Yani nimecheka hadi jino la mwisho na mbavu zangu zinauma sana. hakuna tena haja ya kuhangaika na Slaa maana CCM tayari walishamaliza kazi wenyewe kwa kuonesha ni kwa namna gani wanahusika na jambo hili. Jamani hivi kweli Mzee Kinana na akili zako zote za kisiasa umekubali hiki kitu cha kuiua CCM kifanyike mbele ya macho yako kweli?! movie ilikuwa imeenda vizuri sana ila kosa lililofanyika la kushadadia sana hiyo movie tene wazi wazi tayari imefungua watanzania wengi waliokuwa nyuma ya SLAA macho. Timu ya ufundi ya CCM hamjifunzi tu yaliyotokea kwa ZITTO, LIPUMBA na sasa mmerudia kosa hilo hilo kwa SLAA tena?!