TBC wajitetea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC wajitetea

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Taso, Nov 3, 2010.

 1. T

  Taso JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Marina Hassan, Tiddo Mhando etc. wako hewani wakijetetea jinsi walivyo cover kampeni huku wakivishambulia vyama. Tukio la Marin Hassan kugombaniwa na wana CHADEMA jangwani wanadai lilitokana na CHADEMA kukiuka makubaliano yao na TBC kwamba wasikashifu mtu kwenye hotuba zao, na hivyo walilazimika kutoka hewani. CHADEMA wakapata taarifa hapo uwanjani kwamba TBC wametoka hewani na Marina Hassan ndio huyo hapo kachomoa waya. Ikabidi CHADEMA watake kumwadabisha hadi polisi walipomnusuru. Marina anadai siku hiyo alilia machozi zaidi kwa kuwa alitukanwa ya nguoni.

  Swali: Wao TBC wamekua ni NEC au Kamanda Kova wanaotoa vibali vya mikutano mpaka wavipe vyama masharti nini cha kusema? Pinheads!

  Narudia rai ya Freeman Mbowe aliyoitoa siku Marin Hassan alipotaka kuchapwa:
  “ Nawaonya TBC kwamba wanalipwa na kodi yetu wananchi maskini, na siku wananchi wakichoka hakuna jeshi litakaloweza kuwazuia.”
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Achana nao nadhani mioyo imewauma hadi wameamua kuwa washing maniacs!
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini Marini hastahili kukaa Dar. Inabidi atafutiwe sehemu za kuishi kwingineko, hatufagilii pumba na elimu zisizo mishiko
   
 4. r

  rushasha JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 732
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa ukweli MUNGU atawalipizia mabaya waliyowafanyia Watanzania. Najua mioyoni mwao wanajua ukweli ni upi na wanatakiwa wafanyeje lakini hawakutaka kutenda haki na kufanya kile cha kweli walichotakiwa kukifanya. MUNGU waonyeshe watu hawa kuwa "WEWE NI MUNGU"!
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  la TBC tushaliweka kando..soon menejiment iabadilishwa ama ikibidi shirika libinafsishwe tu apewe mdau anayeweza kufuata maadili ya uanahabari
   
 6. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Huyu TIDO MHANDO pamoja na kukaa BBC naona alirudi na kumbukumbu ya mambo yale yale alitoyaacha miaka ya 1970 ya kuwalamba watawala ******. Labda pensheni yake ya BBC haitoshi anaganga njaa. Heshima yake imeshuka mno katika miwani yangu. Iko siku CCM itaanguka sijui atajificha wapi? Amefanya TBC kuwa sawa na Radio Uhuru au gazeti la Uhuru vyote mali ya CCM. Dandahead TIDO MHANDO. You can delay change but you can't prevent change.
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  nawachukia na kuwalaani wote wanaowasaidia mafisadi wakiwemo Tido na Marin

  "... wao wana pesa, sisi tuna Mungu .. " (Godbless Lema, MP)
   
 8. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tido na Marine Hassan wana ushabiki wa kijinga. Hata ukiona mijadala yao na maswali yako ni leading questions not hard hitting questions hasa wanapokuwa na mijadala na makada wa CCM. They are not impartial at all.
   
 9. b

  bulunga JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ni oto ndo unaweza kumtukana akalia, nie, nilifikiri hicho ni kipara cha busara kumbe ni bure, ni dhahiri alijua mauti yalimemfika si ajabu alitoa WILL yake:A S angry:
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  T
  Kiongozi kutuhumiwa ufisadi siyo tusi...............Sasa vyama vya siasa visipowafahamisha wapigakura matatizo na changamoto za kuendesha nchi haya yote tutayajuaje? Tutawezaje kuchagua viongozi wazuri kimya kimya?
   
 11. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samahani mkuu naomba ufafanuzi juu ya hii signature yako hapa chini Ufisadi ni sera rasmi ya tabaka tawala, kwa hiyo hata hawa tuliowaweka madarakani sasa hivi, kwa ajili tulichoshwa na ufisadi wakishaingia madarakani ufisadi ndo itakuwa sera yao? Samahani kutoka nje ya mada.
   
 12. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aleluyah!

  Ccm wanapaswa kujua

  Ni haki yetu kujua makosa yanayotendwa na viongozi wetu na isije ikaonekana kuwa dr. Slaa anatenda dhambi kuyaweka bayana. Hii itawasaidia nao kutubu!

  Amani haiji ila ka ncha ya upanga!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Dr slaa wa mobilIze watu kama ilivyo kuwa kule Arusha, Mwanza na Dar tUkadai haki kama kweli unahakika kura zimechakachuliwa na unazo evidence. Kila jimbo tuandamane kwa wakati mmoja nchi nzima. Na TBC mjiandae kuchukua picha na taarifa kamili.
  Tumechoka kuburuzwa kama magunia jamani, Mungu awabariki nyote, Mpe Dr. Slaa Nguvu na Hekima ya kupambana na haya yote. Amen!
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Mimi ninashangaa leo asubuhi walivyomaliza matangazo yao ya matokeo ya Uchaguzi kwa mbwembwe wakati wanajua kuwa kuna majimbo mengi tu bado hayajatangaza matokeo. wasitufanye wajinga. Hii ni kucheza na saikolojia ya watu kuwa uchaguzi umekwisha wakati watawala wao wakiendelea kuchakachua matokeo ya kulikobaki. Hii ni TV inayolipiwa na Kodi za Wananchi. ILitakiwa kuendelea kutoa matokeo ya majimbo hadi jimbo la mwisho. Tido chunga, Yana mwisho haya.
   
Loading...