Heading yako iko vizuri kuwa
TB Joshua amekupa utajiri. Umekosea hapo mwishoni ulipomtaja Yesu kwani
hakuna uhusiano wa anointing water na Neema ya Bure iliyotolewa na
Yesu Kristo wala haiuzwi kwa bei yeyote. Hiyo anointing water ni
ibada ya sanamu na ushirikina ambayo chanzo chake ni shetani. Shetani
anasema ukinisusujudia na kunitumikia nitakupa milki yote ya dunia. Yesu
anasema tafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na haki yake na hayo yote
mtazidishiwa...hapo usimmsingizie Yesu.
Sikiliza wewe mwanamahesabu. Kama jamaa kanunua fuso ya kwanza mwezi wa kwanza. mwezi wa pili kafungua mgahawa mwingine, mwazi wa tatu kanunua fuso na kufungua mgahawa wa tatu. Je mwezi wa nne atakuwa na uwezo kiasi gani? Utabakia Tshs 2M kama mahesabu yako yalivyo sema. Kweli hesabu ni tatizo kwa watanzania wengi
Ivi watu, lini tutaacha upuuzi? Lini tutajielewa?
Ivi wachungaji wangekua na uwezo huo kungeanzishwa hospitali kweli???????
Huyo Yesu ameshakufa, aliebaki ni Mungu, kwanini mnadai nguvu za mfu na kuzitukuza kuliko hata alivyokuwa hai?
Kama yeye muokozi kwanini alishindwa kujiokoa mwenyewe msalabani pale?????
:think: :think: :think:
Alifufuka mkuu ndio maana tunaamini la sivyo ukristo usingekuwepo, na kuhusu kufa msalabani ilikuwa lazima afe ili alipe deni la dhambi zetu ndio maana hakujiokoa. Ila kuna wajanja wachache wanatumia vibaya neema
tuliyopewa bure.
.
.
.
Huwezi kuamini, mauzo yalibadilika kutoka shs laki 2 kwa siku hadi milioni 2.
Ndani ya miezi 3, nimejenga nyumba 2, nimenunua coaster 3, fusso 2 na niko mbioni kufungua restaurant nyingine 2.
ASANTE YESU. ASANTE TB JOSHUA
Kama utakumbuka, miezi miwili iliyopita nilikuja na post juu ya kutoa shukrani kwa Yesu kwa kumtumia mtumishi wa Mungu TB Joshua kuniponya tatizo langu la uvimbe sehemu za siri ambalo lilikuwa likinifanya kushindwa kusimamisha uume wangu kwa miaka zaidi ya 4. Uponyaji wa tatizo langu ulifanyika kupitia maji maarufu ya ANOINTING WATER yanayoandaliwa na kutolewa na TB JOSHUA MINISTRIES.
Leo nataka nikushirikishe juu ya jinsi maji hayo yalivyonipa FUSSO 2, COASTER 3, NYUMBA 2, na RESTAURANT 3.
Nilianza biashara yangu miezi 4 iliyopita. Kalikuwa ni kamgahawa kadogo tu lakini kwasababu niliamini kwenye nguvu iliyomo ndani ya Yesu, sikuwa na hofu yoyote kuwa mafanikio yanakuja.
Kabla ya hapo, nilisikia shuhuda za watu mbaimbali ambao walitajirika baada yakutumia ANOINTING WATER kwa imani. Nikaamua kuyatumia haya maji kwenye biashara yangu kwa imani kubwa. Nilichokifanya ni kupuliza haya maji kwenye milango na makabati ya chakula huku nikiamrisha wateja wafurike kwenye biashara yangu kwa jina la Yesu.
Huwezi kuamini, mauzo yalibadilika kutoka shs laki 2 kwa siku hadi milioni 2. Watu wanajaa kwenye restaurant hadi nikaamua kuweka viti na meza eneo la jikoni na bafuni. Wateja wako radhi hata kula huku wamesimama au wamechuchumaa. Inapofika muda wakufunga huwa inabidi niwafukuze wateja vinginevyo tunaweza kukesha.
Ndani ya miezi 3, nimejenga nyumba 2, nimenunua coaster 3, fusso 2 na niko mbioni kufungua restaurant nyingine 2.
ASANTE YESU. ASANTE TB JOSHUA