TBC Taifa Fm: Kipindi cha Tumwabudu Mungu Jumapili ya Leo: Mada Kuu - Tutubu Dhambi Zetu

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
991
1,412
Heri ya Jumapili wapendwa katika Jina la Bwana aliye Hai.
Kutokana na dozi ya Konyagi ya jana nimeshindwa kwenda Kanisani nikaamua nisali kupitia Kipindi cha Tumwabudu Mungu kupitia TBC Taifa Fm. Kilichonishangaza Mpaka kuleta uzi huu ni pale wahubiri wote wa leo wamesisitiza wanadamu tutubu dhambi zetu na tutende yaliyo mema kwani mtenda mabaya chuki na gadhabu za Mwenyezi Mungu Zitamshukia na hapo ndo utakuwa mwisho wake.
Sasa najiuliza hawa wachungaji waliotoa Mahubiri leo TBC Taifa Fm walijipanga Kumuunga mkono Mchungaji Zacharia Kakobe? Au ni coincidence tu!!!! Tena Radio ya Serikali!!!
Niwapongeze wachungaji wote wa Leo waliotupatia neno la Uzima kupitia TBC Taifa Fm. Haijalishi kama walimuunga Mkono Kakobe au walimlenga Mtu Maalum ila neno la leo limenifundisha sana umuhimu wa Kutubu Dhambi Zetu na kumtumaini Mwenyezi Mungu katika Kila Jambo.
Ila kama kuna mlengwa Maalum basi ajitathimini.
Tumsifu Yesu Kristo. Amina!!
 
kwa ulivyojieleza hapo mwanzo kushindwa kwenda tu kanisan kwa sababu ya kilevi cha konyagi yakupasa kutub dhambi zako maana kama pombe imekufanya usiende kanisani ni dhahiri hata haya uliyoyaongea yana element za ulevi ulevi (punguza pombe ni hatari kwa afya yako ) afya uliyopewa na mungu unaiharibu mwenyewe kwa akili yako mwenyewe uliyopewa na mwenyezi mungu
asubuhi njema
 
Acha uzandiki!!! Mimi husali misa ya kwanza 12 unusu asubuhi; sasa konyagi ndo inizibe maskio. Basi mtafute mkuu wa vipindi TBC akupe hiyo clip kama nadaganya Au uliza yeyote aliesikiliza kipindi cha Tumwabudu Mungu TBC Taifa Fm jumapili ya leo, ukikosa hivyo basi mtafute mshikaji Ryoba.
Nakushauri tu na ufahamu ya kwamba Unywaji pombe au hangover sio kizuizi cha kufanya Tafakuri Jadidi!!! Labda kama ndo unajifunza kunywa Pombe. Pia jikite kwenye Mada badala ya kujadili pombe yangu.
 
b85c05ca286f10837cfac8c812c8bc7b.jpg
 
774d36724cdc08610b36f620f8c276d8.jpg
 
Back
Top Bottom