TBL na Serengeti Bia

Bila shaka na wewe umathirika sana na hii huduma ya serengeti mkuu Balantanda!

Umeona mwananchi ya leo wanavyojaribu kutu-fool hawa TBL, ama kweli wameishiwa. Kizuri chajiuza bwana, wanalalamika eti Serengeti haipaki rangi kwenye mabaa kama ofa kwa wamiliki na kutoa mafunzo kwa wahudumu ndio maana haiuzwi, WHAT A SHIT! Pumba tupu, CHUI anachanja mbuga haitaji promo Za majitaka!

Hizo ni dalili kwamba TBL wameshindwa Vita ya ushindani na SBL.Cha msingi wakae chini na kujiuliza ni wapi wamekwama/wameshindwa badala ya kutumia hizo MBINU CHAFU kabisa ambazo haziruhusiw/hazitakiwi katika USHINDANI HURU wa kibiashara(kama vp wabadilishe watu wote wa kwenye vitengo vyao vya masoko maana waliopo tayari wameonesha kushindwa,wameshindwa kuitumia elimu yao/wanaidhalilisha TAALUMA yao kwa kutumia MBINU chafu kama hizi,hao akaina SHELUKINDO&co waondolewe,wawekwe wengine) otherwise hawatafika mbali,SBL itazidi kupaa na kupaa na wao(TBL) watazidi kufulia....Taratibu naliona ANGUKO la TBL
 
Ukisoma kwa uangalifu lile tangazo la gazeti la Mwanachi leo utaona kuwa ni inside plot ya kampuni moja ya bia dhidi ya nyingine. Wafanyabiashara wa mabaa Dar hawana umoja wao, hawana viongozi, hawajawahi kufanya mkutano hata siku moja kuzungumzia hali hii. Sana sana huwa wanakaribishwa na makampuni hayo kwenye tafrija mbalimbali zinzotayarishwa na makampuni hayo. Walikaa lini wakakubaliana kuandika yaliyoandikwa kwenye tangazo hilo?

Kama wangekuwa na umoja na wakafanya mkutano na kutoa azimio la kuandika tangazo kama linavyoonekana kenye gazeti la Mwananchi leo ingekuwa habari, isingekuwepo haja ya kutoa tangazo.
Alichokifanya mwandishi wa tangazo hili ni kutumia Kiswahili kibovu kisicho na mpangilio imara ili ionekane kuwa limeandikwa na wafanyabiashara wasio na elimu ya kutosha.​

Labda wazee wa media advertising watuletee gharama za kutoa tangazo hilo full page ya Mwananchi. Kweli wenye baa walipe pesa?????? Kwa uchungu gani while on the ground, Serengeti is the leading selling beer brand now? Hata sisi wanywaji tunalitambua hilo, nenda kakae kaunta jaribu kumpeleleza mtu wa kaunta ama hata mhudumu uone. Utasikia Serengeti na Tusker! Na hili ndo linawaumiza vichwa Makaburu kwani soon Tusker nayo itakuwa chini ya SBL, patamu hapo!
 
Heshima mbele!

Naomba msaada wenu kuhusiana na ambacho kampuni ya bia Tanzania imekuwa ikifanya kwenye baa za hapa DSM (nafikiri na mkoani pia). TBL wanam-approach mwenye baa na kumuuliza ni faida gani anapata kwa mwezi kwa kuuza bia ya serengeti? Mwenye baa akisema ni Milioni 2 let say, anapewa ofa ya kupewa 4Mil kila mwezi (wanazidisha faida yako mara mbili), mnakubaliana bia ya serengeti kamwe isiuzwe kwenye baa yako.

Mfano hai kwa walioko DSM. nenda baa ya Maeda pale sinza, barabara ya Mori kuelekea Mlimani City, pale bia ya serengeti haiuzwi na yule Goodluck mwenye baa ana uhakika wa mshiko toka TBL to replace serengeti monthly sales/profit.

SWALI,

Je Mwenye baa hapokei rushwa?

Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission) wanaweza inglia kati.

AMA ndo ushindani wenyewe wa kibiashara?

Ikimbukwe pia kwamba TBL wana mgogoro na East African Breweries Ltd (EABL) kuhusiana na bia ya Tusker, kwani EABL wana mpango wa kuipileka bia ya Tusker Serengeti Breweries Ltd.

Hii migogoro inatutesa wala-KILAJI

Hosea achana na Mwakyembe komaa na hawa Makaburu wa pale Ilala!
 
Wakuu,
Nimemaliza kusoma malalamiko (kutapatapa) kwa "Wamiliki wa Baa" na tangazo lao. Kimsingi ni utoto tu unaowasumbua TBL, kudhani kwamba wanaweza kuwahadaa Watanzania kwa mamilioni, kwamba waliotoa tangazo hilo ni wamiliki wa baa. Kuna masuala kadhaa nimeyaona katika tangazo hilo!

1. Wamekwepa kabisa kugusia kwa undani kiini cha tatizo ambalo ni ushindani usio wa haki, mwisho wake wamebaki kuongelea ushindani wa Pepsi na Coca Cola kila aya, wametoa hoja dhaifu mno za kujitetea. Hoja za majokofu yasiyo na vinywaji vya SBL kuwa ni hasara dhaifu mno!
2. Watoa tangazo (wamiliki wa baa) hawajaweka anuani zao wala baa zao ambazo wanadai wanazitetea, ili tujue ukweli ulipo. Hakika mimi ningeenda ktk baa hizo. Suala la kila baa kuwa na wastani wa matangazo 44 kila moja si la kweli kabisa, nikichukulia mfano wa baa kubwa 5 maeneo ya Mwenge na Sinza
3. Promotional materials zinazowekwa katika baa zao zinatoka makampuni yote ya vinywaji, lakini wao hawaliongelei hili suala kwa uwazi zaidi ya kulalamika kwamba SBL hawawapi hizo materials, kitu ambacho si kweli kabisa.
4. Jirani zetu Wakenya wametukanwa bila sababu za msingi (kama kweli zipo), kwamba walikuwa wanauza bia zenye kondom zilizotumika (kipengele namba 3, aya ya 2). Kwa hoja hii, kwa nini bia hizo chafu wasingezifikisha polisi ili wahusika wachukuliwe hatua.

TBL wanapaswa kujua kwamba Watanzania tumeelimika, hatuwezi kununuliwa kwa hoja zisizo na mshiko km ilivyo katika tangazo lao la leo, ambalo wametumia jina la WAMILIKI WA BAA (ambazo hazijatajwa majina popote katika tangazo hilo, wala zilipo katika Jamhuri hii)
 
tena wanatumia lugha chafu kwenye tangazo mi nawashauri sbl wafikishe tena suala hili kwa FCC na baraza la habari la taifa kwa vile tangazo linachochea vurugu na kuhatarisha amani. na kwa hili tangazo hawa wenye baa ndio wamkubali kabisa na wamethibitisha kununuliwa.

hebu tujiulize hawa wenye baa mbona hakuna logo ya chama na mwenyekiti hajasaini tangazo? huu si uhuni tu? kwanza nasikia huu muungano ni wa baa za ilala tu maana mimi rafiki zangu wana baa mbezi beach na hawamo! na nasikia member ni 70 tu sasa dar peke yake tuna baa na vioski kama 4000...hii ni asilimia ngapi? si ni hawa tu ambao ndio wamenunuliwa?

jamani tuamke SBL msikate tamaa piganeni hii ni vita
 
halafu suala la kibo leo nimebahatika kuongea na jamaa wa kibo zamani, hebu tuangalia KIBO imeuliwa na nani? TBL au EABL?

TBL walipewa KIBO na wakaiua within 24hrs watu wote SBL ikawachukua hii haikuwa kampuni ya kenya, wanatapatapa.na wakati huo kina mareale wlikuwa wanaongoza kuchafua bia za kibo na kuweka condom na vitu vichafu kwani nani hajui

wamefilisika kifikra na nawaonea huruma hawatafika mbali...ila hili la tangazo ni uvunjifu wa amani mbona hao waliotoa tangazo wasijitokeze front
 
halafu suala la kibo leo nimebahatika kuongea na jamaa wa kibo zamani, hebu tuangalia KIBO imeuliwa na nani? TBL au EABL?

TBL walipewa KIBO na wakaiua within 24hrs watu wote SBL ikawachukua hii haikuwa kampuni ya kenya, wanatapatapa.na wakati huo kina mareale wlikuwa wanaongoza kuchafua bia za kibo na kuweka condom na vitu vichafu kwani nani hajui

wamefilisika kifikra na nawaonea huruma hawatafika mbali...ila hili la tangazo ni uvunjifu wa amani mbona hao waliotoa tangazo wasijitokeze front

Tupe data mkuu, mbane huyo ex-Kibo akupe data za kutosha. EABL nao inabidi wa-react dhidi ya hizi kashfa!
 
Nami pia nimelisoma the Guardian la leo lina hiyo press release ya Bar owners. Kwa mtazamo wangu ni kuwa pamoja na ukweli wa ushindani but sitafurahi sana kufanya biashara na wakenya (have shares on Serengeti).Huwa wanatuchukia sana na hawana mapenzi mema kwa Tanzania.

Na ninakuhakikishia kuwa the so called East Africa Cooperation (Tz, Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi) haitastawi. Nina uhakika huu. Niliwahi kuwa Kenya kwa Muda, Wakenya hawataki kabisa kuona Tz inafurukuta, tena from the high authority perspective!!!

At the sametime, hatutakaa tufaudike na huu muungano wa nchi 5. Tena tusipokuwa makini tutapoteza amani na uhuru wetu.
 
Back
Top Bottom