Tatu Kikwete ni jipu litumbuliwe

phantomX

Member
Jul 22, 2015
15
16
Katika halmashauri ya Kibaha kuna hili jipu linaitwa Tatu Kikwete, huyu ni mkurugenzi wa halmashauri ya kibaha vijijini.

Jipu hili limekuwa likiwanyanyasa sana watumishi wa wilaya hiyo kisa ana undugu na yule jamaa (Jakaya Kikwete) na hata hicho cheo alikipata kwa kubebwa tu maana elimu yake ni diploma in education lakini anawanyanyasa watu wenye elimu zao.

Ana lugha chafu kutukana watumishi hadharani, kuwanyima haki za msingi, kuwagawa watumishi yaani anafanya ofisi kama mali yake ya nyumbani.

Mwisho naomba serikali iwe inatoa vyeo nyeti kama hivi kwa kuzingatia elimu pia na sio ujanja ujanja haiwezekani subordinate wakawa na elimu na upeo mkubwa kuliko superbordinate ndio mwanzo wa kupata viongozi vilaza.

Naomba wenye mamlaka wafanye uchunguzi kisha watumbue tu haya majipu ya awamu ya nne yaliyovimba kindugundugu.

Edited; naona kuna watu wengine hapa wanaleta mahaba kwa hili jipu itakuwa nao ni beneficiaries... Kama nilivyoandika hapo juu uchunguzi ufanyike na jipu litumbuliwe sikuja kuandika essay hapa hadi nianze kujielezea na kutoa mifano
 
Kwani mfanyakazi wa serikali ana haki gani? TATU kaza buti mtumbue huyu na kihele hele chake, muache Dada yetu atumie vizuri zamu yake aisee, wivu mbayaaaa
 
sure name zingine hazitumbuliki..

hakuna raisi yoyote Tanzania mwenye jeuri ya kutumbua sure name ya marais wenzake waliopita...

maana anajua nae miaka 10 tu anasepa.. wanalindana wenyewe kwa wenyewe

hii hadi ccm iondoke madarakani...
 
Mkuu kama hizo tuhuma ni za kweli wasiliana na mkurugenzi wa maadili au mkurugenzi msaidizi wake pale ofisi ya utumishi wa umma iliyo karibu na TPA Tower (Feri). Hatachukua round.
uzuri huyu jamaa yupo humu jukwaani naamini atalifanyia kazi, jamaa ananifurahisha huwa ana deal na tuhuma zinazotoka vyanzo vyovyote ingawa mtoa mada alitakiwa aelekeze tuhuma zake na vielelezi (references) ie siku fulani alifanya hivi nk
 
Ana lugha chafu kutukana watumishi hadharani, kuwanyima haki za msingi, kuwagawa watumishi yaani anafanya ofisi kama mali yake ya nyumbani.

Hebu wataje aliowadhalilisha hadharani ili ahukumiwe kwa haki
 
Kuna Mmoja anamwita kikwete mjomba alikuwa mpakani namanga kama Ajenti alikuwa anafanya michezo michafu na viongozi wa pale walikuwa wanapata kigugumizi alinitia hasara sitomsahau .
 
Katika halmashauri ya Kibaha kuna hili jipu linaitwa Tatu Kikwete, huyu ni mkurugenzi wa halmashauri ya kibaha vijijini.

Jipu hili limekuwa likiwanyanyasa sana watumishi wa wilaya hiyo kisa ana undugu na yule jamaa (Jakaya Kikwete) na hata hicho cheo alikipata kwa kubebwa tu maana elimu yake ni diploma in education lakini anawanyanyasa watu wenye elimu zao.

Ana lugha chafu kutukana watumishi hadharani, kuwanyima haki za msingi, kuwagawa watumishi yaani anafanya ofisi kama mali yake ya nyumbani.

Kutokana na tabia zake halmashauri imedumaa na mapato yamedidimia.

Mwisho naomba serikali iwe inatoa vyeo nyeti kama hivi kwa kuzingatia elimu pia na sio ujanja ujanja haiwezekani subordinate wakawa na elimu na upeo mkubwa kuliko superbordinate ndio mwanzo wa kupata viongozi vilaza.

Naomba wenye mamlaka wafanye uchunguzi kisha watumbue tu haya majipu ya awamu ya nne yaliyovimba kindugundugu.

Kabla sijatoa comment, naoma utulie halafu useme kwa ufasaha na mifano halisi:-

1. Anawanyima haki zipi za msingi? Naomba uzungumze bayana.

2. Anatukana matusi gani hadharani? Naomba uandike hayo matusi hapa na utoe mfano dhahiri.

3. Lugha chafu ni kama ipi? Unatakiwa kuainisha na kwa mifano halisi.

4. Anawagawa vipi watumishi? Weka wazi na mifaho halisi.

5. Mambo gani anayofanya ofisini ambayo yanatoa taswira kwamba ofisi sasa ni nyumbani? Tafadhali fafanua.

6. Naomba uwasaidie Mamlaka na kuwarahisishia kazi kwa kuainisha ni vipi huyu anafanya mapato ya halmashauri kudumaa? Tabia zake zipi zinapelekea mapato hayo kushuka. Tafadhali sana naomba ufafanue.

Vinginevyo ukiacha hivi utaonekana unaleta majungu yasiyo na ukweli na itampa nguvu kwamba kumbe yeye ni bora ndiyo maana akawa kiongozi kuliko na wewe ukawa hapo ulipo.

Suala la Elimu yake, linatakiwa liwasilishwe pia kwa mamlaka husika ili liangaliwe kwa namna yake hata kama hakuna haya mengine kama hayapo.

Naomba uwe precise and specific ili kuonyesha kwemba kweli hii habari inaukweli.

Kwa jinsi ulivyoiweka imekaa ki majungu, gadhabu na ki visasi zaidi!. Vuta pumzi, andika kwa utulivu na ufafanuzi.
 
sure name zingine hazitumbuliki..

hakuna raisi yoyote Tanzania mwenye jeuri ya kutumbua sure name ya marais wenzake waliopita...

maana anajua nae miaka 10 tu anasepa.. wanalindana wenyewe kwa wenyewe

hii hadi ccm iondoke madarakani...

usiishi kwa kukariri tumeanza kutumbua zenye surename za waziri wakuu wastaafu wa marais wastaafu its just a matter of time
 
Back
Top Bottom