TBC watangaza rasmi kuonesha Bunge live

TBC watangaza rasmi kuonesha Bunge live

Bunge kibogoyo? Kwa nini linaamriwa na serikali kuhusu lirushwe au la, ndugai anamsimamo gani au ndio sera mpya ya chama chetu pendwa
 
Yule baby mura jana alitoa machozi bungeni akitetea bunge lisioneshwe live. Sasa si ndo atapata presha kabisa. Ila TBC 2!why?
 
Kama kawaida mmekutupuka tena, naona magufuli alikuwa mjanja sana kuwawekea mswahili nape ili awazingue mwanzo mwisho
 
Asilimia 80% ya wapiga kura wapo vijijini.Na watu wa vijijini hawana uwezo wa kuona TBC2.
Bado mfumo wa habari za bunge umeminywa.
 
Umesahau ya kua tuko katika ulimwengu wa digital hata hiyo TBC1lazima ulipie.
Kwani Hujui kwamba TBC1 ni TV ya Uma? Na Umaunalipa Kodi Kuiendesha TBC1?

Hivyo Basi ni Haki TBC1 kuwajibika kwa walipa kodi kuhakikisha wanapata Matangazo ya Bunge LIVE Bila kulipia Senti1.

Watu kama nyie ndiyo Mnawapa kiburi watawala ya kupoka haki ya watanzania kutazama wa wakilishiwao kwa uwezo Mdogo wa Kupambanua Mambo.
 
Mbona hii live ya Tbc Sauti huwa Kama zinapishana? Hebu tusaidieni wataalamu
 
Kwa serikali kusitisha BUNGE LIVE ni kioja cha karne ambacho sikuwahi kukidhania hasa ktk zama hizi
 
bunge live tbc2 lilianza toka j3 hii nimeangalia wizara zote hadi saa 3 usiku.shida hii channel ipo startimes pekee na ni ya kulipia km elfu 10 kwa mwezi.je ni haki
 
bunge live tbc2 lilianza toka j3 hii nimeangalia wizara zote hadi saa 3 usiku.shida hii channel ipo startimes pekee na ni ya kulipia km elfu 10 kwa mwezi.je ni haki
haaaaaaa kumbe kweli? sasa si waruhusu na tv zingine zichukue kwao, au wanataka biashara kuwa kila mtu awe na kinga,amzi cha startimes?
 
Ila tangazo la TBC linasema wazi ni live!
Sio Live wewe,wanaonyesha Live mpaka saa 4(maswali n majibu) then from there wanarecord wanaedit mambo yao wanaonesha saa sita mpaka saa nanenane huko.wanaendelea kurecord hivyohivyo wanaonyesha saa 11 na 4 usiku ..kwahiyo me sioni mantiki yao ya kutoachia tu Live.Hawa wana ajenda nyingine lakini sio hizo walizotuambia...
 
Ila tangazo la TBC linasema wazi ni live!
Sio Live wewe,wanaonyesha Live mpaka saa 4(maswali n majibu) then from there wanarecord wanaedit mambo yao wanaonesha saa sita mpaka saa nanenane huko.wanaendelea kurecord hivyohivyo wanaonyesha saa 11 na 4 usiku ..kwahiyo me sioni mantiki yao ya kutoachia tu Live.Hawa wana ajenda zingine lakini sio hizo walizotuambia...
 
Back
Top Bottom