Mara nyingi kipindi cha wosia wa baba cha TBC Taifa hupiga propaganda kuunga mkono kile kinachotekelezwa na serikali kwa wakati huo. Mfano kama serikali imekamata wala rushwa, itatafutwa hotuba ya Mwl akikemea rushwa ili kuaminisha umma kwamba hata enzi hizo Mwl alikemea.
Katika kipindi ambacho kimerushwa na TBC kwa siku kadhaa sasa Mwl anakemea mtu kujipa uwezo wa kufukuza kazi. "Utakuta kamtu kanamwambia mtu nimekufukuza kazi! unanifukuza kazi utalisha familia yangu?" anasikika akisema Mwl.
Katika clip nyingine Mwl Nyerere anasikika akisema "Sheria hii tuliifanya ngumu makusudi ili watu wasijigeuze wanyampala na kufukuza watu wanavyotaka" Mwl anasema watu walilalamika sana kwamba sheria hiyo inawafanya wawe na kiburi na kutofanya kazi. "Ndiyo, lakini kazi ni uhai hatuwezi kufukuza watu hovyo.
Hotuba hiyo aliitoa Mei Mosi 1981