TBL na Serengeti Bia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBL na Serengeti Bia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Katikomile, Oct 7, 2009.

 1. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Heshima mbele!

  Naomba msaada wenu kuhusiana na ambacho kampuni ya bia Tanzania imekuwa ikifanya kwenye baa za hapa DSM (nafikiri na mkoani pia). TBL wanam-approach mwenye baa na kumuuliza ni faida gani anapata kwa mwezi kwa kuuza bia ya serengeti? Mwenye baa akisema ni Milioni 2 let say, anapewa ofa ya kupewa 4Mil kila mwezi (wanazidisha faida yako mara mbili), mnakubaliana bia ya serengeti kamwe isiuzwe kwenye baa yako.

  Mfano hai kwa walioko DSM. nenda baa ya Maeda pale sinza, barabara ya Mori kuelekea Mlimani City, pale bia ya serengeti haiuzwi na yule Goodluck mwenye baa ana uhakika wa mshiko toka TBL to replace serengeti monthly sales/profit.

  SWALI,

  Je Mwenye baa hapokei rushwa?

  Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission) wanaweza inglia kati.

  AMA ndo ushindani wenyewe wa kibiashara?

  Ikimbukwe pia kwamba TBL wana mgogoro na East African Breweries Ltd (EABL) kuhusiana na bia ya Tusker, kwani EABL wana mpango wa kuipileka bia ya Tusker Serengeti Breweries Ltd.

  Hii migogoro inatutesa wala-KILAJI
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,183
  Trophy Points: 280
  TBL wamefulia na mabia yao mabovu. Si unakumbuka Kibo Breweries walivyowatesa wakaamua kukinunua kiwanda kabisa. Nasikia walikuwa na mkakati wa kuinunua Serengeti Breweries lakini wakagonga mwamba. Serengeti inawatesa si utani. Na kwa hapo, hata waweke mikakati gani, ikibidi serengeti tutaifuata hukohuko kiwandani. Serengeti bia: Achana na hii kitu, inasuuza roho ile mbaya.
   
 3. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45

  Mkuu, kumbe nawe ni mdau wa taifa stars, Serengeti ni noma ati!
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mjasiriamali Shupavu heshima mbele,

  TBL watakuwa hawawatendei haki walaji.

  Mgogoro wa TBL na EABL ni wa siku nyingi kidogo nadhani ulianza wakati EABL waliponunua kiwanda cha KIBO brewaries cha mjini Moshi na TBL nao wakaamua kujenga kiwanda huko Kenya.

  TBL na EABL walikubaliana Kiwanda cha KIBO cha mjini Moshi kimilikiwe na TBL na kile kilichojengwa na TBL Kenya kimilikiwe na EABL .Bila shaka TBL na EABL kila mmoja alitaka kulinda share market yake.

  Wakati deal ya TBL na EABL inafanyika Serengeti brewaries haikuwepo,nadhani TBL baada ya kuichukua KIBO walifikiri wamemaliza adha ya ushindani.EABL bado wanalitamani soko la Tanzania ambalo kwa kiasi kikubwa bado liko wazi sana hivyo wakaamua kupitishia deal yao Serengeti brewaries ambayo wanaitesa sana TBL na bia yao ya Serengeti.

   
 5. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #5
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli TBL wanachofanya sio haki kabisa, wanaweweseka baada ya kuona serengeti bia wapo juu na bia yao ni nzuri sana. pia wamejaribu kuiga Vilta Malta kwani wao kabla walikuwa na malta guiness lakini ilikuwa mbaya sana now wamebadili kuiga Vilta malta.

  TBL wajue kuwa biashara ni ushindani na ushindani hauwi hivyo.
   
 6. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Uongo mbaya Serengeti ina suuza roho. TBL walie tu
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  mE NIKINYWA MABIA YA TBL TUMBO LINANIUMA SANA MPAKA NAHARISHA BORA SERENGETI KWANZA HARUFU YAKE TU SWAAAAFI KWELIKWELI
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,183
  Trophy Points: 280
  Mkuu sehemu ya mshahara wa Marcio Maximo ulitoka kwenye wallet yangu. Achana na ile half litre ya serengeti mkuu. Haina mpinzani kabisa.
   
 9. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Na kwa wale wapenzi wa portable bottle ama wasiopenda kutumia glass, hapo ndo wametupatia kabisa hawa Serengeti, hakuna cha Heineken wala windhoek!

  Ngoja niende lunch nikastua japo kiserengeti kimoja si mbaya kwa afya!
   
 10. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unajua tangu Serngeti inaanza TBL walidharau sana na kuona hawatafika mbali,sasa wameshtuka kuona duh vibwana mdogo vinakuja juu kweli kweli na one brand? sasa wananza visa vya bi mkubwa, ujue makaburu wanataka kuona wao pekee ndio wanongoza kwa kila kitu hapa afica kam si duniani,ukitaka kubisha angalia banks, migodi,shopping malls,yani huwa wanaingia kuuwa viliyopo,sasa hili la mchezo mchafu kuzuia vilaji vya watu is too much, basi watanzania tuwasuse kama hawawezi kuwa na adabu!wanapata hela nyingi sana lakini huwezi amini wafanyakazi wanateseka kifwedha ni noma, wapo wachache wezi kama watu wa makerting,sales basi,kama wataka kujua uliza mfanyakazi ndani ya tbl usikie miyeyusho yake,utakimbia!!
   
 11. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45

  Ama kweli mshika mbili moja humponyoka! serengeti wana brand moja lakini wanatisha kama mabomu ya mbagala!
   
 12. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Sorry, nimetembelea website yao, kumbe hawa jamaa wana brand nyingine kama Stella Artois, the kick na VitaMalt plus.
  http://www.serengetibrew.com/contact.htm
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuna mbinu nyingi za marketing, lakini hii hapa ni mbinu chafu na ya kipumbavu!

  Kwanini wasitafute tu mazingira yatakayofanya wauze products zao kirahisi, kuliko kumzuia muuzaji asiuze?

  Kwa wanywaji wasiobadili misimamo yao ya unywaji wataitafuta bia hiyo hadi waipate, hata kama itawagharimu kutoka Sanawari hadi kwa Morombo!
   
 14. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  yap but brand inayoperform ni serengeti pekee hizo nyingine zinasindikiza tuu,hata jina la company ni serengeti u see?so wakiweza kuzimarket na hizo mbili well tbl watafunga virago
   
 15. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Wadau wa Serengeti, nimepata msg hii toka kwa mkereketwa wa Serenget bia, si vibaya tuka-share!

   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Na umwambie huyu jamaa wa SERENGETI aliyekutumia email awe member wa HAPA JF, aone jinsi watu wanavyosupport Kinywaji yake!

  Na huenda akatusupport kwenye yale mambo yetu ya ``MKONO MTUPU HAURAMBWI`...lol!
   
 17. N

  Nanu JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sio Maeda tu hata pale kwa John Fedha-Kinondoni nao vivyo hivyo!!!!!!!!!!
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Mibia ya TBL inajaza tumbo jamani miaka miwili iliyopita nilikuwa mpenzi wa Kilimanjaro,ukinywa tatu unatafuta Gordon ili ucheue lakini tangu Serengeti Brewaries walipotuletea Serengeti mambo yamekuwa mambo unatandika bia kwa kwenda mbele hakuna cha gesi wala nini.
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Haka kamchezo TBL walikaanza siku nyingi,walitumia mbinu hii pale Amani Bar Njiro juu kidogo ya TEMDO mwenye bar akaanza kupoteza wateja mmoja baada ya mwingine siku hizi hataki kufuata ujinga wa TBL kila brand ya bia anaweka.
   
 20. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbinu ya TBL haina tofauti na mbinu ya chama fulani cha siasa ambacho hununua shahada za kupigia kura. Hongera sana SBL, bia yako ya Serengeti inajiuza.
   
Loading...