Tawala tatu ndani ya Familia. Chunga Sana!

Tawala tatu ndani ya Familia. Chunga Sana!

TAWALA TATU NDANI YA FAMILIA

Na. Robert Heriel

28june2019

Katika Familia kuna vipindi vitatu ambavyo kila kipindi kinamtawala wake. Na kila utawala unaathari ndani ya familia. Mara nyingi utawala wa kwanza ndio hutoa mwelekeo wa familia husika.

Zifuatazo ni tawala zinazotokea ndani ya familia nyingi;

1. UTAWALA WA BABA
Hichi ni kipindi ambacho mwanaume huwa katika ufalme wake. Kipindi hiki ndicho Baba huwa kauli ya mwisho ndani ya familia. Pia Baba ndio nguzo muhimu ndani ya nyumba katika awamu hii ya kwanza. Yeye ndiye hutoa muelekeo wa Familia kuwa itakuwa ya aina gani mbeleni. Utawala huu mara nyingi unachangamoto za kiuchumi na kimahusiano kwani Baba bado damu inachemka. Huanza umri wa miaka 18 ~ 49. Kuanzia siku ya uchumba mpaka ndoa. Baba unatakiwa uilee familia kwa upendo kwani usipofanya hivyo madhara yake utayaona kwenye awamu ya pili ambayo Mama ndiye huingia utawalani. Ifundishe familia yako kuwa na umoja na ushirikiano. Vinginevyo chamoto kinakuja kwenye Tawala mbili zitakazofuata baada yako.

2. UTAWALA WA MAMA
Kipindi hiki huanza mwanaume akiwa na miaka 50 mpaka 65. Hapa mama ndiye huwa na mwelekeo wa Familia. Yeye ndio nguzo muhimu kwa familia husika. Utawala wake kwa kiasi kikubwa unaimarishwa na nguvu kutoka kwa Watoto ambao muda huo ndio wanamaliza chuo na wanaanza kujitegemea. Mama hapa kama aliteseka au hakupata upendo kwenye utawala wa kwanza basi muda huu ndio wa yeye kulipa kisasi. Na kama alipata mapenzi basi hulipa fadhila. Utawala huu mwanaume huweza pata manyanyaso kama sio kuuawa kabisa. Umri huu ni hatari sana kwa utawala wa kwanza kama haukuwa na haki na usawa. Ila ni kipindi kizuri sana ikiwa utawala wa kwanza ulikuwa fair kwani ni muda wa kula matunda ya ujanani.

3. UTAWALA WA WATOTO
Hiki ni kipindi ambacho watoto wameoa na kuolewa na wanafamilia zao. Kipindi hiki watoto ndio huwa na maamuzi ya kila kitu ndani ya familia. Wao ndio wenye muelekeo wa familia. Mara nyingi utawala huu huungana na Mama hasa ikiwa Baba alikuwa mkorofi kwenye utawala wake. Pia kama Baba hakuijenga familia iwe na umoja na upendo. Utawala huu hudondosha rasmi Familia hiyo na inapotea katika ramani. Utawala huu huzingirwa na Vifo vya utawala wa Kwanza au utawala wa pili.

Mwisho, Watu waishi kwa Upendo katika familia kila mmoja aingiapo kwenye utawala wake.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi
0693322300
Umeeleza vizuri sana kiongozi! Na hilo hitimisho limenikosha sana! Kuna mavi-jana hapa nayaangalia tu yanavyoendesha mambo nabaki nasema hiiiii!! Eti kijana linafukuza mke na watoto wakaanze maisha yao lenyewe libaki na mchepuko kwenye nyumba waliyojenga na mke wake wa ndoa? Pumbavu kabisa! Mtoto mpaka ameanza kusema yaani mimi huyu baba kwangu ni takataka kabisa! Inaumiza sana!!
 
Umeeleza vizuri sana kiongozi! Na hilo hitimisho limenikosha sana! Kuna mavi-jana hapa nayaangalia tu yanavyoendesha mambo nabaki nasema hiiiii!! Eti kijana linafukuza mke na watoto wakaanze maisha yao lenyewe libaki na mchepuko kwenye nyumba waliyojenga na mke wake wa ndoa? Pumbavu kabisa! Mtoto mpaka ameanza kusema yaani mimi huyu baba kwangu ni takataka kabisa! Inaumiza sana!!


Game itageuka aombe Afe mapema hiyo ndio pona pona yao
 
Game itageuka aombe Afe mapema hiyo ndio pona pona yao
Sisi tupo tunamwangalia tu! Mke ndio kwanza anahangaika kutafuta kiwanja ajenge nyumba yake na watoto wadogo, baba lipo tu kwenye nyumba na hawara!
 
Hizo tawala zote haziwahusu kbs wale wazee wa kitonga vibenten(vijana) maana wao nguvu kumbwa inawaza kwenye kuvizia ma sugar mami wenye mtonyo tu
 
Utawala wa kwanza huishi kwa mateso na hata kufa kwa sonona ikiwa baba hakuwajibika kwa wanawe na kumnyanyasa mkewe (utawala wa pili) enzi za utawala wa kwanza.


Na hapa Kama Wababa ukileta mchezo unaweza kuugua magonjwa yanayotesa
 
Umechambua vizuri sana na kumbuka watoto uwa hawamwachi mama so tawala ya pili na ya tatu inamuua taratibu tawala ya kwanza. Wanaume tunakufa mapema kwa mengi
 
Umechambua vizuri sana na kumbuka watoto uwa hawamwachi mama so tawala ya pili na ya tatu inamuua taratibu tawala ya kwanza. Wanaume tunakufa mapema kwa mengi


Na tawala ya Kwanza unapofanya matendo ya kiharamia kwenye awamu yake ndio hupata matokeo mabaya zaidi uzeeni
 
Basi umeeleweka na kwa maana hiyo tuzingatie yafuatayo:
Utawala wa baba usipokuwa na msimamo kwa kuogopa kwamba ukizeeka mama atashirikiana na watoto kukunyanyasa basi mama atachukua usukani mapema na familia itaenda ki-mama mpaka uzeeni.

Ili kukabiliana na hilo, wekeza kwenye rasilimali na miliki rasilimali mpaka uzeeni ili usiwe tegemezi kwa watoto au mke wako badala yake wakutegemee wewe au wakuongezee kwa kile ulichonacho.
TAFUTA PESA MKUU....HAYO MAELEZO YOTE BILA PESA NI KAZI BURE
 
TAFUTA PESA MKUU....HAYO MAELEZO YOTE BILA PESA NI KAZI BURE


Pesa pekeake haitoshi.

Pesa na kujenga upendo ndani ya familia ndio muhimu.

Pesa hizo hizo zinaweza zikakutoa roho, aidha Mkeo au watoto wako wakakuangamiza kisa pesa
 
Back
Top Bottom