Ujumbe kwa Rais: Kama nigekuwa Waziri nisiye na Wizara

90sgeneration

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
275
375
Habari wakuu. Mimi sio mtu wa siasa sana, lakini ni mtu ambae nafatilia mambo mbalimbali hasa habari za maendeleo ya nchi na mienendo ya siasa zetu na kijamii, na maisha kwa ujumla. Asante JF imenipa elimu kubwa sana ya mambo tangu nijiunge 2011 nikiwa secondary (kwa ID ya zamani nilisahau pass code).

Kuna matatizo mengi sana ambayo sijui ni either kwa makusudi au basi tunaamua yaendelee na sielewi ni kwa faida ya nani. Ni kwamba Rais wetu (aliepo na waliopita) hana washauri wazuri? Au washauri wake hawazingatii sana haya mambo?

ell pengine wanamajukumu mengi yanayowakeep busy kuliko haya ambayo kimsingi ni ya muhimu sababu serikali ipo kwa jili ya kulinda watanzania wote bila kujali mjinga au mwerevu.

Naomba ni act kwa muda huu kama Waziri asiye na Wizara (nadeal na wizara zote kama mshauri na bwana mipango). Labda naweza kusaidia mahali ambapo pengine mawaziri hawajapaona kama pana umuhimu.

Kwako Raisi na Waziri wa Ardhi;

Nianze na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Raisi, waziri aliepo madarakani ni kweli anajitahidi ila hajatilia hili jambo la utapeli wa viwanja na nyumba ambao umeota mizizi kila kona ya nchi hii. Watu wengi wanadhulumiwa ardhi na viwanja na hata nyumba zao.

Wengi wamelalamika, wamelia, wamekufa kwa presha, wamerudishwa nyuma kimaendeleo, wameletewa umaskini na hawa matapeli.

Wengine wanamagenge kabisa makubwa na wanafanya utapeli kwa kujiamini sababu wanajua mwisho wa siku hawawezi kufungwa kwa kesi ya utapeli, zaidi ya kupata dhamana, na mdai kuzungushwa na mwisho kukata tamaa na kuamua kuacha, na hapo akiwa ameathiliwa vibaya.

Kwa nini hili tatizo halitatuliwi na matapeli wanaongezeka?

SABABU ni hii, matapeli wanajua kabisa kesi ya utapeli wa aina hii hua sio jinai, huishia kua kesi ya madai na blabla then case closed. Na anaeumia zaidi sio tapeli, bali alietapeliwa.

Only watu wenye guts za kuwakomesha personally hao matapeli ndio hua wanaweza kwa kuwadhulu (kitu kinachoongeza kesi za mauaji mitaani), japo only 10% kati ya 100% ambao huweza kurudishiwa hasara, na 10% kulipwa half, waliobaki hubaki na vilio. Hivyo kwa hili utapeli huu kamwe hautaisha tukiendelea na hii trendy.

Mh Raisi na Mh waziri wa ardhi, Mimi kama waziri mshauri, nashauri sasa umefika muda wa makosa ya utapeli huu wakipumbavu unaowaletea umasikini watanzania wanaojaribu kupambana kujiletea maendeleo kukomeshwa. Nashauri mashauri ya aina hii ya utapeli wa viwanja, nyumba na ardhi yahamishiwe katika category ya makosa ya jinai.

*Mtu anaetuhumiwa kutapeli, iwe kuuza kiwanja, nyumba, ardhi na chochote kisicho chake, kutengeneza document na mihuri fake na kujifanya mwenyekiti, au kiongozi wa sehemu husika (wanaotapeli hua na mihuri na hujifanya wenyekiti wa mitaa na hua na docs zote) basi ashitakiwe kwa kosa la jinai na si la madai.

  • Kusiwe na dhamana.
  • Kifungo kiambatane na fidia na adhabu zingine ikiwemo kufilisiwa.
-Kifungo kianzie miaka 10+ kutokana na kesi husika na madhara yaliyopatikana (kuna watu hufariki au kuharibiwa maisha kabisa), hivyo hakimu/judge ataamua mwenyewe.
- Na mashauri haya yawe yanaharakishwa, na wakithibika bila shaka, basi wawe wanatangazwa hadharani.

FAIDA

Raisi na Waziri wa Ardhi
Haya mambo yanarudisha sana nyuma watanzania, badala ya kuendelea watu wanarudishwa nyuma. Serikali inapambana kuwezesha wananchi na wananchi wanapambana na mwisho wa siku mapato ya jasho lao yanamalizwa na wahuni wachache ambao wanadharau hafi mahakama zetu. Wanaotapeliwa sio wajinga, ila situation zinawakuta tu either kwa kukosa elimu au shida. Ni kazi ya serikali kuwalinda watu wake na utapeli huu.

Faida ni kwamba, kwa kuhamisha kesi hizi kuwa jinai, kwanza kabisa, watu wataogopa (haitaisha for 100%) lakini watu wataogopa, sababu sasa hawatapata dhamana, ambayo kwa hili inasemekana wanashirikiana na police wasio waaminifu kuwaachia huru na wanaamini sio rahisi kwao kufungwa.

Ila kama hakuna dhamana basi itakua kama ilivyo kesi za mauaji, sio kwamba watu hawauwai, lakini sheria ya jinai inapunguza mauaji. Na pia itawapa confidence wananchi kununua viwanja.

Hii itapunguza sana huu utapeli sababu sasa matapeli watakua wanajua kabisa kua wakikamatwa basi wameishia jela hakuna cha dhamana wala ujinga wa kulipa na kuachiwa, bahati nzuri kesi hizi za matapeli hua zina evidence nyingi mala nyingi.

Raisi;

Maendeleo ya wananchi hayawezi kuja ikiwa kila siku wanatapeliwa, mala pyramid schemes, mala kylinda sjui D9 sjui global, sjui matakataka gani, msiachie tu watu wakatapeliwa, wekeni sheria kali kuwakomesha matapeli.

USHAURI MUHIMU WA ZIADA

Pia Mh. Waziri wa ardhi, wizara yako ni wakati sasa wa kuweka kitengo maalumu cha uuzaji wa viwanja, ambacho ndio kitakua kinatoa document maalum za mauziano. Kitengo hichi kiwepo chini ya halmashauri zetu au ofisi za ardhi ambapo:

Mtu akiwa anauza kiwanja chake, au nyumba au shamba, akishapatana na mteja wake, akaenda kukiona, wakakubaliana bei, basi waelekee katika ofisi hiyo wakiwa na batua ya serikali za mitaa husika au kijiji au mji, kisha wakifika ofisi hiyo ijiridhishe kuwa kiwanja ni cha muuzaji kwa kuweka utaratibu ambao upo (sina hakika).

Kisha mauziano yafanyike chini ya wizara ya ardhi na iingie kwenye data base, kwamba 90sgeneration kamuuzia Hamad Rashid kiwanja no x,mtaa x kwa kiasi cha sh 900, tarehe 22/02/2023.

Shahidi ni Mwenyekiti wa mtaa Mbwana Ally, imethibitishwa na afisa ardhi bwana David Mshana. (Hili pia litaingizia serikali mapato, ambapo mnaweza weka only 2% au chini au zaidi (ila isimuumize mtu) ya bei ya mauziano iingie serikalini kama kodi)

NOTE: Kama hamna database ya kutambua kila mmiliki wa ardhi please anzisheni. Watu wasajiri ardhi zao, nyumba, shamba nk.

Kila eneo ambalo serikali itagawa viwanja, basi watu wataopewa taarifa zao ziwekwe kwenye database, kila kampuni ya kuuza viwanja ikiuza viwanja, basi taarifa zikasajiliwe ardhi na ziweke kwenye data base, kwamba eneo fulani sasa linamilikiwa na fulani, likiuzwa au kurithishwa basi taarifa zibadirishwe pia, na asiefanya hivyo basi hata eneo likiuzwa kitapeli asilalamike.

Ifike mahali Raisi mambo ya kijinga yaliyozoeleka yatatuliwe kibabe, sio kuvumilia upuuzi na watu wapuuzi. Sheria ya makosa ya utapeli yawe ya jinai, ili kukomesha Tanzania kua shamba la bibi au nchi ya wajinga.

Ni kazi yetu kama serikali kuwalinda watu wetu na aibu za kuonekana Taifa la wajinga wanaodhurumiwa ovyo, hata makosa ya wizi wa mtandao yawekwe category ya jinai, yasiwe na dhamana na adhabu ziwe kali ikithibitishwa. Kesi ziendeshwe kwa uwazi kuepuka mahakimu wala rushwa. I

fike mahali kesi za ardhi ziendeshe live TBC Taifa, hii itasambaza uelewa zaidi wa mambo ya ardhi, na tutakomesha upuuzi.

Hata viongozi wa serikali ambao wanatabia ya kuuza maeneo ya wanavijiji hovyo na kuwadhurumu haki zao ardhi zao, wapewe kesi za jinai. Hawa ndio wanasababisha kila siku migogoro kati ya wawekezaji na wananchi. Ni wakati sasa wa kuondoa ukiritimba kwenye ardhi. Yani hadi watu wanaogopa kununua viwanja kuogopa utapeli.

Aisee nina mengi ningeweza kushauri, najua mnajua mengi mawaziri wenzangu, hapa najaribu kuwakumbusha na kuwapa mbinu mpya au idea.

Niishie hapa kwenye wizara ya ardhi. Nakuja na Wizara ya kazi, vijana,ajira na wenye ulemavu.

Ni mimi 90sgeneration,
Waziri asie na wizara,
ofisi ya Raisi kazi maalum na ushauri.
 
Wizara Ya Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu.

Mh. Raisi na Mh. Waziri wa wizara hii.

Hii wizara inachangamoto pia ambazo kiukweli hazijatatuliwa kwa miaka mingi sana. Yani vijana nchi hii wanamamtatizo mengi, ambayo hayahitaji hata budget kutatuliwa, ila unashangazwa why hayajatatuliwa. Kuna thread humu inazungumzia kazi za viwandani. Hivi kweli kwa maisha ya sasa Mh. Raisi vijana nguvu kazi bado wanalipwa 4500 kwa siku tena wanafanya hadi 12hrs kwa 4500? kweli watu wanasema vijana wengi wanaumia viwandani na hawalipwi stahiki zao wanaishia kufutwa kazi, mazingira magumu ya kazi, hakuna sehemu ya kulalamikia (kama ipo basi 99% ya watu hawaijui).

Viwanda na mashirika mengi yanaajiri wageni hata kwenye kazi za kawaida, na tena wanalipwa vizuri kuliko wazawa kwa kazi zile zile, haya sio malalamiko mapya, yamo hata humu for years, but Mh. Waziri you have done nothing! hizi ndio kazi za kushughulikia, waelekeze watumishi wako waache kukaa ofisini, wazunguke. Kuna vyama vya wafanyakazi, lakini they arr doing nothing, wapo kupokea tu michango ya wafanyakazi. Watu wanafukuzwa kazi kiholela tu bila utaratibu, yani mtaishia kusema vijana wa Tanzania sio waaminifu ni wezi wanaiba maofisini na makazini, YES, wataacha kuiba wakati hawana assurance ya kazi? yani hawajui anafukuzwa saa ngapi bila hata notice, wanaiba ili wajioange harakaharaka watafute mitaji. Yani vijana wengi sio waaminifu makazini sababu hawana usalama makazini, wapo kama vibarua, na serikali haina msaada wowote ule.

Hivi kuna hata sanduku la maoni huko wizarani ambalo waziri tu ndio analifungua? angalau hii itasaidia mtu yoyote aruguhusiwe kureport maoni na taarifa direct kwa waziri bila kutambulika.

Mh. Raisi, hatutaendeleza vijana kama hatuwawekei mazingira yanayowalinda na kutenda haki. Wawekezaji wafate sheria ndio, lakini kama sheria hazitiliwi mkazo, unadhani nani atajali? yako mengi mengi mengi sanaaaaaa, yani hadi unajiuliza, hiyo wizara hua inajishughulisha na nini ikiwa kwenye issue za ajira ndio ukiritimba umelala kila kona.

Anyway, mimi kama Waziri wa ofisi ya Raisi Nisie na wizara maalumu nashauri yafuatayo:-

Kwanza kabisa, sheria za kazi kuanzia sasa ziwe wazi. Shida sheria ziko zimefichwa ofisini kwa waziri, watu hawajui sheria na hawajui haki zao. Hivyo solution ya kwanza ni kuhakikisha watu wanajua sheria na haki zao sehemu za ajira. Sasa watajiaje?

-Tumieni mitandao ya kijamii, na page mbalimbali za wizara, websites, social media pages nk, watu wajue haki zao kuanzia wakati anaajiriwa au anapewa kibarua, anapokua kazini, anapopata matatizo, na anapoachishwa kazi. Hii itawapa confidence katika kuface mambo ya kuumiza na kumnyima haki kazini.

-HR wote kwenye makampuni na maofisi, iwe ni lazima kuwapa muongozo wa sheria na haki na mfanyakazi kwa wafanyakzi wote, yani mtu anapoajiliwa tu, apewe hiyo document kutoka wizarani, yenye sheria, kanuni na taratibu zote na haki zote za mfanyakazi, asome aelewe na iwe lazima, asiewapa wafanyakazi na ikathibitika basi achkuliwe hatua kali, ikiwemo (kama kuna leseni) basi wafutiwe, na faini pamoja na kulipa fidia kwa mfanyakazi huyo ambae hakupewa na akakosa haki yake.

-Wizara iweke informers ambao watakua wanatembelea kwa siri viwanda na makampuni kujua hali za wafanyakazi na kujua kama sheria za kazi zinafuatwa na muajiri, yani kama kuna kuvaa helmet je watu wanazo? na wanavaa? watu wanafanya kazi kwa masaa ya kisheria? kama ni over time je wanalipwa stahiki zao? kuna unyanyasaji?, kazi hii isifanyike kwa kwenye kuwahoji, no one will talk, kazi ifanyike kwa hao informer kwenda kama wafanyakazi kuomba kazi na vibarua, wafanye kazi hapo kwa muda wachukue taarifa zote na evidence wawasilishe wizarani, bila hao informer kujulikana.

-Waajiri watakaokua wamekiuka , basi waadhibiwe na kulioa fidia kali wale waliofanyiwa ukatili makazini au kwa kutofata sheria. Lakini pia makampuni yanayofanya vizuri yapongezwe na kupewa misamaha mbalimbali ili kutia hamasa.

-Liwekwe sanduku la maoni, kwanza wizarani, na pili kwa waziri husika, tatu kwa Mh. Waziri Mkuu., waajiliwa na waajiri waruhusiwe kuweka taarifa za siri (zilizothibitika au zinazoweza kuthibitika) ambazo wanaogopa kuwasilisha kwa wahusika kwa kuogopa kufukuzwa kazi, au kudhuliwa.

Mwisho, nimeongelea upande wa ajira tu, lakini pia suala la fursa kwa vijana na mitaji, hapa mmejitahidi hata mmeweka mikopo ya vijana ya halmashauri nk. LAKINI tatizo ni moja, taarifa zinafichwa fichwa sana, yani hata utaratibu unafichwafichwa, mambo hayakowazi kiasi hata vijana hawajui waanze wapi, yani wafate hatua gani.

Huko halmshauri kuna watumishi wasio waaminifu wanahatibu na vijana wanaopata ni wachache tena kwa kujuana na inachukua muda mrefu sanaaaaaaaaaaa, maomba yanatumwa mwezi wa kwanza, majibu yanarudi December. Hakuna uwazi, hilo ni tatizo.

Haoa kwenye fursa na mikopo ya vijana, i wish nipewe hiki kitengo ni regulate, yani iunde taasisi maalumu kila mkoa, yani mikopo isiwe chini ya halmashauri, bali chini ya hiu taasisi, ambayo inajitegemea, ambayo itakua inatafuta fursa, inawapa vijana na inawapatia mkopo na kuwasimamia vijana katika miradi hiyo, kuna fursa nyingi sana za biashara nnje na ndani ya nchi, ila si rahisi vijana wengi kuzifahamu, hivyo taasisi inakua inafanya research na inawapa vijana fursa na kuwawezesha mikopo na kusimamia utekelezaji. Taasisi iwekwe chini ya Ofisi ya Raisi au Waziri Mkuu. Hoi itasaidia sana vijana, hebu mnioe hiyo kazi even for 1 year muone vijana watakavochachalika na kupewa support.

Ni hayo machache tu kwa wizara hiyo. Kazi iendelee.

Ni mimi 90sgeneration,
Waziri asie na wizara,
Ofisi ya Raisi kazi maalumu ya ushauri.
 
Safi sana waziri asiye na wizara. Maono mapana ila sio kila kitu unachofikiria ukahisi kinatendeka kirahis hivo. Japo jambo la utapeli lipo mpaka serikalini... nikiwa na maana kuna Mwalimu alijifanya mwanajeshi na kutapeli wananchi mwisho sijui kesi yake imeishia wapi?.

Tanzania bado Rushwa inafanya kazi kwa hiyo ukitambua kauli mbiu ya Rushwa unagundua bado iko . Maendeleo hakuna na hali hakuna.
 
Safi sana waziri asiye na wizara. Maono mapana ila sio kila kitu unachofikiria ukahisi kinatendeka kirahis hivo. Japo jambo la utapeli lipo mpaka serikalini... nikiwa na maana kuna Mwalimu alijifanya mwanajeshi na kutapeli wananchi mwisho sijui kesi yake imeishia wapi?.

Tanzania bado Rushwa inafanya kazi kwa hiyo ukitambua kauli mbiu ya Rushwa unagundua bado iko . Maendeleo hakuna na hali hakuna.
Is true mkuu, lakini at least they should try, kila jambo lina changamoto but sheria kali zinasaidia kupunguza uhalifu, waweke sheria za utapeli kua kosa la jinao unaloweza 30 years au kufungwa maisha , itasaida, hii ya mtu anatapeli million 100 then akipatikana anafungwa 2 years anatoka, utapeli hautaisha trust me, na sio lazima uishe ile utoke from 85% to 5%
 
Is true mkuu, lakini at least they should try, kila jambo lina changamoto but sheria kali zinasaidia kupunguza uhalifu, waweke sheria za utapeli kua kosa la jinao unaloweza 30 years au kufungwa maisha , itasaida, hii ya mtu anatapeli million 100 then akipatikana anafungwa 2 years anatoka, utapeli hautaisha trust me, na sio lazima uishe ile utoke from 85% to 5%
iko hivi ngoja nikusaidie kitu.. sio kila kiongozi hana lengo la kukomboa Taifa ila sasa watu hali nao. Tambua mtu anapenda PEPO ila why anaogopa kifo? Iko hivo kwa hawa viongozi wetu maana hata matapeli wengine wako na watu wao serikalini.. kitu kingine Rushwa ndo inatutesa Tanzania
 
Back
Top Bottom