TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Tulishasema Tanzania hakina Demokrasia na kujishau tu hamkutuelewa. Sasa mnaona CCM inakotupeleka?



Serikali imechukuwa uamuzi sahihi kabisa, ilikuwa inafikia wakati unakwenda ofisini kupata huduma wafanyakazi wamekodoa kwenye luninga wanaangalia Bunge, Nasema SAFI SANA NAPE!
 
Watarudia kuonyesha kuanzia saa nne usiku baada ya kuhaririwa
Nape:

Anatangaza kuwa TBC
itakuwa inatangaza baadhi
ya matukio ya Bunge
Lengo ni kubana
matumizi..


Anasema gharama za kuendesha Bunge zimefikia 4Bln kwa Mwaka.


Anasema kutakuwa na
kipindi maalum kitakachokuwa kinarushwa usiku kuanzia saa 4 hadi 5 Usiku.



.
Sasa hizo pesa za kulipia vipindi vya bunge nadhani ni sehemu ya kodi zetu swali langu ni kuwa je TBC hawapati ruzuku toka serilkalini au nayo imebinafsishwa kama UDA ,na kama wanapata sasa kigugumizi cha nini wakati wananchi ndio wanaiwezesha ? Kuna baadhi ya vipindi havina manufaa kwa jamii na wanavionyesha huwa vinagharamiwa na nani ,au ndo hawataki wananchi waone mawaziri mizigo wakichambuliwa ?
 
Magufuli hawezi ingilia (tumbua) tena hapa, mambo yataenda hivyo hivyo maiaka yote kumi
 
Kama tatizo ni gharama, basi wapunguze posho za wabunge, mawaziri na Makatibu, na mishahara yao pia japo kwa 5%. Itatosha na kubakiwa na kiasi kikubwa cha kuendelea kurusha live kwa miaka miwili mbele.
 
Ngachoka mm wacha waendelee mdu alianzia kwenye kamati za bunge baada ya watu wenye weledi kufichwa kwenye kamati zisizo na mashiko
 
Unaonaje wakiwa wanazima mitambo yote ya simu pia ili uwe unafanya kazi


Hilo nalo ni wazo lkn haliko chini ya uwezo Serikali, hili la Bunge ni rahisi kwa maana Bunge ni chombo cha Serikali na ndiyo kinaamua nani arushe matangazo yake!
 
Chenge amehairisha bunge kuruhusu kamati kujadili TBC kurusha bunge live baada ya upinzani kuhoji uhalali na busara zilizotumika kufikia uamuzi huu.
 
Zama za msoga mtazikumbuka sana maana aliachia watu mkosoe mnavyotaka sasa hapa kazi tuu


Jakaya tutamkumbuka kwa kutoa Uhuru wa kutoa na kupata habari


Hata bunge lilianza kuonyesha 2005 tu..


Hapa Kazi Tu lkn hawataki tuzione hizo kazi zikijadiliwa.
 
Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.

Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.

Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
CCM wako predictable ile mbaya ..,. haya yote yalibashiriwa ... kama kweli serikali ya Magufuli iko kwaajili ya wananchi hofu ya nini?
 
Ndio maana nilikuwa najilazimisha kuikubali hii serekali ya Magufuli ila moyo ukawa unakataa kabisa hii serekali inaweza kuwa ya kidikiteta kwanza bomoa bomoa pili wamezima tbc watu wasione udhaifu wao.. Hata mawaziri alio chagua ni wale wa hovyo tusiowatalajia.. Wallah nawaambia Kikwete alikuwa rais na tutamkumbuka.. Kikwete ambae tulipo lalamika kuhusu mawaziri wake kuwa wabovu aliwapiga chini nakuweka wengine kwa Magufuli hiyo hamna.. Leo tbc juzi mawio kesho sijui nn
 
Kama tatizo ni gharama, basi wapunguze posho za wabunge, mawaziri na Makatibu, na mishahara yao pia japo kwa 5%. Itatosha na kubakiwa na kiasi kikubwa cha kuendelea kurusha live kwa miaka miwili mbele.


Tatizo siyo gharama amesema hivyo ili wavivu msilalamike lkn sababu hasa ni kwamba huu ni muda wa kazi na siyo wa kuangalia luninga, hivyo fanyeni kazi na Bunge mtaliona jioni baada ya kazi au wkend!
 
Safi sana hiki kilikuwa ni kilio changu siku zote, Watu wafanye kazi na waache kuangalia Bunge, mkirudi nyumbani jioni baada yakazi mtaangalia Bunge tani yenu au kama mmechoka hata wkend!

Safi sana W. Nape!
Hebu tingisha kichwa chako kidogo, je unahisi nini?
 
Hii nayo kali aisee
Nmemsikiliza nkachoka
Tv ya Taifa inashindwa kurusha matangazo ya bunge kweli
Hapana aisee hii serikali yaanza nitia shaka
NA Bado Tutasikia Mengi Mno!!! Tusubirie Tu!!! Tehe! Tehe! Tehe!!! KUNA Hidden Ajenda Tu, Huyo Aliyetangaza, Si Ndio Katibu Wa Itikadi Na Uenezi!!!!!??? Ngoja Tusubirie Tuone Na Tusikie!!!!
 
Back
Top Bottom