Nape jibu hoja hizi kuhusu bunge live

Afixa0

JF-Expert Member
Jun 16, 2015
464
485
Mtu anaposema kwamba bunge halirushwi live kwasababu Watanzania wengi hawana muda wa kuangalia bunge live kwenye Tv kwasababu mchana wanafanya kazi. Je huyu mtu anashindwa kuelewa kwamba sio kwamba wote wana angalia bunge kwenye runinga, wengine wana sikiliza radioni huku wakiwa wanafanya kazi na wengine wana angalia live wawepo ofisini na sehemu zingine.

-Je bunge linaporushwa live asubuhi kipindi cha maswali na majibu kuanzia saa 3 hadi 4, huu muda kwa Tanzania sio muda wa kazi? Na je, huu muda watanzania huwa wanakuwa wanaenda kazini au huwa wapo nyumbani wametulia na familia zao kama wanavyodai watu Fulani?

-Kama Watanzania wanafanyakazi na hawana muda wa kuangalia bunge inavyodaiwa na watu fulani, Je wanapata wapi muda wakuangalia vipindi vilivyo haririwa vinavyorushwa na TBC CCM usiku. Mimi nina amini usiku ni muda ambapo watu wanatakiwa wapumzike baada ya uchovu mwingi toka kazini, ili kesho wawahi kazini. Sasa kama mtu anayesemwa kwamba hawezi akaangalia bunge live mchana kwa sababu yuko kazini, anaangalia bunge usiku, Je kesho atawezaje kuamka mapema na kuwahi kazini wakati amechelewa kulala kwasababu ya kuangalia bunge usiku? Kuna watu wanatoa hoja za chekechea kweli kweli.

Hivi kama ajira zenyewe ni shida hivi, hao watanzania tunaombiwa wanaowahi kazini, wanakuwa bize hadi washindwe kuangalia bunge ni wangapi? Kwasababu kutokana na hali ya maisha ya sasa hivi tunapoangalia bunge ndipo tunaweza pata faraja japo kidogo kuhusu hatima ya maisha yetu pale ambapo wawakilishi wetu wanatusemea na tunasikiliza au kutazama.

Mtu, mwingine amesema juzi alipokuwa anahojiwa DW kwamba, Watanzania wengi ni wakulima kwahiyo wawezi wakapata muda wa kufatilia bunge. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na ni udharau mkubwa; Kwahiyo mkulima kwa kuwa analima hatakiwi kupata habari kuhusu hatima yake ndani ya kilimo hicho katika nchi yake?

#HAPA HOFU TU
 
Back
Top Bottom