Njoo Tuongee na Mwakyembe: Afunguka kuhusu Bunge Live, asema mwenye pesa ya kurusha Bunge Live ajitokeze asipige porojo

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Ni wiki nyingine tena ambapo tunaendelea kuwaweka 'Kitimoto' Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano kupitia programu yetu mpya ya [HASHTAG]#NjooTuongee[/HASHTAG] ambayo hurushwa kila siku ya Ijumaa, Saa 12 na nusu jioni LIVE kupitia Star TV, JamiiForums YouTube Channel na kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita tulikuwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Ndg. January Makamba >> Njoo tuongee na January Makamba: Asema nyumba ya mama Lwakatare inasubiri maamuzi ya mahakama kubomolewa


---------

Kipekee kabisa tunapenda kuwashukuru WanaJF wote kwa maswali ya msingi mliyouliza ambayo kama mlivyoona kwa kiasi kikubwa ndiyo yaliyotumika kuendeshea mjadala wetu na Waziri huyo.

Ijumaa hii kiti huenda kikawa cha moto zaidi! Tutakuwa na Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mwakyembe.jpg


Je, una Swali, Maoni au jambo lolote unataka kuliwasilisha kwa Dkt. Harrison Mwakyembe?

Tuwekee hapa..

Kipindi hiki kimetayarishwa na Twaweza kwa kushirikiana na Star TV, JamiiForums na Compass Communications.
Presenters: Aidan Eyakuze na Maria Sarungi-Tsehai
========================

Katika kipindi chetu cha leo cha "Njoo Tuongee" tuna na Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe.

Ungana nasi hapa kuangalia moja kwa moja (Mubashara) na kujionea jinsi waziri huyo atakavyojibu maswali ya Wananchi mbalimbali ikiwemo yale ambayo yalitumwa kwenye 'thread' iliyokuwepo hapa JamiiForums.



Karibu sana!

Update
>>>
Mlituaminisha kuwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge kupitia TBC ni gharama kubwa na pia wananchi wanatakiwa kujikita kufanya kazi na sii kufuatilia bunge. Lakini ikumbukwe pia taasisi ya Tanzania Media Foundation (TMF) ilijitokeza kulipia gharama hizo. Je mko tayari kuwaruhusu TMF walipie gharama za kuonyesha bunge mubashara(Live)?

Mwakyembe: Pengine swala hili lilichukuliwa kama kawaida watanzania kikitokea kitu wataongea weee bila hata kuwa na takwimu sahihi. Live coverage ipo na tunafanya hivyo hata kwenye vipindi vya maswali na kama kuna kitu muhimu kinatokea. Hii serikali ya awamu ya tano imekuja na sera mpya ya kuhakikisha kwamba kila pesa tunayoipata itumike pale ambapo inahitajika. Lakini leo tunashangaa kukatishwa kwa Live coverage ya Bunge ambayo ni gharama hata sisi wenyewe TBC hatuwezi lakini watu hawashangai sisi viongozi hatusafiri kabisa kuenda nje, lakina kwa mtanzania kitu cha kawaida. Leo hatuna posho zozote za mikutano tunakuta hivihivi.

Hiyo TMF, ilijitolea kwake huyo muuliza swali au ilituambia sisi? Leo tukiwaambia lipieni watapotea. Basi waje na proposal kwa Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo kwamba tuna pesa hii iwekwe pale mezani tuone kama watamudu Live Coverage hata kwa wiki moja. Waje wasipige porojo tu maana watanzania ni wazuri sana kusema tu.

Na niwahakikishie vipindi vyote vya Bunge ukienda usiku utaviona vyote TBC Mjadala wote utauona. lakini tukiweka live, sisi leo tunazungumzia kuchapa kazi tu watanzania tuchape kazi. Mimi nafahamu hichi kipindi kikiwa live wakati ya awamu ya tatu na nne watu wanaacha kazi kabisa ni kuangalia Bunge, anawabunge kuajua tunaonekana basi hata mijadala yenye tija hakuna ni kurusha vijembe ili kushamngiliwa na watu mitaani.

>>>Toka umekuwa waziri, umefanya jitihada gani kuboresha kituo hiki cha TBC na umejipangaje kufanyia kazi changamoto za Picha zisizo na muonekano mzuri (Angavu) na habari zinazobagua kwa lengo la kuipendelea serikali?.

Mwakyembe: Haijawahi kutokea TBC kuwa na habari tu za Serikali, mimi ningependa watu wawewakuja na mifano. TBC ndio shirika pekee la Televisheni la utangaji ambalo lina coverage kubwa kupita shirika lingine. Wapo wanaotumia visumbuzi vyao na tume-cover nadhani tumebakiza robo ya nchi kuweka minara na najua mashirika mengine hayajafika hata mikoa mitatu, minne, mitano kwa hiyo tumeenda mbali sana. Kwa sasa kazi iliyobaki ni kuboresha muonekano wa TBC na kuporesha vipindi vyao, japo mazingira ya kazi ni magumu lakini wanajitahidi sana hawa vijana wanafanya kazi kwa uwezo mkubwa sana.

Sisi kama Serikali tumeonyesha mabadiliko makubwa sana, Kwanza mashirika mengi yanapata faida kutokana na matangazo sana sana. TBC ina bajeti yake. Mwaka huu wa pesa tumeweka pesa kuongeza usikivu wa TBC has upande wa redio. Hasa maeneo ya pembezoni kule maana usikivu wetu ni mbaya Meneo ya Nyasa, Lushoto, Namanga na hata Kakonko. Na mwaka huu tumepata milioni kama 3 nadhani tuaongeza wilaya nyingine.

>>>Gabriel Zacharia wa TBC alipotangaza fake news juu ya Rais wa nchi aliadhibiwa yeye pamoja na wafanyakazi wengine na sio TBC kufungiwa, mbona magazeti yanafungiwa wakati kosa ni la mwandishi mmoja kama ilivyokua kwa Gabriel Zacharia?

Mwakyembe: Hakuna gazeti ambalo limefungiwa bila kuonywa kwa zaidi ya mara sita. sasa naomba tuambie kituo cha TV ambacho kumepotosha halafu tukakionyoa kama mara 5 au 6 natukakiacha

>>>Kwanini Kifungu 59 kimetumika kufungia gazeti wakati kinampa uwezo wa kufungia maudhui tu?

Mwakyembe: Unajua mimi na Msemaji wa Serikali tuna nyazifa tofauti. sasa naomba siku tupate muda na sisi tuje na ushahidi wetu, pengine vyombo vya habari vilivyofanya makosa tuvihoji mbele ya watu. Maana watu wanaweka habari bila source

>>

Niliwambia waandishi wa habari wajaribu kuwasiliana na Wizara yake. Ukiwa na shida nenda wizarani jenga hojan Wizara yangu ipo wazi masaa 24. Njoo tuzungumze tujenge hoja

>>> Kupitia sera sheria za ulaya zimejenga ajira nyingi kwa Ulaya. Serikali imejipanga vipi kuhusu hilo?

Mwakyembe: Kwenye michezo ni sehemu ambayo tukijipanga watanzania wanaweza kupata ajira sana. Kupitia waziri mkuu tunataka kuanzisha michezo na kutoa kipaumbele kwenye michezo ya sekondari na primary na itaenda bila kusimama ili kulea vipaji.

Sisi ni wenyeji wa AFCON 2019 kwa vijana Watanzania watashangaa ni wazuri kuliko vijanalipita. Na viwanja vile tutavibadili nyasi maana zimeshachoka.

Sasa hivi tunaweka misingi kuhakikisha tunaonekana Duniani.

>>Kukataliwaa Zanzibar CAF na FIFA kunarudisha nyuma maendeleo katika soka, unawasaidiaje?

Mwakyembe: Tumepigana sana kuhakikisha kuwa Zanzibar inakuwa mwanachama wa CAF na FIFA ila wao wamekataa. Hivyo tumechukua hatua kadhaa tumetuma ujumbe na tusingependa hili swala kuzungumziwa sana maana wenzetu wao wana uwezo mkubwa sana. Ila tunalifanyia kazi

>>>Je sheria inaweza kuwalinda vipi wanafunzi juu ya swala la hati miliki?

Mwakyembe: Kama umefanya utafiti fulani ukiwa chuoni au shuleni basi huo utafiti ni mali ya hiko chuo. Na kama unafanya kazi sehemu fulani ukagundua basi wewe na muajiri wako mnahusika

Mambo ya stika kwa wasanii, mimi niliwakusanya wasanii na kuwaambia tuhamie kwenye swala la Tehama. Kama kuna mtu analeta shida kuhusu stika aje wizarani au aende Basata

>>>Vazi la Taifa lilishia wapi?

Mwakyembe: Serikali ilikuwa inaogopa kuwapangia watanzania kuhusu vazi la taifa, na tuliacha watanzania waibue wenyewe vazi la taifa. ila kama watanzania wanahitaji vazi la taifa basi kupitia wawakilishi wao walibue tena na kujadili

>>>Kuhusu wanamuziki kuimba nyimbo za siasa, je wanaruhusiwa iwe kukosoa au la?

Mwakyembe: Ukitaka kufanikiwa katika sanaa hebu usijiingize wewe kujifanya ni mwana siasa. imba nyimbo za kawaida ambazo haziusiani na siasa. ukitaka kuwaiga wana siasa wanaweza kukuponza maana wewe ni mwananchi wa kawaida na wabunge wana katiba inawalinda.

Ila imba unachotaka na wala usitukane watu, ukiimba ujinga sio lazima serikali hata wananchi watakukosoa.

TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WENU NA ASANTENI KWA KUWA NASI. TUKUTANE TENA IJUMAA IJAYO KWA KIPINDI HIKI TUNAPOKUWA NA WAZIRI TOKA WIZARA NYINGINE
 
Last week nilikuwa nategea nione mtauliza zile nondo au mtafanya censorship? Maana karibia maswali yote yalikuwa chokonozi kwa Januari..

Mfano ishu ya wafanyakazi wa NEMC, Jumba la Mama Rwakatare nikadhani hayatoulizwa (na nilibishana sana kwenye ule uzi kwamba aliyeuliza asahau), lakini mkayanyoosha kama yalivyo na hapo tu ndipo ninapoipendea JF!

By the way, huyu Mwakyembe ni mjanja mjanja sana kwenye kujibu maswali kwa sababu ana advantages 3 na anajua kuzitumia vyema;
1. Mwanasheria
2. Mwanahabari
3. Mwanasiasa

WanaJF, tumkaangeni huyu mzee ishu ngumu ngumu kama ya Makonda, Nape, Kufungia magazeti na kadhalika..

Anayejua kuuliza anisaidie kuformulate basi! Lol
 
Swali la pili Gabriel zacharia wa TBC alipotangaza fake news juu ya Rais wa nchi aliadhibiwa yeye pamoja na wafanyakazi wengine na sio TBC kufungiwa mbona magazeti yanafungiwa wakati kosa ni la mwandishi mmoja kama ilivyokua kwa Gabriel zacharia?
 
Kwa nini hatuoni bunge live kipindi cha mijadala ya bunge? Kama hoja walisema zinawapotezea wananchi mda wa kufanya kazi je live coverage za ikulu na mikoani mbona hazipigwi marufuku maana nazo ziko live?
Haliwezwi ulizwa hili
 
Muulizeni wana mpango gani wa kuanzisha tamasha la ngoma za asili za Tanzania ili kuzienzi? wasiishie kushangilia tu fiesta!
 
Swali la pili Gabriel zacharia wa TBC alipotangaza fake news juu ya Rais wa nchi aliadhibiwa yeye pamoja na wafanyakazi wengine na sio TBC kufungiwa mbona magazeti yanafungiwa wakati kosa ni la mwandishi mmoja kama ilivyokua kwa Gabriel zacharia?
Hili swali hawezi kulijibu...lipo juu ya uwezo wake
 
Wizara INA mpango gani wa kuanzisha mashindano ya vijiji ya michezo yote ambapo washindi watakaoshinda watashindana na wengine kwenye mashindano ya tarafa,wilaya.mkoa ,mikoa na kitaifa ili kuibua vipaji vilivyolala vijijini nchi nzima visivyoweza jua vitafikaje juu kwani vijijini pia kuna wakimbiaji wazuri ,wacheza mpira wazuri nk
 
Nina maswali yafuatayo:

1. Sheria ya Tanzania inataka magazeti yote nchini yaandike taarifa za kweli, zinazoheshimu haki za raia wengine, kwa nini Magazeti yanayoandika taarifa zinazotafsirika kuwa ni za kuwalisha maneno yasio yao viongozi wa serikali ndiyo yanayobanwa yaombe radhi, kupewa onyo na hata kufungiwa LAKINI yale ambayo huwaandika vibaya watu wa kawaida wasio viongozi wa kiserikali kama vile wasanii wetu kwa habari za Kiudaku za kizushi zisizo za kweli dhidi yao, zikiwemo habari Zinazoingilia hata faragha zao Hatuoni serikali Ikiyapa onyo au kuyafungia magazeti ya aina hii?. Je kwa nini serikali haiyachukulii hatua kali magazeti haya ya Udaku yaliyokithiri kufanya tabia hii?.

2. Swali la pili, kuna taarifa zinazagaa mitandaoni kuwa serikali ina mpango wa kupeleka muswada bungeni kutunga sheria ili kubana uhuru wa watu kupata taarifa kupitia mitandao Je Ukweli ni upi?

3. Swali la tatu kuhusu michezo, Wakati wa Uongozi wa baba wa Taifa serikali ilihakikisha wananchi wake wanaburudika ipasavyo kupitia michezo na kuwa tekinolojia ya wakati huo ilikuwa ni radio basi michezo yote Muhimu ya Ligi na Mechi ya za Timu za Taifa zilirushwa redioni watu wakasikiliza, Sasa kwa kuwa tekinolojia imekua na sasa hivi kuna Televisheni Kwa nini Serikali ya awamu ya Tano kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) inawanyima wananchi fursa za kuona LIVE Mechi za Timu yao ya Taifa Taifa Stars pindi ikicheza, na Pia inawanyima wananchi Fursa za kuona LIVE mechi zenye maslahi mapana ya umma kama za Simba na Yanga, Kwa kufanya hivi serikali haioni kwamba ni wananchi wachache wenye uwezo wa kulipia ving'amuzi ndo wanaweza Kushuhudia Timu yao ya Taifa ikicheza, Je kwa kufanya hivi serikali haioni kwamba inakosa fursa ya kujenga uzalendo wa wananchi kupitia hamasa Michezo muhimu ambayo ingerushwa na TBC?

,
 
Tunaona rais akitoa matamko na vijimaneno vyenye utata katika taifa na baadae wanatokea watu fulani kukanusha alichosema na kuweka wanayoyataka wao,
SWALI,Je hii sio kupotosha jamii na umma kwa ujumla kwa hawa wasaidizi na Je kwa sheria ya adhabu ya upotoshaji inataka wachukuliwe hatua gani kwa kudanganya umma kupitia vyombo vya habari hata ikulu
 
Ni kwanini sasa hivi vyombo vya habari vyote vimejikita kusifia tu awamu hii, na chombo chochote kisichosifia na kuwa na muekekeo wa kukosoa kinajikuta kwenye wakati mgumu ama kufungiwa kabisa? Je ni mtindo (fashion) mpya ya kusifia tu ndio inayotakiwa awamu hii? Kwa mtindo huu wa kutaka wananchi wote kusifia tu ndio italijenga taifa hili? je waziri haoni mwenendo huu utasababisha watu kushindwa kujua tofauti ya uzalendo na ujinga?
 
Ni wiki nyingine tena ambapo tunaendelea kuwaweka 'Kitimoto' Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano kupitia programu yetu mpya ya [HASHTAG]#NjooTuongee[/HASHTAG] ambayo hurushwa kila siku ya Ijumaa, Saa 12 na nusu jioni LIVE kupitia Star TV, JamiiForums YouTube Channel na kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita tulikuwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Ndg. January Makamba >> Njoo tuongee na January Makamba: Asema nyumba ya mama Lwakatare inasubiri maamuzi ya mahakama kubomolewa


---------

Kipekee kabisa tunapenda kuwashukuru WanaJF wote kwa maswali ya msingi mliyouliza ambayo kama mlivyoona kwa kiasi kikubwa ndiyo yaliyotumika kuendeshea mjadala wetu na Waziri huyo.

Ijumaa hii kiti huenda kikawa cha moto zaidi! Tutakuwa na Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

View attachment 627322

Je, una Swali, Maoni au jambo lolote unataka kuliwasilisha kwa Dkt. Harrison Mwakyembe?

Tuwekee hapa..



Hii sio media ya kuitangazia star Tv.
Kama Mwakyembe anaamini kuwa great thinker wako huku JF tunamuomba aje tumuulize maswali yetu ajibu humu!
Habari ya maswali ya kuchaguliwa dizaini hatutaki.

We can't afford brainwashing.
 
Binafsi sina cha kumuuliza wala kusikia kutoka kwake, ila ushauri tu awe makini na atakachozungumza asije akaaibishwa na bosi wake kama alipokuwa kwenye wizara ya kabla.
 
Hii sio media ya kuitangazia star Tv.
Kama Mwakyembe anaamini kuwa great thinker wako huku JF tunamuomba aje tumuulize maswali yetu ajibu humu!
Habari ya maswali ya kuchaguliwa dizaini hatutaki.

We can't afford brainwashing.

Ukisha pangiwa cha kuulizwa basi tayari wamesha uingilia uhuru wako ..

Nami nnaunga mkono hoja yako Mkuu..
 
Maswali yangu nikama yafuatavyo.

1]Kuhusu uwanja mkubwa wa mpira ambao serikali ya Morroco ilihaidi kutufadhiri mkoani Dodoma,hatua zake zimefikia wapi na kama bado nini tatizo la kutoanza kwa ujenzi huo?

2]Tunajua viwanja vingi vya mpira vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi,na vingi vyao ni dhoofu li hali.Pitch za kuchezea na majukwaa si ya kupendeza.Nini mpango wa serikali katika kuboresha viwanja hivi kwa kuweka atleast nyasi bandia kwenye viwanja vya makao makuu ya mikoa na kutengeneza majukwaa hili viwe na mvuto.

3]Mpango wa kujenga kijiji cha olympic umefikia wapi?
 
hivi kuna uhuru wa vyombo vya habari? nasubili jibu udànganye
 
Back
Top Bottom