Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,101
- 8,032
1. Paulo, aliyefahamika awali kama Sauli, alikuwa Farisayo aliyejitoa kuwaudhi Wakristo wa kwanza. Alishiriki moja kwa moja katika kuuawa kwa Stefano na alikuwa na chuki kubwa dhidi ya jina la Yesu.
2. Alikutana "live" na Yesu na kubadilishwa kabisa. Akiwa njiani kwenda Dameski ili kuwakamata Wakristo, Yesu mwenyewe alimtokea kwa nuru kuu na kumwambia: "Sauli(Paulo) mbona waniudhi?" Tangu siku hiyo, Paulo aligeuzwa kabisa, kutoka kuwa mtesaji hadi kuwa Mtume jasiri wa Injili.
3. Alitumiwa na Mungu kwa viwango vya juu. Mungu alimpa Paulo neema ya pekee ya kufundisha mataifa. Kupitia yeye, tunapata mafundisho muhimu ya Ukristo kama vile:
Paulo bado anaendelea kuibua hisia kali duniani. Jina lake halikomi kutajwa katika makanisa, vyuo vikuu vya teolojia, mijadala ya imani na hata mitandaoni. Barua za Paulo ndio sehemu kubwa ya Agano Jipya, na zinaendelea kuongoza mamilioni ya waumini ulimwenguni. Kwa sababu hiyo, shetani hatulii, anahangaika kuwashawishi watu wapotoshe mafundisho ya Paulo. Hii yote ni kwa sababu Paulo alifunua siri za Mungu kwa watu wa mataifa.
5. Yesu alipomtokea Sauli(Paulo) hakumuuliza: “Mbona unawaudhi Wakristo?” Bali alimuuliza: “Sauli, Sauli, mbona waniudhi?” (Mdo 9:4)
Swali hilo ni ishara kwamba kumbe kuipinga Injili ni sawa na kumuudhi Yesu mwenyewe. Kwa hiyo, mtu yeyote anayeshiriki kueneza uzushi dhidi ya Ukristo wa kweli, anayeshambulia mafundisho ya Paulo au ya Yesu Kristo, anaulizwa pia na Yesu: “Mbona waniudhi?”
Kama dhamiri yako inakushuhudia kwamba umekuwa ukimuudhi Yesu, usiendelee kuwa mkaidi. Tubu sasa. Mungu aliyembadilisha Sauli atakusamehe, na ikimpendeza, anaweza kukufanya chombo safi cha kueneza kweli ya Neno la Mungu. Ukiendelea kushupaza shingo, kumbuka Maandiko haya: "Anayeonywa mara nyingi akawa mkaidi, atavunjika ghafla asipone tena." (Mit 29:1)

- Wokovu unapatikana kwa neema, kwa imani katika Yesu Kristo, si kwa matendo (Waefeso 2:8–9)
- Anayempokea Yesu anakuwa kiumbe kipya (2 Kor 5:17)
- Matumaini ya kufufuka kwa waliokufa katika Kristo, siku Yesu atakapokuja (1 Kor 15)
- Utatu Mtakatifu: Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (2 Kor 13:14).
- Jinsi tunavyopaswa kuishi kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu badala ya kuongozwa na tamaa za mwili (Rum 8; Gal 5:22–25)