Hata waseme vipi, watanzania wanampenda Dr. Slaa, No one will change it.Moyo wa mwanadamu ndivyo ulivyo. Mwaka 2005 kikwete alipendwa sana lakini kipindi chake kimeshapita.Every thing has got an end. For your information kitu ambacho kitazidi kuiangamiza serikali ni kuendeleza propaganda dhidi ya Dr. Slaa.
Jeshi la polisi lisijidanganye kwamba linaweza kujisafisha lenyewe kwa hizo Propoganda zao.Tangu lini Hakimu akajihukumu kwenye kesi yake mwenyewe(Conflict of Interest).Njia Pekee ya kutatua hili swala ni kuundwa kwa Tume huru yakimahakama kufanya uchunguzi wa hili swala na wale wote watakaobainika kuhusika kuua na kujeruhi Mkondo wa Sheria uwaadhibu na kwakufanya ivyo Wananchi Watarudisha Imani ktk Jeshi la Polisi ila Kuingiza Propaganda kwenye swala lililogharimu maisha ya Watu na wengine kusababishiwa Ulemavu wa Maisha hakutawasaidia.
kwa walichofanya pale na ile sinema yao kwa mwenye akili timamu ataelewa mipango yao iliyofanywa na polisi na serikali,ila watambue hawawezi kudanganya watu wa kizazi cha leo kisichodanganyika.
Sasa sitoshangaa mchakachuaji mkuu aka kubwa la maadui aka mlinda mafisadi akatoa kauli.
kumbukeni hata wakisema wawaue au kuwafunga viongozi wa chadema,sio dawa ya kuzuia mabadiliko hata chembe.
Nina uhakika leo hii CDM wapo tayari kwa mdahalo kuhusu suala la Arusha. Je, CCM na polisi yao wapo tayari????
CDM nao wapewe airtym based on TBC questions. otherwise CDM weka matukio yote ya Arusha kwenye CD bila kuedit. Mutauza kukijengea chama uwezo na pia kutupa ujasiri.
chadema walishajulikana ni watu wanaotaka kuleta vurugu na uvunjifu wa amani wa nchi hii.
Sababu za msingi hawana, kuhusu katiba jmk kisha waambia tayari tunashughulikia uundwaji wa tume. Umewashuka.
Kuhusu arusha umeya, mpaka saini zao za mahudhurio ya kumchaguwa meya zipo kwenye kitabu, kuwa walihudhuria, walipoona wanashindwa wakatoka. Mara wameanzisha fujo, wakapigana risasi, kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa chadema wenyewe ama kwa kutumia mbinu za chokochoko ndio waliuwa kwa risasi na kutaka kuisingizia serikali. Umewashuka.
Wanachotaka ni umwagikaji damu, kafara za kanisa kila miaka 50 ni damu ya binadaam.
Dr. Slaa sasa ana chini ya mwaka mmoja tu katika umaarufu huu wa sasa, kumbuka kuwa ata Mtikila na Lyatonga Mrema pia walikuwa na umaarufu miongoni mwa Watanzania na Umaarufu ule wa Mrema bado haujafikiwa na Dr. Slaa mpaka sasa lakini pamoja na umaarufu wao huo kadri muda ulivyokwenda walizidi kuwa irrelevant na kupoteza thamani zao kisiasa, somo hili linajulikana.
Muda mfupi huu baada ya uchaguzi, Dr. Slaa anaanza kupoteza sifa muhimu ya kuisimamia amani ya nchi hii na busara ya uongozi ya kujali maisha ya wafuasi wake, kama ilivyokuwa kwa Mtikila na Mrema ni suala la muda tu kabla hajaonekana kituko katika ulingo wa siasa za Tanzania, wait and see...