Janga la kuwa High Blood Pressure nalo limenifata leo baada ya balaa la hatihati kuambukizwa Ukimwi

Mfalme_wa_Nyika

JF-Expert Member
May 24, 2023
391
859
Ukisikia kama kuna pepo la magonjwa linampango wa kukuandama nakukuangamiza nadhani ndio huku.....

Wakuu na madaktari wa jf nawapa heshima zenu wasalaam....niende kwenye mada...

Takribani wiki mbili zilizopita nimetoka kumaliza kutumia dawa za PEP hii ni baada yakufanya mapenzi na na binti ambaye baadae niligua ni muathirika wa ukimwi, Mungu anasaidia hii ni wiki takribani ya saba toka kile kitendo na nimepima majibu yangu ni NEGATIVE.

Kiukweli hakuna kipindi kigumu nilipitia kama kipindi hiko chakumeza ile midawa ya PEP na kipindi hiki kwa ujumla kujua hatma yangu stress level iko juu sana.

Nimekuwa nikiishi kwa hofu mno kipindi hiki cha takribani miezi miwili, sasa leo nilitaka kwenda kufanya kipimo cha full blood picture ila nilipoanza kupimwa tu pressure na uzito niliamua kuahirisha mengine nirudi nyumbani kutafakari.

Nimepimwa nimekutwa na pressure ya 140/90 na uzito umeongezeka toka kilo 68 mpaka kilo 79, kitu ambacho sio kawaida yangu, mara ya mwisho niliendaga hospitali takribani miezi mitatu na sikuwahi kuambiwa nina pressure na uzito wangu mara nyingi unacheza 68 ikizidi sana 70 kg.

Naombeni ushauri wenu naogopa kuwa mtu wa hypertension nifanyeje!? Ukiniona niko kawaida kabisa, mimi situmii pombe, sigara wala kusema kula chumvi sio kivile sana na nina miaka 33 tu, pia ni mtu sana wa mazoezi, ni kwamba baada yakupata janga la kufanya mapenzi muathirika maisha yangu yakawa shaghala bagala miezi ya hivi karibuni niko na hofu na mapigo ya moyo hayako vizuri.

Nawaza hii pressure ya 140 kwa 90 nimeitoa wapi!? Na je ninawezaje kuwa normal nifanyaje!? Daktari aliniambia hii sio issue sana ingawa ni hatua za awali kuwa naweza kuwa mtu wa pressure, kimoyomoyo nikasema ananipa moyo tu, mimi naogopa....

Nawaza nirudi nyumbani niague mizimu maana naona kams majanga yananifata, la ukimwi ndio hilo Mungu anapambania, sasa hili la pressure ndio linanipa pressure kabisa maana najuta kufahamu najuta kwenda hospitali kujua naona ndio nazidi kuwaza tatizo.

Naombeni ushauri na mawazo....

Asanteni
 
140/90 kwa uzito huo bado sio tatizo. Ifuafilie daily kwa siku kama 15 hiv... Change life style yako... Punguza miwanga na stress then fanya mazoez atleast 75 minutes per week. Itarud poa tu. Usikimbilie midawa maana ukishaianza ndo umeianza milele.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Asante kwa ushauri naanza rasmi kubadili lifestyle
 
Iyo hypertension ni ishu ya hofu ya possibility ya kuwa na HIV. Ushauri wangu kabla miezi mitatu haijafika ili uwe na uhakika( ingawa kuna tests zinazoweza kuukamata hiv in 2 weeks) fanya research and pia watch testimonies za watu wanaoishi na vvu; normalize that picture na jione Km Wewe and assume the worst ili uone bado utakuwa binadamu na unaishi. Kumbuka HIV isn't a death sentence anymore and utaishi mpk uzeeni hata ukikutwa positive; so pole sana and regardless of the outcome learn from this and always use protection. So again cheki YouTube and cheki many people ambao wanaishi na VVU. Iyo itakusaidia sana na Pia mtafute mtu mmoja who u can share that burden with so stress zipungue.
 
Ukisikia kama kuna pepo la magonjwa linampango wa kukuandama nakukuangamiza nadhani ndio huku.....

Wakuu na madaktari wa jf nawapa heshima zenu wasalaam....niende kwenye mada...

Takribani wiki mbili zilizopita nimetoka kumaliza kutumia dawa za PEP hii ni baada yakufanya mapenzi na na binti ambaye baadae niligua ni muathirika wa ukimwi, Mungu anasaidia hii ni wiki takribani ya saba toka kile kitendo na nimepima majibu yangu ni NEGATIVE.

Kiukweli hakuna kipindi kigumu nilipitia kama kipindi hiko chakumeza ile midawa ya PEP na kipindi hiki kwa ujumla kujua hatma yangu stress level iko juu sana.

Nimekuwa nikiishi kwa hofu mno kipindi hiki cha takribani miezi miwili, sasa leo nilitaka kwenda kufanya kipimo cha full blood picture ila nilipoanza kupimwa tu pressure na uzito niliamua kuahirisha mengine nirudi nyumbani kutafakari.

Nimepimwa nimekutwa na pressure ya 140/90 na uzito umeongezeka toka kilo 68 mpaka kilo 79, kitu ambacho sio kawaida yangu, mara ya mwisho niliendaga hospitali takribani miezi mitatu na sikuwahi kuambiwa nina pressure na uzito wangu mara nyingi unacheza 68 ikizidi sana 70 kg.

Naombeni ushauri wenu naogopa kuwa mtu wa hypertension nifanyeje!? Ukiniona niko kawaida kabisa, mimi situmii pombe, sigara wala kusema kula chumvi sio kivile sana na nina miaka 33 tu, pia ni mtu sana wa mazoezi, ni kwamba baada yakupata janga la kufanya mapenzi muathirika maisha yangu yakawa shaghala bagala miezi ya hivi karibuni niko na hofu na mapigo ya moyo hayako vizuri.

Nawaza hii pressure ya 140 kwa 90 nimeitoa wapi!? Na je ninawezaje kuwa normal nifanyaje!? Daktari aliniambia hii sio issue sana ingawa ni hatua za awali kuwa naweza kuwa mtu wa pressure, kimoyomoyo nikasema ananipa moyo tu, mimi naogopa....

Nawaza nirudi nyumbani niague mizimu maana naona kams majanga yananifata, la ukimwi ndio hilo Mungu anapambania, sasa hili la pressure ndio linanipa pressure kabisa maana najuta kufahamu najuta kwenda hospitali kujua naona ndio nazidi kuwaza tatizo.

Naombeni ushauri na mawazo....

Asanteni
Mkuu pole sana kwa hayo maradhi yako ya Presha nitafute kwa wakati wako ili nikupe dawa presha yako ikae sawa isipande wala kushuka uguwa pole.
 
Back
Top Bottom