Tazama ramani utaona nchi nzuri (wimbo)

Tazama ramani utaona nchi nzuri (wimbo)

jamaan msaada naomba mwenye wimbo huo tazama raman utaona nchi nzuri.naupenda sana wimbo huo lkn sijui nitaupata vp.sipo dar mwenye wimbo huo naomba auupload tuupate bse najua wengi wanaupenda.
natanguliza shukran

Ndio nasikia ULIKUWA WIMBO WA TAIFA TEULE; Kabla ya MAMBO YA UKOMBOZI KUWAINGIA VIONGOZI WETU
 
Siku hizi watunzi wetu wanajua kutunga nakupenda mpenzi tu
 
huu ndo uwe wimbo wa taifa na wapemba na waunguja wote walazimishwe kuuimba
 
Nakushauri uende kwenye radio station yoyote unaweza upata , mm mwenyewe ninautafuta sana ngoja nikikumbuka nitaenda UPLANDS FM NJOMBE nione kama wanao
 
mimi nilikua na mdogo wangu mtoto wa mjomba wangu akiwa darasa la nne, basi kila nilikua nikienda kwa mjomba namwambie niimbie wimbo wa Tazama ramani. basi anauimba woote nafurahi sana
 
Kwa nini huu wimbo hawauimbi shuleni? Inawezekana ndiyo sababu pia ya watoto kufeli.
Maana hawapati motisha za kuwafanya waipende nchi yetu au yao.
 
nenda duka lolote la vitabu kanunue kitabu cha OXFORD CIVICS IN FOCUS BOOK 4 umeandikwa wote.
 
Mkuu huo sio wenyewe huo ni "Tanzania Tanzania". Wimbo wa "Tazama Ramani" uko tofauti sana na ni mzuri sana! Na mie natamani niusikie tena.

"Tazama ramani utaona nchi nzuri...
yenye mito na mabonde mengi ya nafakaaa...
nasema kwa kinya halafu kwa kufikiriii (nadhani nimechapia hapa) ....
nchi hiyo mashuhuru huitwa Tanzaniaaaa....
majira yetu hayaaaa ....
yangekuwaje sasaaaaa...
utumwa wa nchiii Nyerere ameukomeshaaaaa...."

Safiii
 
jamaan msaada naomba mwenye wimbo huo tazama raman utaona nchi nzuri.naupenda sana wimbo huo lkn sijui nitaupata vp.sipo dar mwenye wimbo huo naomba auupload tuupate bse najua wengi wanaupenda.
natanguliza shukran

watu Wa Radio One watatusaidia kwa hili.kuna kipindi fulani ambacho baba Wa Taifa anasikika, kabla husikika wimbo Wa tazama ramani, tuambieni wapi tutazipata nyimbo hizi za kuienzi nchi yetu
 
Kama kuna yeyote mwenye wimbo wa Tazama Ramani Utaona Nchi Nzuri mp3 naomba autupie.
Nimetafuta kwenye Google Search Engine bila mafanikio. Naupenda sana na nina muda mrefu. sijausikia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom