Tb Joshua alivyonipa utajiri

Tb Joshua alivyonipa utajiri

hilo jina unalotumia ni la yesu huyu huyu wa bethlehemu nazaret brazil yerusalemu au wawapi anayegawa pesa kiasi hicho?
 
Waliokukejeli wamekejeli mimi naomba tu uni pm ukinieleza yanakopatikana hayo maji. malumbano sitaki
 
Ushudua wa kishetani huu. Kwann hujataja location za hiyo migahawa na hayo magari yanapiga route za kuzimu au?
Hata baiskeli ya anita hutanunua kama utaendelea kujilandua na mibangi ya mchana kweupe ewe bwana chacha!
 
Wewe mwei kweli biblia umeisoma kweli
Hasa injili???usichafue Hali ya hewaa humu Watu wakaanza kuhoji uhalali Wa mwez mtukufu wkt miez yote sawa.Hapa tunahoji nguvu za johua vs Ukweli Wa neno la Bwana yesu. Yesu kristo alikufa Na kufufuka hatmaye kupaa.alikufa msalabani ili neno litimie dats wy akayashinda maut.nakusihii sana omba kabla ya kusoma bblia then soma injili ktk ktabu chako cha Quran/Msahafu.utaufaham Ukweli Wa yesu kristo.
 
tena ndani ya miezi 4.
FUSSO 2, COASTER 3, NYUMBA 2, na RESTAURANT 3. tena wanalia chakula Bafuni nafasi na viti hazitoshi.
Innocent chacha huo ni uongo mkubwa au ni upiga debe kwa TB Joshua
kwa ninavyojua sasa hii biashara ya kuuza haya maji itashika ksi ndio maana hata Member na sisi kutoka Bara hatuhitaji kujua yalipo kwani huenda ni ya Mochwari
Soma (Mathayo 12;18 Tazama Mtumishi wangu niliyemteua, mpendwa wangu anipendezaye moyoni. Nitaiweka Roho yangu juu yake naye atatngaza hukumuyangu kwa mataifa yote
Mathayo 12;19 Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele wala sauti yake haitasikika barabarani
)
INNOCENT CHACHA badilikeni bado hamumfuati YESU
 
miezi 4 inakuwa milioni 240, kitu ambacho hakiwezekani.

Kwanza ni chini ya hapo Kwani jumapili hafungui tena atoe matumizi bila kusahau fungu la 10,kodi,umeme,maji,tra(tena kama anauza m2 kwa siku kodi yake si mchezo),bila kusahau ana wafanyakazi wangapi na anawalipa kiasi gani .Afanye hesabu halafu atupe maelezo vizuri
 
duh..!!viti vya mgahawa mpaka chooni na bafuni..?!!.
Tena kama kweli huyu jamaa ni mlokole atuambie mgahawa wake uko wapi,watu wa manispaa na TFDA waje wamlime faini kubwa yani anauzia chukula chooni
 
Actually unamtumikia shetani bila kujua... Yesu sio wa kuhusishwa na biashara za laki mbili kua milioni mbili. Haya makanisa yenu haya balaa sana..There are no shortcuts in life hao kina TB joshua wanajua walitendalo na wakipatacho
Mkuu lengo kuu la mleta mada ni kutaka kuchota watu akili hasa walala hoi, buzz word hapa ni "lala masikini hamka kesho TAJIRI!!" Ukisoma kwa umakini unajua wazi kwamba, baadae atajitangaza kwamba kapewa kibali au kaingia ubia na Nabii/Mtume JOSHUA wamefungua Branch yake hapa DAR kuwahudumia Watanzania, hivyo Watanzania wanaweza kupata/nunua maji sijui ya "uzima" kutoka kwake, hakuna haja ya kuyafuata Nigeria!! Ukinunua kwake ukajipaka tu - kesho yake utapata uwezo mkubwa wa Kimungu wa kuweza kujenga nyumba inanyo lingana lingana na Kempkisk, ma YATCH, Helicopter, Rolls Royce na Private jet juu, lunch yako itakuwa inatayarishwani Miami Florida, oh yes uta-kiss GOODBYE umasikini uliyo kithili - na Watanzania tulivyo, atawavuna WENGI.
 
tena ndani ya miezi 4.
Atuambie hizo investment zake ziko mtaa ngani na zinaitwaje tupate ushuhuda wa macho ,na pia serikali ipate kodi zake stahili nahisi kwa kasi hiyo huyu hakupata nafasi ya kujisajili sawasawa!
 
Nipe ushahidi wa maadiko ndugu yangu acha utapeli.... waoneeni huruma watanzania maskini kwa kuwauzia vitu visivyo kuwa na maana yeyote kama anointing water kwa dola 50 na kuwadanganya kuwa hiyo ni damu ya Yesu.
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ...."Hosea 4:6

TB Joshua ni mtumishi wa MUNGU na sisi wakristo kinachotumaliza ni ufarisayo tu. Unamtambua mtumishi wa MUNGU kuwa ni yule anayekuongoza tu. Jihadharini jamani.
 
Watu mnalalamika sana, Jamaa kasema wazi kua utajiri kautoa kwa tb joshua, mbona yuko specific kabisa.... kautoa kwa mwanadamu mnamlalamikia bure
 
Kama utakumbuka, miezi miwili iliyopita nilikuja na post juu ya kutoa shukrani kwa Yesu kwa kumtumia mtumishi wa Mungu TB Joshua kuniponya tatizo langu la uvimbe sehemu za siri ambalo lilikuwa likinifanya kushindwa kusimamisha uume wangu kwa miaka zaidi ya 4. Uponyaji wa tatizo langu ulifanyika kupitia maji maarufu ya ANOINTING WATER yanayoandaliwa na kutolewa na TB JOSHUA MINISTRIES.

Leo nataka nikushirikishe juu ya jinsi maji hayo yalivyonipa FUSSO 2, COASTER 3, NYUMBA 2, na RESTAURANT 3.

Nilianza biashara yangu miezi 4 iliyopita. Kalikuwa ni kamgahawa kadogo tu lakini kwasababu niliamini kwenye nguvu iliyomo ndani ya Yesu, sikuwa na hofu yoyote kuwa mafanikio yanakuja.

Kabla ya hapo, nilisikia shuhuda za watu mbaimbali ambao walitajirika baada yakutumia ANOINTING WATER kwa imani. Nikaamua kuyatumia haya maji kwenye biashara yangu kwa imani kubwa. Nilichokifanya ni kupuliza haya maji kwenye milango na makabati ya chakula huku nikiamrisha wateja wafurike kwenye biashara yangu kwa jina la Yesu.

Huwezi kuamini, mauzo yalibadilika kutoka shs laki 2 kwa siku hadi milioni 2. Watu wanajaa kwenye restaurant hadi nikaamua kuweka viti na meza eneo la jikoni na bafuni. Wateja wako radhi hata kula huku wamesimama au wamechuchumaa. Inapofika muda wakufunga huwa inabidi niwafukuze wateja vinginevyo tunaweza kukesha.

Ndani ya miezi 3, nimejenga nyumba 2, nimenunua coaster 3, fusso 2 na niko mbioni kufungua restaurant nyingine 2.

ASANTE YESU. ASANTE TB JOSHUA

heh! jaman tupeni na sisi watafuta ajira tupate ajira.
 
Nilichosema ni uhakika mtupu. Sijapunguza wala kuongeza neno. Mambo ya rohoni hayapaswi kuaminiwa na watu wa mwilini. Kwahiyo sipati shida ninapoona kuna idadi kubwa ya watu wanabishia ushuhuda wangu.
 
TB Joshua ni mtumishi wa MUNGU na sisi wakristo kinachotumaliza ni ufarisayo tu. Unamtambua mtumishi wa MUNGU kuwa ni yule anayekuongoza tu. Jihadharini jamani.

Nimeomba support ya maandiko kuwa kichupa cha maji ya TB ya Joshua ni damu ya Yesu...hayo mengine ni porojo tu. Ukristo wa kweli huongozwa na Biblia Takatifu sio maoni ya watu binafsi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom