Uta Uta
JF-Expert Member
- Feb 2, 2016
- 3,739
- 8,736
Habari wanajamvi?
Mi ninasikitishwa sana na mwenendo wa kituo chetu cha Taifa TBC1 haswa kuhusuana na suala la michezo.
Mi nimeshuhudia mara kadha kituo cha Taifa cha Msumbiji kikionesha kila mechi wanayocheza timu yao ya taifa iwe ya kirafiki au ya mashindano.
Tena Msumbiji walienda mbali zaidi wakawa wanaonesha mechi zote za kombe la CAF wakati Samata anachezea Mazembe utadhani Samata ni raia waMsumbiji.
Lakini sisi wenyewe Tanzania hatujivunii hilo, kama Samata angekuwa Msumbiji mechi zote za Genk zingeoneshwa.
Tuache hilo, timu yetu ya vijana kwa mara ya kwanza inashiriki Michuano ya Afrika, inakuwaje kituo cha Taifa kinashindwa kuonesha.
Wananchi tunahimizwa kuwa wazalendo tumeitikiwa wito, inakuwaje kituo cha taifa kinashindwa kuwa mstari wa mbele kuongoza uzalendo?
Mh Waziri na mkurugenzi wa TBC liangalieni hilo swala kwa umakini. Nchi inatakiwa kuunganishwa kutoa sapoti kw timu yetu. TBC kwa hili mmeteleza sana.