Tawala tatu ndani ya Familia. Chunga Sana!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
TAWALA TATU NDANI YA FAMILIA

Na. Robert Heriel

28june2019

Katika Familia kuna vipindi vitatu ambavyo kila kipindi kinamtawala wake. Na kila utawala unaathari ndani ya familia. Mara nyingi utawala wa kwanza ndio hutoa mwelekeo wa familia husika.

Zifuatazo ni tawala zinazotokea ndani ya familia nyingi;

1. UTAWALA WA BABA
Hichi ni kipindi ambacho mwanaume huwa katika ufalme wake. Kipindi hiki ndicho Baba huwa kauli ya mwisho ndani ya familia. Pia Baba ndio nguzo muhimu ndani ya nyumba katika awamu hii ya kwanza. Yeye ndiye hutoa muelekeo wa Familia kuwa itakuwa ya aina gani mbeleni. Utawala huu mara nyingi unachangamoto za kiuchumi na kimahusiano kwani Baba bado damu inachemka. Huanza umri wa miaka 18 ~ 49. Kuanzia siku ya uchumba mpaka ndoa. Baba unatakiwa uilee familia kwa upendo kwani usipofanya hivyo madhara yake utayaona kwenye awamu ya pili ambayo Mama ndiye huingia utawalani. Ifundishe familia yako kuwa na umoja na ushirikiano. Vinginevyo chamoto kinakuja kwenye Tawala mbili zitakazofuata baada yako.

2. UTAWALA WA MAMA
Kipindi hiki huanza mwanaume akiwa na miaka 50 mpaka 65. Hapa mama ndiye huwa na mwelekeo wa Familia. Yeye ndio nguzo muhimu kwa familia husika. Utawala wake kwa kiasi kikubwa unaimarishwa na nguvu kutoka kwa Watoto ambao muda huo ndio wanamaliza chuo na wanaanza kujitegemea. Mama hapa kama aliteseka au hakupata upendo kwenye utawala wa kwanza basi muda huu ndio wa yeye kulipa kisasi. Na kama alipata mapenzi basi hulipa fadhila. Utawala huu mwanaume huweza pata manyanyaso kama sio kuuawa kabisa. Umri huu ni hatari sana kwa utawala wa kwanza kama haukuwa na haki na usawa. Ila ni kipindi kizuri sana ikiwa utawala wa kwanza ulikuwa fair kwani ni muda wa kula matunda ya ujanani.

3. UTAWALA WA WATOTO
Hiki ni kipindi ambacho watoto wameoa na kuolewa na wanafamilia zao. Kipindi hiki watoto ndio huwa na maamuzi ya kila kitu ndani ya familia. Wao ndio wenye muelekeo wa familia. Mara nyingi utawala huu huungana na Mama hasa ikiwa Baba alikuwa mkorofi kwenye utawala wake. Pia kama Baba hakuijenga familia iwe na umoja na upendo. Utawala huu hudondosha rasmi Familia hiyo na inapotea katika ramani. Utawala huu huzingirwa na Vifo vya utawala wa Kwanza au utawala wa pili.

Mwisho, Watu waishi kwa Upendo katika familia kila mmoja aingiapo kwenye utawala wake.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi
0693322300
 
Basi umeeleweka na kwa maana hiyo tuzingatie yafuatayo:
Utawala wa baba usipokuwa na msimamo kwa kuogopa kwamba ukizeeka mama atashirikiana na watoto kukunyanyasa basi mama atachukua usukani mapema na familia itaenda ki-mama mpaka uzeeni.

Ili kukabiliana na hilo, wekeza kwenye rasilimali na miliki rasilimali mpaka uzeeni ili usiwe tegemezi kwa watoto au mke wako badala yake wakutegemee wewe au wakuongezee kwa kile ulichonacho.
 
Basi umeeleweka na kwa maana hiyo tuzingatie yafuatayo:
Utawala wa baba usipokuwa na msimamo kwa kuogopa kwamba ukizeeka mama atashirikiana na watoto kukunyanyasa basi mama atachukua usukani mapema na familia itaenda ki-mama mpaka uzeeni. Ili kukabiliana na hilo, wekeza kwenye rasilimali na miliki rasilimali mpaka uzeeni ili usiwe tegemezi kwa watoto au mke wako badala yake wakutegemee wewe au wakuongezee kwa kile ulichonacho.


Umenielewa haswa Mkuu
 
Utawala wa Pili

*ilishaandikwa katika vitabu vitatakatifu "Ishini nao kwa akili" na hii ni kuanzia siku ya kwanza ya 6 x 6
 
Basi umeeleweka na kwa maana hiyo tuzingatie yafuatayo:
Utawala wa baba usipokuwa na msimamo kwa kuogopa kwamba ukizeeka mama atashirikiana na watoto kukunyanyasa basi mama atachukua usukani mapema na familia itaenda ki-mama mpaka uzeeni. Ili kukabiliana na hilo, wekeza kwenye rasilimali na miliki rasilimali mpaka uzeeni ili usiwe tegemezi kwa watoto au mke wako badala yake wakutegemee wewe au wakuongezee kwa kile ulichonacho.
Mkuu hii mentality ndio inaponza washua wengi, amini mali sio kitu kabisa linapokuja swala la kuishi kama familia na amani ya familia.

Unaweza ukawa na mali zakutosha alafu ukawa na familia iliyoparaganyika, yaani wewe baki na mali zako alafu mkeo naye anatafuta mali zake na watoto nao wanatafuta mali zao. Mkuu hapo sonona haikuachi salama daima utakuwa mtu wa mawazo sana.

Usiwaze kutumia mali kama fimbo yakuichapa familia yako hapo utaanguka Mkuu, na kumbuka nguvu huwa zinaisha ukizeeka kuna maradhi yataambatana na wewe pia, hapo hautakuwa na jeuri tena.

Wanaume wengi tunakuja kukumbuka swapa la kuishi kama familia ukubwani sana na inakuwa tushachelewa.

Kipaumbele chako siku zote kiwe familia yako na sio wewe kuwa mwamba kwenye familia yako. Kuwa na familia imara inaitaji akili sana.
 
Back
Top Bottom