TBC-Ndivyo Sivyo !!

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Kuna kipindi cha TBC Taifa kinaitwa Ndivyo Sivyo.
Kipindi hiki ambacho hurushwa kama saa saba na nusu hivi usiku, maudhui yake ni mazuri sana kwa maana kwamba huwa kinajaribu kuangalia mambo ambayo hayaendi sawa kimfumo katika jamii yetu ya Kitanzania.

Tatizo nililoliona katika kipindi hiki ni kwamba, sijui updates zake hufanyika baada ya muda gani. Kwani nakumbuka nilisikiliza mara ya mwisho kama miezi mitatu hivi iliyopita, cha kushangaza nimekisikia tena leo (usiku wa jana kuamkia leo) mahojiano yaliyofanyika humo yalihusu dada zetu wanaosakata kabumbu (footbal) kumbuka ni miezi mitatu tangu nilisikiliza mara ya mwisho na bado kinarushwa vilevile, KULIKONI?

Wana JF mwenye direct contact na Mkurugenzi wa TBC atusaidie ili Tido atuambie tatizo ni kwamba hakuna topic zingine za update mambo?

Au kwa kuwa vipindi vyenyewe ni vya usiku bora liende?

Nawasilisha !
 
Back
Top Bottom