TBC aibu tupu - Maigizo matupu

TBC aibu tupu - Maigizo matupu

Kwa trend hii atakayefuatia ni waziri wa nishati!!
Baada ya Dr. Mponda kuondoka (kama Rais ataridhia) basi madaktari watasema hawawezi kufanya kazi kwa sababu hakuna umeme wa uhakika hivyo Waziri wa Nishati aondoke.

Hivi tunategemea TV ya Serikali kweli ishangilie mgomo dhidi ya serikali? Aaaah jamani kweli?


Kwa nchi za wenzetu ambao wana viongozi na si watawala marafiki waliopeana ulaji, hilo nalo waziri angewajibika. Waziri mkuu Pinda si alipewa mfano na daktari wa temeke pale alipoenda kuzungumza nao muhimbili jinsi watoto wanne waliokuwa kwenye oxygen iliyokuwa inategemea umeme walivyofariki mmoja baada ya meingine baada ya umeme kukatika na hospitali haina generator na watumishi wa afya wakiwa wanaangalia tu. madaktari hao kama wangeamua kulichukulia serious wangeweza washauri wazazi wa watoto hao kuishtaki serikali, au wangeweza omba waziri wa nishati awajibishwe ( ingawa mngrpiga propaganda kama kawaida). Inahitaji mtu mwenye akili ya kuanalyse mambo kuweza kuunganisha ni vipi mtumishi wa afya anaweza kumuwajibisha waziri wa nishati.
 
Niliachaga siku mingi kuangaliaga hiyo tbc nikiangaliaga huwa anahisi kichefuchefu
 
Jamani ndugu zanguni, mimi sijui kama mna uchungu na mwenendo wa hii serikali kama mimi, nimeangalia habari TBC leo jinsi ambavyo wanatangaza etc, very stupid and no creativity, nafikiri mkurugenzy wake ameamua kutotumia akili yake kabisa, ***** mtupu!

Wanatangaza habari au wanajaribu kuwa wana CCM wa serikali corrupt ya Kikwete? naona watangazaji wake wamefikia hatua ya kuongelea and in a way if you read between the line kuwashauri madaktari wasigome, haya mi madudu na ujinga ambao hata mwanangu wa miaka 10 hawezi kufanya.

Wanaongea tu kuwa watu wanakufa, na kuwalaumu madaktari, can you imagine hii ni demand ya watu over 40,000 against 2 people ambao wanataka watu wa 2 tu wajiuzulu, ni lawama kwa madaktari kugoma watu wanakufa, lakini sio lawama kwamba inasababishwa na kukumbatia mawaziri wawili corrupted wa serikali corrupted!

Halafu hawa vilaza wakati mwingine wanatangaza kitu kingine, na kuweka video au taarifa tofauti na kile wanachotangaza, then wanasema kumradhi ..... very stupidy, nilikuwa sina uwezo wa kuweka DSTV kwangu, ila nimempigia Babu yangu nampa STAR times yangu then kwa udi na uvumba niweke DSTV.

My take:

Siku inakuja, nayo yaja, ambapo HAWA wote tuta wa Libya, subirini tu, nimechoka na huu ujinga.

Nawasilisha wakuu

Hivi JF kazi yake ni kupinga kila kitu cha serikali, na kila atakaetetea jambo la serikali kwa muono wake? JF haithamini uhuru wa mawazo wa kila mwananchi? Ili nisitukanwe au ili niwe popular ni lazima niiponde serikali?
 
Yanii kama Marini Hasani ndo no
one wa kuboa anapohoji mtu akiwa yupo tofauti na ccm!
 
Hivi JF kazi yake ni kupinga kila kitu cha serikali, na kila atakaetetea jambo la serikali kwa muono wake? JF haithamini uhuru wa mawazo wa kila mwananchi? Ili nisitukanwe au ili niwe popular ni lazima niiponde serikali?
Mbona wewe upo JF lakini unaitetea serikali? Huo ni muono wako si wa JF.
 
Sasa unashadidia madaktari wagome ili iweje? Wewe unanufaikaje na mgomo huo? Kama ni siasa fanyeni siasa za kistaarabu,ikulu haipatikani kwa utovu wa nidhamu!

Madaktari kugoma ni haki yao mkuu. 1. Serikali yetu haifanyii kazi maoni ya wananchi mpaka tugome 2. Wengine ndugu zetu ni hao madaktari, wanatulipia ada vyuoni (kama unavyofahamu seikali haitoi mkopo 100%) kwahiyo wakati wewe unasema hivyo nifikirie mimi ambaye ni ndugu yake Dokta aliyegoma

Halaf mkuu hakuna yeyote aliyeongelea kuhusu kuingia IKULU hapa, mgomo wa madaktari has nothing to do with "kuingia ikulu kwa nidhamu". It seems wewe ni mwanasiasa/kiongozi na si MWANANCHI MZALENDO
 
Poleni sana mnaoendelea kuangalia hii tv sisi huwa tunaiangalia kwenye maigizo na ze comedi tu taarifa ya habari ni DTV
 
Habari za jana zilikuwa hopeless na hovyo kabisa!
Imagine mtu anaamua kuonyesha habari za mgomo wa madaktari, halafu ameenda kurekodi huko mikoa ya Lindi Mtwara, na Ruvuma, sijui Ligula wapiwapi huko...my parts!..Kwanini wasionyeshe Ilala, Bugando, Temeke na mahospitali makubwa?
Halafu kabla ya kuongea na mtu nadhani wanamuonya ili aongee positively tu!

Yaani wafanyakazi wa shirika hili wamefungwa kamba shingoni kama kondoo anayepelekwa machinjioni, huku wakiamriwa kutangaza kwa mujibu wa matakwa ya chama!...Wabakaji wakubwa wa Professionalism!...puuuuuuuuf!
 
Wadau mwenzenu nipo gizani,umeme hakuna...wamenikatili hata habari sijaona,halafu masaburi ndio nini maana yake?

Masaburi ni jina la ukoo la Meya wa Jiji la Dar es salaam Bw. Didas ambaye wakati wa sakata la kuuzwa kwa UDA aliwatuhumu wabunge wa Dar kuwa wanatumia Makalio badala ya bongo zao kufikiri. WanaJF kwa kuzingatia mila na desturi za kitanzania ambazo zinakataza kutumia maneno makali wameamua kutumia jina la Masaburi badala ya Makalio kuwakashifu watu wanaodhaniwa kuwa hawatumii bongo zao kufikiri na kutafakari mambo. Nadhani ushanfahamu sasa.
 
Hivi JF kazi yake ni kupinga kila kitu cha serikali, na kila atakaetetea jambo la serikali kwa muono wake? JF haithamini uhuru wa mawazo wa kila mwananchi? Ili nisitukanwe au ili niwe popular ni lazima niiponde serikali?

Hapana JF inatoa ruksa kwa yeyote, hata wale wanaoiunga mkono serikali, kutoa maoni yao kwa uhuru. Wewe kama una point za kuunga mkono serikali na maamuzi yake mbali mbali zimwage tu hadharani. Ila uelewe tu kuwa kuna wana JF pia wana uhuru wa kupingana na mawazo yako. Hatuko hapa JF kutafuta popularity tuko hapa kutafuta taarifa na uelewa wa mambo mbalimbali.
 
Mi nishaacha kucheki hiyo TV CCM Siku nyingi sana. Pumbafu sana hawa vibaraka.

Nakushauri uwe unaiangalia TBC na TV station nyingine nyingi kama inavyowezekana. Ukitaka kuwa Great Thinker wa ukweli ni sharti uwe tayari kusikiliza maoni ya watu ambao haukubaliani nao kimtazamo kwa mambo yote. Kwa kuelewa mantiki ya mitazamo ya watu unaopingana nao unaweza kuhoji mantiki ya mitazamo yako na kuinoa ili iweze kuwa sahihi zaidi.
 
Tatizo letu watanzania tumezoea kulia lia sana! Kama unaona haikutendei haki achana nayo, tune station nyingine! Hamna anayekulazimisha kuangalia TBC1

TBC inaendeshwa kwa fedha za Watanzania na hivyo ni yetu Watanzania na inatakiwa ifanye kazi kwa utashi wetu (wamiliki). Ile kazi wanayofanya sasa hatuitaki kabisa. TBC kama Chombo cha habari tunataka ifanya kazi kwa uhuru na wala isitumiwe na baadhi ya watu kwa maslahi yao. Wanavyotangaza kwa namna ya kuonyesha kuwa Madaktari wana makosa kwanini hawataki kutuonyesha madai yao kinaganaga? Moja ya madai ya madaktari ni ukosefu wa vifaa muhimu katika Hospitali kama mashine za kufulia nguo na majenereta kwa ajili ya tahadhari ya umeme wa TANESCO kukatika. Kwa nini hakuna anayejibu hilo?

Suala la kujiuzulu kwa waziri wa afya na naibu wake linapotoshwa kwa makusudi kabisa. Hao madakatari kabla ya kugoma waliomba kuongea na mawaziri hao lakini hawakuwasikiliza madaktari, vivyo hivyo kwa katibu mkuu na Dakatari mkuu wa serikali katika wizara hiyo hiyo nao hawakuwa tayari kuwasiliza madaktari. Waziri mkuu alipochukua jukumu la kuwawajibisha katibu mkuu wa wizara ya afya (tofauti na alivyoshindwa kwa katibu mkuu wa nishati na madini) na Daktari mkuu wa serikali alitaka kutuambia nini? Alipoahidi kuwa atamshauri rais/ atamwachia rais kuhuusu suala la kuwawajibisha waziri na naibu alimaanisha nini?

Ni uzandiki wa pekee kwamba serikali leo inatuambia kuwa madai ya madaktari yanafanyiwa kazi na serikali baada ya kuundwa chombo cha kufanyia kazi madai yao kana kwamba waziri, naibu waziri, katibu mkuu na dakatari mkuu walinyimwa majukumu ya kuyafanyia kazi madai ya madakatari. Ni wazi kuwa waziri, naibu waziri, katibu mkuu na daktari mkuu walishindwa au walipuuzia madai ya madaktari. Kwanini leo madaktari walaumiwe kwa kuendelea na mgomo kama kwa kitendo cha serikali kutambua madai yao inaonyesha kuwa walipuuzwa huko nyuma?

Tunasihi vyombo vya habari hasa TBC waache kufanya propaganda bali waonyeshe yepi madai ya madaktari na na upi utetezi wa serikali unaojibu hoja za madai ya madaktari. kitendo cha kuwachukua wageni kwenye studio zao, wageni ambao wanakwenda kwa mtazamo wa kuitetea serikali.
 
Tatizo la nchi yetu, hao magamba wanadhani wana hati miliki na hata na vyombo vya habari vya vinavyoendeshwa na kodi za wana-TZ wote,
 
Tatizo kubwa la chombo cha utangazaji cha TBC licha ya kuwa ni chombo cha umma, kinachoendeshwa na kodi ya wa-TZ wote,lakini kimejigeuza kuwa chombo cha propaganda cha magamba,ndiyo maana walimtimua Tindo Mhando, kwa kuwa yeye hakutaka kuidhalilisha taaluma yake,alielewa kuwa mwanahabari yeyote lazima abalance story, sasa wamemteua huyu kada mwenzao Mshana kuongoza chombo hicho,ambaye yeye anakiongoza chombo hicho kutokana na maelekezo ya mabosi wake magamba!!
 
Kwani wewe hufahamu kuwa hiyo tbc ni mojawapo ya tawi la ccm...pamoja na baazi ya magazeti yao....?
 
Back
Top Bottom