Nimesoma comments za watu wote hapa nimeona nami niseme kidogo kuhusu uwezo wenu mdogo wa kufikiri ninyi wote mliotoa maoni. Kwanza hamkumuelewa mtoa mada arushaone ambaye kifupi hakueleza nini kinamkera zaidi ya kuonyesha hapendi taarifa za ccm kupewa nafasi. Hii nayo ni tatizo. Mfano jk akisema jambo ukatangaza hata kama si mkutano wa ccm utachukia kwakuwa yeye ni wa ccm? Habari ngapi za ccm zimetangazwa hadi ufikie hitimisho la kusema tbc tv haina maana na ni aibu kwa shirika la umma? We sema kwamba unataka habari za cdm zitangazwe hata kama hazina habari mpya.
Kumbuka tbc ni chombo cha umma, hakipaswi kuingia katika malumbano ya siasa, siku chama chama chako kikishinda tbc itatangaza sana habari zake kwakuwa si tu ni chama tawala lakini pia kila kiongozi atakayesimama kutoa tamko ni mwanachama wa chama hicho kitakachounda serikali na ni lazima apate nafasi kwenye chombo cha umma.
Sasa tafakari wewe unayefagilia itv je ni kwa kiwango gani inatangaza habari zenye mrengo wa kitaifa?
Toa tuhuma zenye kueleweka kwa tbc na si kuituhumu kama haitangazi habari za cdm, utakuwa hautendi haki. Haya sasa wewe uliyetaja kwamba tbc ilipaswa kutangaza habari ya waziri kusaini mktaba bila kuusoma, je uliona tv ipi imetangaza? Usihoji kazi ya wanahabari kama wewe hufahamu misisngi ya habari inavyotakiwa kutangazwa.
Mimi nawashauri wanajamii tuwe makini kuunga mkno tuhuma za mtu bila kujua undani wake na pia sababu ya huyo myu kutoa tuhuma, je madai yake ni ya kweli? Na wewe umemuelewa? Kama hapa wengi hawakuelewa wameanza kueleza hisia zao za tangu tido. Sasa hii ndiyo sisi wahadhiri tunaita shalow knowledge which is very poison.