TBC yadanganya, hatua stahiki zichukuliwe

TBC yadanganya, hatua stahiki zichukuliwe

Mnaangaishana bure na TBC-CCM.... Inatazamwa mwisho Dar es Salaam.
Jamani kwa nimi mnaifuatilia hiyo substandard TV station...??
 
Sasa wewe mtoa post hilo uliloandika na kichwa chako habari vinaendana?mbona nawe umedanganya??
Hapo TBC imedanganya wapi? Unaboa na hao wafuata upepo wenzako wakakusapoti bila nao kuangalia ulichoandika,sasa wewe hapo ndio umedanganya.
 
Nataka kuona utendaji makini WA TCRA
katika hili. TBC ni mali ya watanzania wote inakuwaje wanaonesha upendeleo huo waziwazi???
 
Wana JF,

Ni kwa kawaida ya serikali kufanya mabadiliko au kuwafukuza wafanyazi wake wenye weledi pindi wakionyesha weledi wao katika kazi kwa ubora wao, lakini huku wanakumbana na shinikizo nyingi kutoka serikalini, kama vile kupindisha habari, kukuza habari zisizo habari na kudanganya ikitokea , watangazaji, wanahabari waratibu wa habari huwa wana wakati mgumu wa kufukuzwa kazi kipindi cha uchaguzi ikiwa wataenda tofauti na maelekezo ya kutoka kitengo.

My Take.
Hatujui safari hii watamfukuza nani maana lowasa ndio katawala media, huku nyuma yake wakuu wa nchi wakisema huo ni moto wa mabua utazima, tu, hayo ni makapi yatakauka tu.

Tiddo Mhando sasa hivi anaipaisha Azam, TBC imebaki kama Makumbusho.
 
Sasa wewe mtoa post hilo uliloandika na kichwa chako habari vinaendana?mbona nawe umedanganya??
Hapo TBC imedanganya wapi? Unaboa na hao wafuata upepo wenzako wakakusapoti bila nao kuangalia ulichoandika,sasa wewe hapo ndio umedanganya.
usijitoe ufahamu...ni kweli alipodai ''habari zilizopewa kipaumbele'' ndio hizo alizosoma ?
 
Hata hayo magazeti yenyewe yameandikwa kishabiki mno. Si kila kinachoandikwa lazima kisomwe
 
Maskiini wanatia huruma watangazaj wa TBC kwa kutetea kitumbua chao kisiingie mchanga
 
Sasa wewe mtoa post hilo uliloandika na kichwa chako habari vinaendana?mbona nawe umedanganya??
Hapo TBC imedanganya wapi? Unaboa na hao wafuata upepo wenzako wakakusapoti bila nao kuangalia ulichoandika,sasa wewe hapo ndio umedanganya.

wewe ulijitoa ufahamu,hv ukiwa ccm mpaka uwe mjinga au uweke akili zako kando?unajua maana ya habari zilizopewa uzito?Kwenye gazeti habari huwa inapewaje uzito?Huoni msomaji anasema habari zilizopewa uzito halafu anasoma vimaandishi vidogo vya habari za pembeni wakati maandishi makubwa yaliyobeba picha akiyakwepa!Huo huoni ni udanganyifu?
 
Mkuu hii habari imenichekesha sana. yaani mtangazaji anaiona kabisa habari iliyopewa kipau mbele lakini anasoma vingine. na wasiwasi huyo atakuwa mwana chadema. maana kwa staili hiyo anaipromote chadema kuliko kuiangamiza. maana kama ni TV kila anayetazama anaiona hiyo habari lakini mtangazaji anasoma kingine. hili suala itabidi nianze kulifikiria kwa upande wapili wa shilingi.

Ila tofauti ya TBC na ITV ni kuwa ITV walidanganya wakati TBC hawakuripoti.
 
Ni kweli kabisa mkuu.

Mm nimeona TBC1 na SIMU. tv kupitia TBC1.
Habari kuu: SHIKAMOO LOWASSA, MAFURIKO MBEYA, POLISI YASHINDWA KUZUIA MAFURIKO YA LOWASSA.

Alikuwa hazisomi anatafta habari zingine ndogondogo za juu ya Magazeti husika. Ni bora tu wasisome Magazeti ijulikane Moja.

HILI NI SHIRIKA LA UMMA SI MALI YA CCM!
Huu ni UKUDA TBC1
 
Hata hayo magazeti yenyewe yameandikwa kishabiki mno. Si kila kinachoandikwa lazima kisomwe

Kama magazeti yameandika kitu ambacho si sahihi pia kuna chombo cha kuyashughulikia, sema walipokosea nao wapewe adhabu stahiki.
 
Uyo mtangazaji nae zuzu kweli, au hajui hiyo ni tv station na si radio?😦😦
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom