Tazara: Wezi wapora gari kwa kutumia silaha

Tazara: Wezi wapora gari kwa kutumia silaha

Hee buguruni tena ? Nimetoka kusoma uzi wengine wavamia gari maeneo ya Dar group ,kweli kazi zimeanza
 
Mwezi wa sikukuu huu jamaa wanatafuta fedha za starehe
 
Unaweza kuta hela zenyewe za ufisadi ila hizo roho za watu tu!
 
Wazee hizo shaba mzisikie tu! Siku hizi wamezirogea yaani risasi zinapinda kona zinafuata damu ilipo, ndio maana TZR hukaa mita 200.
 
ha ha ha.. chichi polich tuko bize na Ukawa.. murah hayo majamaa hacha yachukue chao mapema mura.. over
 
mwizi hana huruma hata kwako mpita njia na pia hata escort ikiwepo wakijipanga wanatekeleza. Tusiwaunge mkono kamwe
 
IGP atueleze hawa askari 70 elf waliotolewa kipindi cha uchaguzi kwani hawapo tena, manake waliweka ulinzi imara wa watu wasilinde kura na wakafanikiwa kwa hilo, sasa kwanini wasiendelee kulinda raia na mali zao, au wale walimwagwa kwa kupiga raia wakiwa wanalinda kura zao, hii nchi bana, nilishangaa kusikia askari 70 elf nikasema hii nchi ina ulinzi wa kutosha watu tunaweza tukalala milango wazi bila kuvamiwa, askari 70 elf ni wengi sana, jana nasikia tazara watu wameporwa, akina kova tunataka ufafanuzi kwa hili msitoe askari kutupa mkong'oto raia tusio na hatia na majambazi yanapeta tu
 
Askari rushwa Tanzania kuna askari labda uozo jambo mpaka waamue wao
 
Mkuu, kuna watu walikuwa wanahangaika kupiga picha gari iliyokutwa na maswaibu baada ya vijana wa kazi kutokomea kwa kutumia usafiri pendwa! Najua wengine wapo huku, muda si mrefu watatupatia picha zote muhimu.

Mkuu naona kama vile unawasifia hao majambazi, na kama watasoma maelezo yako watajisifu na kuona wamefanya kazi nzuri
 
Tulianza kusahau matukio kama haya!!!!!!!!!!!!!!!
 
Vijisenti tu hovyp.msiwe nashaka
 
Back
Top Bottom