TBL na Serengeti Bia

now you guys are talking mimi nafikiri tuanzishe kampeni maana watu wakikosa bia kwenye baa moje watahamia kwingine. TBL inabidi waende shule kujifunza jinsi ya kusoma alama za nyakati. wakati wa apartheid umekwisha maana huu ukaburu ndio walikuwa waiitumia kabla ya uhuru wa SA.

inabidi waelewe watanzania wameenda shule watawadanganya hao hao wadogo na wenye baa kujiharibia wenyewe. Nimesikia SBL wakiingia ubia na DIAGEO/EABL products zao zitakuwa Johny Walker zote red/black/blue na green, baileys, vat 69, smirnoff vodca, smirnoff ice, captain morgan, tusker, white cap light, white cap, alvaro, malta guiness na mazagazaga mengine

SBL watatisha maana nasikia pamoja na taifa stars Tusker project fame itakuwa yao, tusker cup yao, malta street dancer yao..kasheshe watu watajinyonga humu!


Sasa SBL mtanikamata vizuri make huko kwenye spirit nako nipo na karibu mna brand zote nipendazo.

Mkuu Kidumempiganaji, vipi kuhusu Mohans? Si ndo muuzaji wa vitu hivi au hana exclusive right?
 
TBL wamefulia na mabia yao mabovu. Si unakumbuka Kibo Breweries walivyowatesa wakaamua kukinunua kiwanda kabisa. Nasikia walikuwa na mkakati wa kuinunua Serengeti Breweries lakini wakagonga mwamba. Serengeti inawatesa si utani. Na kwa hapo, hata waweke mikakati gani, ikibidi serengeti tutaifuata hukohuko kiwandani. Serengeti bia: Achana na hii kitu, inasuuza roho ile mbaya.

Ewaaaa Mkuu. Ubarikiwe. Achana na kojozi la serengeti. Full kuchamba koo.
 
Heshima mbele!

Naomba msaada wenu kuhusiana na ambacho kampuni ya bia Tanzania imekuwa ikifanya kwenye baa za hapa DSM (nafikiri na mkoani pia). TBL wanam-approach mwenye baa na kumuuliza ni faida gani anapata kwa mwezi kwa kuuza bia ya serengeti? Mwenye baa akisema ni Milioni 2 let say, anapewa ofa ya kupewa 4Mil kila mwezi (wanazidisha faida yako mara mbili), mnakubaliana bia ya serengeti kamwe isiuzwe kwenye baa yako.

Mfano hai kwa walioko DSM. nenda baa ya Maeda pale sinza, barabara ya Mori kuelekea Mlimani City, pale bia ya serengeti haiuzwi na yule Goodluck mwenye baa ana uhakika wa mshiko toka TBL to replace serengeti monthly sales/profit.

SWALI,

Je Mwenye baa hapokei rushwa?

Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission) wanaweza inglia kati.

AMA ndo ushindani wenyewe wa kibiashara?

Ikimbukwe pia kwamba TBL wana mgogoro na East African Breweries Ltd (EABL) kuhusiana na bia ya Tusker, kwani EABL wana mpango wa kuipileka bia ya Tusker Serengeti Breweries Ltd.

Hii migogoro inatutesa wala-KILAJI


Acheni kunywa mabeer yanaharibu afya kwa kuleta vitambi, kwanini msiwe kama mimi

whisky_range.jpg



Ama

flavored-rum-konyagi-200.jpg
 
Yatawashinda TBL tu mimi naamini ushindani mzuri sio kuzibiana ila ni kuongeza ubora full stop, haya mengine ni kuweweseka tu
 
Acheni kunywa mabeer yanaharibu afya kwa kuleta vitambi, kwanini msiwe kama mimi

whisky_range.jpg



Ama

flavored-rum-konyagi-200.jpg

Kwa kiingereza changu cha shule ya kata, nakumbuka hivi vimaneno...........The pudding of the food lies in eating and the beauty of the thing is in the eyes of the beholder!
 
Mkuu,

Duh kumbe wewe tupo jirani?

Hivi hili jina Nyamachabez lilitokana na nini? Kuna mtaa hapa unaitwa Hugo Chavez, yawezekena hii Chabez = Chavez?

Anyways Serengeti ina aroma kama ya RUBISI na kwa hakika inanikumbusha Karagwe Kaisho

SBL - Kazi Nzuri, jihadhari na mafisadi

Inawezekana, si unajua tena yale maeneo yanaitwa Nyaishozi. Mitaa ya kwetu ile swahiba.
 
na jana nilikuwa hongera baa sinza hamna, tukaenda topland bar magomeni hola, tukahamia highway bar nako patupu kasheshe hupati Chui kafichika! ila nafikiri akitoka huyu chui atauma sana watu. Chuiiiiiii uko wapi

TBL wamefulia na fire extinguishers zao, CHUI anatisha. Uzuri wa chui, kuna take away, hata wakizibania uswazi, supermarket zipo kibao hadi kwa Mohans zinapatikana! Wakawaonge basi na shoprite ama samaki samaki!
 
kuna kipindi flani serengeti ilikuwa juu tbl wakaona style ya kuiondoa sokoni ni kuzinunua bia zaserengeti zote kwenye bar mapemaaaaaa asubuhi,kwahiyo ukienda mida ya mchana kupata kilaji unaambiwa serengeti zimeisha,na unaamua kuagiza bia nyingine ambayo itakuwa ya tbl,walifanya hivyo wakiamini kwa muda fulani wa kufanya hivyo wanywaji watazoea kunywa bia yao na kusahau serengeti,lakini iliposhtukiwa hiyo deal,serengeti wakaongeza uzalishaji na usambazaji wa kilaji yao,basi ikawa mkusanyaji wa tbl akipita tu kukusanya,baada ya muda msambazaji wa serengeti anapitisha tena,ikifika jioni tbl na serengeti wote wapo mezani kama kawa, tbl wakaamua kuacha kamchezo.sasa naona wameamua kuja na style nyingine,na hivi wametuharibia kilaji yetu ya ndovu basi watafulia sanaaaaaa
 
Kuna mbinu nyingi za marketing, lakini hii hapa ni mbinu chafu na ya kipumbavu!

Kwanini wasitafute tu mazingira yatakayofanya wauze products zao kirahisi, kuliko kumzuia muuzaji asiuze?

Kwa wanywaji wasiobadili misimamo yao ya unywaji wataitafuta bia hiyo hadi waipate, hata kama itawagharimu kutoka Sanawari hadi kwa Morombo!

sanawari mpaka kwa morombo???????
pale city garden sanawari chui wapo wa kutosha mkuu usihofu
 
kuna kipindi flani serengeti ilikuwa juu tbl wakaona style ya kuiondoa sokoni ni kuzinunua bia zaserengeti zote kwenye bar mapemaaaaaa asubuhi,kwahiyo ukienda mida ya mchana kupata kilaji unaambiwa serengeti zimeisha,na unaamua kuagiza bia nyingine ambayo itakuwa ya tbl,walifanya hivyo wakiamini kwa muda fulani wa kufanya hivyo wanywaji watazoea kunywa bia yao na kusahau serengeti,lakini iliposhtukiwa hiyo deal,serengeti wakaongeza uzalishaji na usambazaji wa kilaji yao,basi ikawa mkusanyaji wa tbl akipita tu kukusanya,baada ya muda msambazaji wa serengeti anapitisha tena,ikifika jioni tbl na serengeti wote wapo mezani kama kawa, tbl wakaamua kuacha kamchezo.sasa naona wameamua kuja na style nyingine,na hivi wametuharibia kilaji yetu ya ndovu basi watafulia sanaaaaaa


Nasikia bia ya ndovu ni uzuri wa mkakasi tu, wameongeza alch kutoka 4.2 to 4.8
 
TBL tabia yao katika competition siyo nzuri hata kidogo. Tukumbuke kuwa waliwahi kuzuia agents wao wasiuze heineken, jamaa wa heineken wakaenda mahakamani TBL wakashindwa kesi.

EABL wamekuja na mpango wa kununua shares serengeti ili waweze kupitisha bia zao pale,TBL wameenda mahakamani. Kama bia ni nzuri waache tu,wateja watachagua. Jamaa wana competition y a kitoto sana.

Jamani wanywa serengeti endeleeni,kwanza TBL walikuwa wanadhamini ligi ya bongo,lakini walivyokuja hawa makaburu wakajitoa. Faida yote wanayopata, hakuna wanachotufanyia watanzania kama namna ya kushare faida. Serengeti tumejionea misaada wanayotoa kwa timu ya taifa. Kama kodi wote wanalipa,ilitakiwa kuwe na kitu cha ziada kama udhamini wa michezo.
 
Kama kweli TBL wanafanya hivyo basi si sahihi. Ila ninachojua ni kwamba sioni tofauti ya TBL na EABL, wote ni wakuja na faida itaenda ama Kenya au Bondeni. Wanaoshabikia EABL kuingia Serengeti wanaupeo mdogo hasa katika hii ushindani wa kuhodhi soko la East Africa. Nimebaki mashabiki tu wa uchumi huku wenzetu Kenya wanakimbia. Leo hii Tanzania kuna Benki ya Kenya, East African Cable ni Wakenya, Wananunua Ardhi kwa bei yeyote ile, moheteli yote ya kitalii ni Wakenya n.k. Tanzania hutufikirii na hata hatuna ubavu wa kuweka kitu Nairobi.

Tuamke jamani - achana na kushabikia ujinga.
 
na jana wameenda lillies pub msasani , nguruko mbezi wamengoa matangazo yanayowaka wakamuoffer meneja 30elfu akakataa wakangoa meneja akalichukua akaliweka yaani hawa watu wamedhamiria kweli inabidi serikali
 
TBL waling'oa mitambo ya Kibo kuipeleka Mbeya mpaka leo zinaoza kwa kushindwa kujenga kutokana na kesi ya kiwanja kuwa mahakamani.
Sasa SBL wanajenga kiwanda Moshi na hii inawaudhi sana TBL hawana raha na wanajuta waliifunga Kibo.
Pia bia ya TBL wameumia zaidi baada ya EABL kuamua Tusker itengenezwe SBL.
Sasa huyu marketing director wao inabidi kwanza afukuzwe kazi na kampuni kushitakiwa kwa CFC.
 
na jana wameenda lillies pub msasani , nguruko mbezi wamengoa matangazo yanayowaka wakamuoffer meneja 30elfu akakataa wakangoa meneja akalichukua akaliweka yaani hawa watu wamedhamiria kweli inabidi serikali

Hii sasa ndo wanaonesha kabisa wamefulia-kimarketing! Yaani wanang'oa mabango wanafikiri tutaihama Serengeti? Mi naona marketing team wameuza timu! hapa lazima refa kaongwa!
 
Hii sasa ndo wanaonesha kabisa wamefulia-kimarketing! Yaani wanang'oa mabango wanafikiri tutaihama Serengeti? Mi naona marketing team wameuza timu! hapa lazima refa kaongwa!


Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti
!
 
Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti!
Serengeti! serengeti!

Kaka nina kaugonjwa kakusahau kidogo! Huu ubeti ni ule wa AKUDO ama tangazo jipya la chui. Ila tuache utani Chui anafunika mkUU!
 
Back
Top Bottom