Waziri Bashe azikaanga kampuni za TBL, Serengeti. Agomea kukutana nao

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mwandishi wetu,

Waziri wa kilimo nchini, Husein Bashe "amezinyooshea vidole "kampuni za bia za Tanzania Breweries Ltd pamoja na Serengeti kwamba endapo watashindwa kuingia makubaliano na wakulima wa shayiri wasahau kukutana na yeye.

Bashe,alitoa kauli hiyo Jana katika kituo cha utafiti wa kilimo Tari kilichopo Selian mkoani Arusha wakati alipoenda kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho.

Akizungumza katika kituo hicho Bashe alisema kwamba mwaka 2020 kampuni hizo zilifika ofisini kwake kuomba punguzo la kodi kwa ajili ya mradi mkubwa wanaoujenga mkoani Dodoma.

Bashe,alisema kwamba wakiwa ofisini kwake kampuni hizo zilidai kuhangaikia maombi yao kwa kipindi cha miaka sita serikalini bila mafanikio na kuomba awasaidie.

Alisema kwamba kufuatia maombi hayo yeye kama waziri alivutana na wizara ya fedha kwa mwaka mmoja na nusu kupigania maombi yao mpaka yakakubalika lakini wameingia mitini.

" Tumevutana na wizara ya fedha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kupigania hii kesi baada ya kupata wanaleta (games)mchezo "alisema Bashe

Alisisitiza kwamba kampuni hizo zilikubali kununua shayiri kutoka kwa wakulima ambapo TBL walipanga kununua tani 6000 na Serengeti tani 2000 lakini wameenda kinyume na makubaliano.

Hata hivyo,alisema kwamba pamoja na kampuni hizo kuomba kukutana naye Mara kwa Mara lakini hatoweza kuitikia wito huo mpaka pale watakapoingia mkataba na wakulima wa shayiri.

" Wameniomba kukutana nao sitaki kuonana nao waje kwangu wakishaingia mkataba na wakulima yaani narudia they should never(wasirudie)"

"Leo wame withdraw (wamejitoa) kuingia mkataba na wakulima walisema hawajengi mpaka serikali iwape insective (nafuu) Leo serikali imewapa wanasema hawajengi" alisisitiza Bashe

Alipotafutwa meneja wa kampuni ya TBL mkoani Arusha, Joseph Mwaikasu alisema kwamba suala hilo litatolewa ufafanuzi na makao makuu.

Alipotafutwa msemaji wa kampuni ya TBL makao makuu, Mesiya Mwangoka alijibu kwa kifupi "no comment".

Mwisho.

IMG-20220131-WA0014.jpeg
IMG_20220131_141606_169.JPG
IMG_20220131_141426_225.JPG
 
TBL wana utamaduni wa kuharibu/kuhujumu viwanda vya ndani.

Mfano halisi ni namna walivyokiua kiwanda cha chibuku yaani DarBrew LTD,mitambo iko salama kabisa lakini wanatoa hoja eti kiliwatia hasara.

Kiwanda kiliendeshwa kwa faida sana na mwekezaji wa mwanzo ila wao TBL wanatumia hoja ya kuwa hakina faida ili kiuzwe na wao wanunue ili wapate eneo la pale...shida yao ni eneo tu na wala hawajali watanzania walio wengi ambao wangenufaika na ajira n.k.

Baadhi ya Watendaji wa jiji la Ilala wanahusika na hujuma hizo...soon nitawataja kwa majina na kwa ushahidi ktk uzi wangu wa hivi karibuni.
 
Pia amesema atavifungia viwanda vyote vya Beer, wines, Spirit na pombe za kienyeji kwasababu UISLAM hauruhusu matumizi yake

Na amegoma kukutana na wamiliki wa viwanda hivyo kwaajili ya majadiliano.
Kwahili, maza atamfaya suni...🤨.... Maana walevi tutahama nchi
 
TBL wana utamaduni wa kuharibu/kuhujumu viwanda vya ndani.

Mfano halisi ni namna walivyokiua kiwanda cha chibuku yaani DarBrew LTD,mitambo iko salama kabisa lakini wanatoa hoja eti kiliwatia hasara.

Kiwanda kiliendeshwa kwa faida sana na mwekezaji wa mwanzo ila wao TBL wanatumia hoja ya kuwa hakina faida ili kiuzwe na wao wanunue ili wapate eneo la pale...shida yao ni eneo tu na wala hawajali watanzania walio wengi ambao wangenufaika na ajira n.k.

Baadhi ya Watendaji wa jiji la Ilala wanahusika na hujuma hizo...soon nitawataja kwa majina na kwa ushahidi ktk uzi wangu wa hivi karibuni.
Jaziaga nyama basi Mkuu
 
Sometimes wawekezaji kutoka nje huua viwanda vya ndani kwa mtindo huo. Hununua viwanda shindani na kisha kuviua au kuvitelekeza nk. Ili kuwe na fair competition, hawakutakiwa kupewa kile kiwanda.
 
TBL wana utamaduni wa kuharibu/kuhujumu viwanda vya ndani.

Mfano halisi ni namna walivyokiua kiwanda cha chibuku yaani DarBrew LTD,mitambo iko salama kabisa lakini wanatoa hoja eti kiliwatia hasara.

Kiwanda kiliendeshwa kwa faida sana na mwekezaji wa mwanzo ila wao TBL wanatumia hoja ya kuwa hakina faida ili kiuzwe na wao wanunue ili wapate eneo la pale...shida yao ni eneo tu na wala hawajali watanzania walio wengi ambao wangenufaika na ajira n.k.

Baadhi ya Watendaji wa jiji la Ilala wanahusika na hujuma hizo...soon nitawataja kwa majina na kwa ushahidi ktk uzi wangu wa hivi karibuni.
Lete mambo tuwasagie kunguni hawatujali kbs sisi walala hoi
 
Bashe kukataa kuonana na hao wenye viwanda sio suluhisho la tatizo!! Angekuwa na busara angewasikiliza matatizo yao na hao “ contract “ farmers na kuona sababu za kutofautiana kwao!! Huko nyuma Hawa wakulima si walikuwa wanawalimia shayiri kwa mikataba, sasa kuna kitu gani hakijaenda sawa? Kuwapatia hizo exemptions toka Treasury isiwe sababu ya kuwakandamiza!!

Bashe asitake sifa za kijimga za kujionesha kuwa na yeye yupo; kumbuka Hawa TBL na Serengeti Breweries ni walipa kodi na waajiri wakubwa nchini hivyo usidhani kuwa Samia atakusifia kwa kuwamishandle!! Usije jikuta unarudi kwa boss wako Rostam!!
 
Pia amesema atavifungia viwanda vyote vya Beer, wines, Spirit na pombe za kienyeji kwasababu UISLAM hauruhusu matumizi yake

Na amegoma kukutana na wamiliki wa viwanda hivyo kwaajili ya majadiliano.
Uislamu unakupa shida sana
 
Nafikiri kabla ya kuyafokea Makampuni angaengalia kwanza ubora wa shairi inayolimwa na hao Wakulima inatimiza vigezo? Aanzie kwa Wakulima kwanza !
Uko sahihi Mkuu, je, shayiri ina kiwango kinachohitajika na viwanda vya pombe??
Au naye yupo kuweka mazingira tu ya vikundi vya watu fulani wenye mashamba Yao Makete, Mbeya, n.k

Huyo naye anajifagilia Tu kisiasa aonekane alitoa matamko mengi kama chiriku Ummy kule afya.

Kuna matatizo makubwa wizarani kwake alipaswa kuja na suluhisho! Ni kama kapata pa kujifichia!
Kuna uhaba wa MBOLEA, MBOLEA inauzwa laki, wakulima tunalima mwaka huu, tuna wakati mgumu.
 
Pia amesema atavifungia viwanda vyote vya Beer, wines, Spirit na pombe za kienyeji kwasababu UISLAM hauruhusu matumizi yake

Na amegoma kukutana na wamiliki wa viwanda hivyo kwaajili ya majadiliano.
Hata kodi zinazolipwa na viwanda hivyo serikali isizipokee.
 
Alipotafutwa meneja wa kampuni ya TBL mkoani Arusha, Joseph Mwaikasu alisema kwamba suala hilo litatolewa ufafanuzi na makao makuu.

Alipotafutwa msemaji wa kampuni ya TBL makao makuu, Mesiya Mwangoka alijibu kwa kifupi "no comment".
Injili kwa kwenda mbele
 
Mwandishi wetu,

Waziri wa kilimo nchini, Husein Bashe "amezinyooshea vidole "kampuni za bia za Tanzania Breweries Ltd pamoja na Serengeti kwamba endapo watashindwa kuingia makubaliano na wakulima wa shayiri wasahau kukutana na yeye.

Bashe,alitoa kauli hiyo Jana katika kituo cha utafiti wa kilimo Tari kilichopo Selian mkoani Arusha wakati alipoenda kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho.

Akizungumza katika kituo hicho Bashe alisema kwamba mwaka 2020 kampuni hizo zilifika ofisini kwake kuomba punguzo la kodi kwa ajili ya mradi mkubwa wanaoujenga mkoani Dodoma.

Bashe,alisema kwamba wakiwa ofisini kwake kampuni hizo zilidai kuhangaikia maombi yao kwa kipindi cha miaka sita serikalini bila mafanikio na kuomba awasaidie.

Alisema kwamba kufuatia maombi hayo yeye kama waziri alivutana na wizara ya fedha kwa mwaka mmoja na nusu kupigania maombi yao mpaka yakakubalika lakini wameingia mitini.

" Tumevutana na wizara ya fedha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kupigania hii kesi baada ya kupata wanaleta (games)mchezo "alisema Bashe

Alisisitiza kwamba kampuni hizo zilikubali kununua shayiri kutoka kwa wakulima ambapo TBL walipanga kununua tani 6000 na Serengeti tani 2000 lakini wameenda kinyume na makubaliano.

Hata hivyo,alisema kwamba pamoja na kampuni hizo kuomba kukutana naye Mara kwa Mara lakini hatoweza kuitikia wito huo mpaka pale watakapoingia mkataba na wakulima wa shayiri.

" Wameniomba kukutana nao sitaki kuonana nao waje kwangu wakishaingia mkataba na wakulima yaani narudia they should never(wasirudie)"

"Leo wame withdraw (wamejitoa) kuingia mkataba na wakulima walisema hawajengi mpaka serikali iwape insective (nafuu) Leo serikali imewapa wanasema hawajengi" alisisitiza Bashe

Alipotafutwa meneja wa kampuni ya TBL mkoani Arusha, Joseph Mwaikasu alisema kwamba suala hilo litatolewa ufafanuzi na makao makuu.

Alipotafutwa msemaji wa kampuni ya TBL makao makuu, Mesiya Mwangoka alijibu kwa kifupi "no comment".

Mwisho.

Hawa jamaa wanajiamini sana sababu ya sisi walevi. Ngoja niache kunywa muelewe
 
Nchi hii kuna maeneo wananchi watavumilia maji yakikosekana Ila siyo 🍻🍺

Itakuwa vitaaaa😃
 
Back
Top Bottom