Germany, US,

Ukileta bidhaa kutoka kwenye nchi tajwa utapiga nazo picha Watu wamechoka pesa awana ndio Maana wafanyabiashara wanaingia bidhaa fake bei kitonga weki Moja unarudi kumunua kitu kile kile nadhani tatizo ni uchumi mbovu bora bidhaa used ya nchi tajwa hapo juu kuliko mzigo feki uliko kariakoo
 
Zanaco

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,500
2,000
Makampun Kama national Panasonic Toshiba Honda Yaham ukuzikuta kariakoo zichunguze vizuri utakuta copy bidhaa OG kwenye soko la Africa ni mtihani sana mchina kalijambia soko na bidhaa fake
 
nG'aMBu

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
1,814
2,000
Kadeti n balaa
Sema zile original zipo sema bei Sasa kuanzia 40 hv
Duuh, umenikumbusha pale quality centre, kuna duka nilinunua kadeti elf75, nimekaa na ile kadeki miaka 5 na nikagawa, mm ni heri ninunue kitu original bei kubwa kuliko kununua haya malonyalonya
 
Zanaco

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,500
2,000
Sioni mantiki ya malalamiko ya waswahili kwa sababu sisi Tunapenda bidhaa za bei rahisi pengine ni kulingana na uwezo wetu.
Nchi ambayo bado mitumba hata ya taulo, vyupi nk ni dili ni nchi masikini na yenye Watu wasiojitambua. Kuwauzia bidhaa feki haiepukiki
Ni lini ulinunua tishet 60000?au kadet 75000?bidhaa original zipo ila hatuzimudu bei na mfanyibiashara anaangalia walaji wanataka nini kulingana na uwezo wao.
Asante chukua Kvant hapo kwa mangi nitumie code namba ya lipa kwa simu ninfanyie muamala
 
mr chopa

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
5,297
2,000
Siyo kweli.

Leo hii ukitaka vifaa vya umeme vya kutoka Japan, UK, Germany, Brazil, US, siyo rahisi kuvipata. Zimejaa takataka za China.

Kwangu mimi na wengi wenye kujitambua, ni aheri ninunue kitu kwa laki 2 kinachodumu miaka mitano kuliko ununue kitu toka China kwa sh laki 1, halafu kikadumu miezi 6.

Bidhaa za China, katika uhalisia ni aghali sana. Maana unaweza kununua kiatu sh 90,000 ukavaa miezi miwili tu, kimeachia sole, wakati Italy original 200,000 unakaa nacho miaka 6. Ioi ni aghali katika viatu hivyo viwili?
Ndugu unaishi dunia gani bidhaa Kila aina zipo ni mfuko wako tu ukitaka ya bei rahisi (china) zipo ukitaka bei ghali (mataifa mengine) ni wewe tu na mfuko wako,tena unachagua ni chukue kipi
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,610
2,000
Umaskini wetu uko kuanzia kichwani hadi kwenye uchumi.Wachina hawana makosa maana wao wanachojali ni pesa.shida iko kwetu .
 
Zanaco

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,500
2,000
Nimejikuta nawaza tu. Kwa nini Tanzania kwa shehena ya pamba inayovunwa tusiwe na viwanda vya kadet, tishet, blauzi, mashati, chupi, suti, mashuka, jezi, pedi, pamba za hospitali, makanzu, vest, vitambaa. Tuuze nguo soko la ndani na afrika mashariki na kati na afrika nzima.

Hata kwenye viatu ni hivyohivyo

Tunakwama wapi, je gharama ni kiasi gani?
Import duties zinalipa tunapata pesa chap kwa haraka ukileta habari za viwanda kodi mtazingua kulipa nfano Gari Dogo unaagiza kwa 4m ushuru 7m unataka tuwe na viwanda vyakazigani wakata tunatengeneza faida kuzidi campuny ya Toyota ilotengeza gari
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Viatu ndiyo usiseme nilinunu kiatu nilikivaa toka kariakoo had I mnazi mmoja sori ikachomoka,siku hiyohiyo
Nami kuna siku nilinunua safety boot kwaajili ya kuelekea porini, nikakivaa kabla ya masaa 6 ya kutembea porini, sole ikawa imechanika.

Wachina ni wevi. Ule ni wizi, sawa na wanaowauzia watu vyupa wakiwadanganya ni almasi.

Serikali za Afrika ni vema zikapambana na huu wuzi wa Wachina.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Nimejikuta nawaza tu. Kwa nini Tanzania kwa shehena ya pamba inayovunwa tusiwe na viwanda vya kadet, tishet, blauzi, mashati, chupi, suti, mashuka, jezi, pedi, pamba za hospitali, makanzu, vest, vitambaa. Tuuze nguo soko la ndani na afrika mashariki na kati na afrika nzima.

Hata kwenye viatu ni hivyohivyo

Tunakwama wapi, je gharama ni kiasi gani?
Tatizo kubwa ni sera hovyo za nchi yetu. Ukijenga kiwanda, kwa kiasi kikubwa utaishia kwenye hasara kutokana na msululu wa kodi. Anayeagiza bidhaa hizi mbovu toka China anapata faida kubwa kuliko wewe ukijenga kiwanda hapa nchini.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Hata Marekani yenyewe imejaa bidhaa za China, sasa sijajua hasira zako zinatokea wapi
Plese argue intelligently. Marekani au Ulaya hawanunue bidhaa toka China zinazotengenezwa na viwanda vya wachina. Nchi za Ulaya na America, wananunua bidhaa ziluzotengenezwa China kutoka kwenye viwanda vyao walivyowekeza China, na makampuni yao ndiyo yanayosimamia ubora wa bidhaa hizo. Muwe mnafuatilia mambo yanayoendelea Duniani.

Mnakaririshwa tu kuwa hata Ulaya na America wananunua bidhaa za China, basi bila ya kwenda hatua moja mbele.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
waTZ wanaoenda kuigiza sana,hivi mtu mshahara wa laki5-million,unaweza kumudu kununua suruali ya 70000 na BADO vitu vingine na familia kiujumla,Sisi tukubali mchina anatuweka na sisi ktk ulimwengu wa kisiasa tu Japo ni low quality,Hivi kama si Tecno,Itel na simu nyingi za kichina mpaka leo tungeendelea kwenda internet cafe kulipa jero jero,na Hata TV tungezisikia kwenye bomba huku tukiendelea kujipachinga mitumba mwili mzima tena ile sagurasagura.

Cha muhimu tu tukuzeni viwanda vidogovidogo vya ndani na kuwaezesha Zaid Sido,ikiwezekana tuamishe technology ya china na viwanda VYAO kufanyia shughuli zao hapahapa.

Pia kodi za serikali na soko la uhakika liwepo nchini,hopefully tutapunguza maronya walau kudumu hata 3years tu
Sera na sheria zinazosimamia viwanda na kodi, kwa Tanzania ni ovyo kabisa. Kodi 40, nani atajenga kiwanda hapa. Mara sijui OSHA, mara sijui SUGUA, mara ushuru, mara tozo, utampata nani?
 
wajingawatu

JF-Expert Member
Jan 20, 2013
1,762
2,000
Mara kadhaa, watu mbalimbali wamekuwa wakihoji uwezo wa TBS katika kuhakikisha ubora wa viwango vya bidhaa wanazopewa Watanzania.

Kuhusu TBS, mara kadhaa, tumeuliza:

1) Je, haina utalaam?
2) Haina maadili?
3) Au haina vifaa?

Leo, kila mahali, zimezagaa bidhaa duni kabisa kutoka China. Bidhaa za China zisizo na ubora, ni balaa kubwa kwa uchumi wa Afrika.

Kwa upande mwingine, wanaouhujumu uchumi wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla ni wafanyabiashara. China, bidhaa zenye ubora ni zile zinazotengenezwa na makampuni ya Ulaya na America, yaliyowekeza nchini China, ambazo soko lake kubwa huwa ni huko huko Ulaya na America. Makampuni mengi ya China, yanayomilikiwa na Wachina, ndiyo yanayotengeneza bidaa duni za kuiga, ambazo soko lake ni Afrika. Bidhaa hizi ni janga kwa uchumi na ustawi wa Afrika, ni bidhaa zinazoua uchumi wa Afrika.

Wafanyabiashara wa Tanzania, ndio wanaoenda kununua bidhaa kwenye makampuni hayo ya wachina yanayotengeneza bidhaa duni, na kuzileta Tanzania. Bidhaa hizi ni za viwango duni sana, na zinaua uchumi wa Tanzania na Afrika, huku zikiitajirisha China. Huu ni wizi wa wazi unaofanywa na Serikali ya China kwa Waafrika. Huu ni wizi wa kidola. Kwa nini nchi ya China iruhusu makampuni yanayotengeneza bidhaa fake? Kwa nini iruhusu bidhaa hizi duni kusafirisgwa kuja Afrika? Ina maana Serikali ya China imeruhusu uharamia huu dhidi ya Afrika?

Jambo la kusikitisha, siku hizi, karibia maduka yote yamejaa hizi bidhaa duni toka China. Kwenye baadhi ya miji, unazunguka maduka yote, hakuna duka hata moja ambalo lina bidhaa kutoka mataifa mengine.

Ushauri kwa wafanyabiashara, baadhi yenu agizeni bidhaa toka mataifa kama Japan, Singapore, Hong Kong, Malaysia, UK, Germany, US, au bidhaa zilizotengenezwa nchini China kwenye makampuni ya kutoka Ulaya na America, hakika mtapata wateja wengi, waliochoshwa na hizi bidhaa duni za makampuni ya Kichina.

Serikali iamke, idhibiti ubora wa bidhaa toka China. Serikali iangalie uwezo wa TBS kiutaalam na kiutendaji. Kwa utendaji wake wa sasa taasisi hii ya TBS haina maana yoyote kwa Watanzania.
Siyo bidhaa za china tu hata zinzotengenezwa hapa nchini nazo ni za kichina china pia. Angalia ubora wa msomari wa inchi tatu, urefu na unene wake ni sawa na inchi mbili na nusu. Nondo ni ft 39 badala ya ft 40., square pipe ft 19 badala ya 20., bati zinapata kutu baada ya miezi mitatu. TBS wapo tu
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
7,244
2,000
Nami kuna siku nilinunua safety boot kwaajili ya kuelekea porini, nikakivaa kabla ya masaa 6 ya kutembea porini, sole ikawa imechanika.

Wachina ni wevi. Ule ni wizi, sawa na wanaowauzia watu vyupa wakiwadanganya ni almasi.

Serikali za Afrika ni vema zikapambana na huu wuzi wa Wachina.
Nikweli kabisa
 
Gemima20

Senior Member
Dec 15, 2019
106
225
Nami kuna siku nilinunua safety boot kwaajili ya kuelekea porini, nikakivaa kabla ya masaa 6 ya kutembea porini, sole ikawa imechanika.

Wachina ni wevi. Ule ni wizi, sawa na wanaowauzia watu vyupa wakiwadanganya ni almasi.

Serikali za Afrika ni vema zikapambana na huu wuzi wa Wachina.
usinikumbushe ungonjwa wa moyo nafytua tofali za biashara kutumia umeme wa Generator nilinunua generators tatu ndani ya miezi mitano migenerator ya kichina inabugia wese na mikelele alafu inatoa umeme kidogo ,pesa ya mkopo nilitaka kupata kichaa simu yangu ilijaa namba za mafundi generator Unachukua pesa za oda ya tofali mwisho pesa unazitema bilakutaka

Nilisaidiwa na jamaa moja aliniunganisha na jamaa wanasafirisha mizigo kutoka Japana nikanunua Gereretor kva 30 la Deny la mtumba huu nimwaka wa tatu linatumia diesel kidogo sana linatoa umeme mwingi zaid ya vot 400 three phase kwa moto mdogo sana bila mikelele,kazi yangu ni kumwaga oil kila baada ya masaa kuenea kazi nyepesi usiku na mchana linafanya kazi vizuri

Jambo la kushangaza bidhaa za mtumba zimewekewa kodi kubwa sana ukilinganisha na feki mpya.

bidhaa feki ni utapeli tunapigwa serekali ingalie upya tunatiana umasikini vibaya mno.
 
Ungeliwaza umeme wa jua japo sijajua nguvu ya vifaa unavyotumia
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Siyo bidhaa za china tu hata zinzotengenezwa hapa nchini nazo ni za kichina china pia. Angalia ubora wa msomari wa inchi tatu, urefu na unene wake ni sawa na inchi mbili na nusu. Nondo ni ft 39 badala ya ft 40., square pipe ft 19 badala ya 20., bati zinapata kutu baada ya miezi mitatu. TBS wapo tu
Upo sahihi kabisa. Msumari wa inchi 2, zamani usingweza kuupindisha kwa mkono. Leo msumari wa inchi 6, nondo ya milimita 16, unakunja kwa mkono.

Lakini nondo ya UK, hata ya milimita 8 hukunji kwa mkono.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
usinikumbushe ungonjwa wa moyo nafytua tofali za biashara kutumia umeme wa Generator nilinunua generators tatu ndani ya miezi mitano migenerator ya kichina inabugia wese na mikelele alafu inatoa umeme kidogo ,pesa ya mkopo nilitaka kupata kichaa simu yangu ilijaa namba za mafundi generator Unachukua pesa za oda ya tofali mwisho pesa unazitema bilakutaka

Nilisaidiwa na jamaa moja aliniunganisha na jamaa wanasafirisha mizigo kutoka Japana nikanunua Gereretor kva 30 la Deny la mtumba huu nimwaka wa tatu linatumia diesel kidogo sana linatoa umeme mwingi zaid ya vot 400 three phase kwa moto mdogo sana bila mikelele,kazi yangu ni kumwaga oil kila baada ya masaa kuenea kazi nyepesi usiku na mchana linafanya kazi vizuri

Jambo la kushangaza bidhaa za mtumba zimewekewa kodi kubwa sana ukilinganisha na feki mpya.

bidhaa feki ni utapeli tunapigwa serekali ingalie upya tunatiana umasikini vibaya mno.
Pole sana ndugu yangu. China ni kaburi la kumzikia mwafrika. Watu hawajatambua. Ukitaka ufilisike, uwe maskini, nunua mashine za China, na ziwe ndiyo determinant ya mafanikio yako, lazima ufilisike.

Ni aheri ununue mashine used ya Japan, UK, Germany au US, utafanya kazi kwa utulivu wa akili na moyo. Utaumizwa na bei ya kununulia lakini baadabya hapo utatulia kusubiria matunda.

Kuna rafiki yangu aliwahi kununua plant ya kutengenezea kokoto toka China, kila mwezi anafanya order ya vipuli ilihali jiranibyake aliyenunua mitambo used toka Uholanzi, ametulia akitengeneza hela. Aliyenunua mchina, anahangaika ili angalao apate hela kiasi fulani aagize mtambo used, lakini pesa haikusanyiki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom