Ni kodi zetu wanazitumia.
Tuna haki ya kuhoji.
Utahoji kitu ambacho hakihojiki Bavaria?Hapa kwetu hakuna UHURU wa vyama vya upinzani.Na ukiwa mpinzani unaonekana ni hayawani,mlevi,hujitambui,kibaka,muhuni tu,msaliti ukiangalia kwa UNDANI system yenyewe yaani Serikali,Polisi,Jeshi,Tiss pamoja na wanachama wa CCM bado hawaoni kama vyama vya upinzani ni haki kupewa nafasi yoyote.
Wengi wa hawa wanona ukisupport upinzani humuenzi Baba wa Taifa (Mwl.JKN) kwa hiyo hiyo ndiyo inayozidi kudumaza siasa za vyama vingi.Chuki zimejijenga hasa kwa chama tawala.Angalia viongozi wakuu wanvyoongea,wasomi wetu,utamsikia mtu oh mimi CCM ndiyo imenisomesha,ukimuuliza sasa tufanyeje?
Ufisadi,rushwa na ubadhirifu wa mali za umma unaoendelea ndani ya serikali ya CCM watu hawauoni!!!!!!!!Inanishangaza wizi wa ESCROW wahusika wote wamepeta kwenye Ubunge,leo tumebaki kumnanga mtu aliyekosea miaka nane iliyopita,halafu hawa wengine tunasema ni WASAFI,mpaka wazee kabisa wanamuona Lowassa ndiyo mkosaji kabisa,lakini haoni UKWELI uliojificha.
Haki kwenye mahakama hakuna,Tume ya HAKI za Binadamu sijui hata kama inajua shughuli zake ni zipi.TISS badala ya kulinda MASLAHI ya NCHI wanalinda MASLAHI ya watu binafsi,hakika katika Taasisi ambayo ilipaswa kuwa HURU kabisa ni TISS..........
Kuna kazi ya ziada ya hasa viongozi wetu wote kuelimishwa kuhusu vyama vingi,tusipoangalia tunaikaribisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.