Mtimti
JF-Expert Member
- Feb 23, 2008
- 942
- 644
Nimesoma taarifa kuwa TBS wamewapa tenda kampuni ya SERENGETI GLOBAL SERVICE ya London kuwa wakaguzi wa magari yote yanayotoka uingereza na kuyatoza gharama ya dola za kimarekani 200. Nikiwa kama mkazi wa Uingereza na nikiwa kama mdau wa usafirishaji wa magari nasema wazi kuwa hiki kitu hakikubaliki, na ni kutuletea usumbufu usio na sababu sisi watanzania tunaokaa mbali London. Tbs inaonesha hawajui wanachokifanya au wameshinikizwa kuwapa tenda Serengeti kwa sababu za kisiasa au wanaendeleza upuuzi waowaliofanya siku za nyuma hapa uingereza.
Kipindi cha nyuma magari yalikuwa yanasafirishwa bila kukaguliwa,baada ya Tbs kuanzisha utaratibu wa magari kutoka nje yanayoingizwa Tanzania yawe yamekaguliwa ndipo hapa Uingereza deal hilo akapewa mtoto wa aliyekuwa mkurugenzi wa TBS (Mamamutabazi(R.I.P)), huyu kijana alikuwa ana kiofisi chake London hivyo ukiwa nagari yako unataka kusafirisha na upon nje ya London ulikuwa unamtafuta kwa simu na mnalipana kisha anakutumia cheti. Hivyo kulikuwa hakuna ukaguzi wowote bali ni ulaji tu alikuwa amepewa kijana . baada ya miaka kadhaa TBS walimnyima huyujamaa kutoa hii huduma .
Kwanini sikubaliani na TBS kuwapa zabuni hii(sijui kama kweli wameshinda tenda au wamewapa tu kama walivyompa mtoto wa mama mutabazi)
Magari yote yanayokuja t Tanzania kutoka u Uingereza huwa lazima yawe na M.O.T(ministry transport test), hii inakuwa nitest kwa gari yako kama ina viwango vya usalama barabarani na usalama wa mazingira, maana kuna mitambo ambayo ni computerized inayolipima gari lako kuanzia engine mpk moshi inaouzalisha kisha unapewa certificate kutoka DVLA(driver and vehicle licensing agency), hawa dvla ndio wanaotoa leseni zote za udereva hapa uingereza. Hivyo basi hapa utaona kuwa magari yote yanayokuja Tanzania kutoka uingereza huwa yana viwango na yanafaa kwa matumizi ya barabarani maana hakuna mtu anayenunua gari ambayo haijapass MOT
Kwanini Serengetihawakidhi vigezo?
Serengeti hawana mtambo wa ukaguzi wa gari tofauti na ukaguzi unaofanywa na mawakala wanaofanya MOT hapa uingereza. Mitambo wanayotumia na cheti watakachotoa ni sawa na cheti ntakachopata sehemu yoyote hapa uingereza nikipeleka gari yangu kuifanyia ukaguzi. Hivyo hapa utaona kabisa kuwa TBS wamewapa jamaa njia ya kutuibia pesazetu
Serengeti wana ofisi moja tu tena ipo hapo tilbury(east london) na ina wafanyakazi hawazidi watano,je inaweza kuhudumia kila mtanzania aliyepo kona za uingereza? Kumbuka uingereza ina bandari zaidi ya nne .na kwanini nifuate hii huduma London wakati mi naishi nje ya London na huku nnapoishi kuna bandari na huwa naitumia? Hata kama waoSerengeti wanasema wana mawakala u Uingereza nzima (kitu ambacho si kweli, )basi hao mawakala si ndio hawahawa tunaowatumia kila siku kufanya MOT ambao wao wanachaji pounds 30-50?.....kama kuna ukaguzi wanaofanya ni tofauti na wanavyofanya ukienda kupasisha gari yako kwenye MOT basi chris lukosi aje hapa aseme na mimi ntakuwa wa kwanza kumuomba msamaha
Ushauri wangu kwa serikali na pia watu wenye dhamana basi walikemee hili, serikali ifikie mahali iwe inafikiria njia za kutupunguzia mizigo sisi wananchi tunaoishi nje na sio kutuongezea gharama zisizokuwa na sababu. Ushuru tu wa gari upo juu sana halafu bado hawa TBS wanatuongezea huu upuuzi wa kuwapa watu ulaji kwa kutunyonya kimacho macho.
Hili suala siku si nyingi ntatafuta waandishi na radio stations za Dar ili niliseme vizuri..aksanteni