Tatizo siyo watu wanaoishi "mabondeni" bali ni wale wanaoishi "magogoni"

Nyani, sasa tunazungumza; na ninaona umeenda na kugusa pembezoni mwa hoja. Hawa watu wa mabondeni wana sababu ya kuja na kuishi huko. Dar-es-Salaam ni mji mdogo sana ambao ungeweza kujengwa na kupangwa vizuri. Lakini angalia nyumba nyingi zilivyojengwa maeneo mengi ni bungalows; na chache sana zina ghorofa zaidi ya moja (siku hizi ndio maduplex n.k yanazidi. Watu wengi wanaishi kwenye nyumba hizi za chini na wengi wana uwezo wa kujenga nyumba ya aina hizo. Matokeo yake? Spiraling ya jiji la dar is more horizontal na siyo vertical kama yalivyo majiji ya wenzetu.

Hilo moja la pili ni vile vile hilo unalogusia. Sisi huku kwetu ukitaka kupanga unaweza kupanga kwa uwezo wako tu. Kuanzia mahali pa gharama ya 300USD hadi 2000usd (nazungumzia metro detroit). Na hii ni typical ya miji mingi Marekani. Hata New York ambapo tunaambiwa pana gharama sana ya real estate utashangaa watu wanaishi pembezoni na kufanya kazi downtown na kwa gharama nafuu lakini wenye uwezo wao wanaishi katikati kabisa ya jiji.

Sasa Dar ikoje? well mjini bado kuna nyumba nyingi ambazo ni za gharama za chini na kuna maeneo mengi ya wazi. Hapa ndio mgogoro ulipo - kwanini mtu aishi mbali na jiji kama kwa kuishi kwa gharama nafuu katikati ya jiji kunamuweka karibu nakazi na huduma mbalimbali? Watu wa mabondeni wanaamua kuishi maeneo hayo kwa vile wengi wao ni walalahoi na wafanyakazi wa ngazi za chini na wajasiriamali binafsi. Watumishi wengi wa umma wenye uwezo wao hutafuta viwanja na kupanga mbali na katikati ya jiji! Lakini wale ambao maisha yao yanategemea mara zote kudra za mwenyezi Mungu katikati ya jiji it makes sense - wanaenda kufanya shughuli zao na haiwatahitaji kwenda mbali. Wanaweza kwenda mahali poopote mjini kwa miguu na huduma zozote muhimu ziko karibu.

In short, hata ningekuwa mimi katika mazingira yao nadhani ningeweza hata kujenga kibanda changu huko huko mabondeni? why kwa sababu the symbiotic relationship kati ya walio nacho na wasio nacho yamekamilishwa mabondeni. Siwezi kushangaa hata mabondeni kuna minara ya simu na wateja wengi tu wa makapuni ya simu!
 
Upo Tanzania kweli wewe?
Nipo Tanzania na kama vipo over priced bado nauliza ni kwanini wakazi wa mabondeni walikataa viwanja vya buree. Kwahiyo tusitumie viwanja vya mauzo ya kawaida kufunika ukweli kuwa watu hawa walipewa viwanja vya bure. Hapo ndipo hoja yangu inaposimamia.
 
Mkuu viwanja viko overpriced Tanzania tena naweza sema kila kitu ni over priced kutokana na kwamba vilivyopo havitoshelezi.. demand kubwa kuliko supply. Swala na nyumba ndio kabisaa labda tufikirie upya maneno ya Mwanakijiji hapo juu..

Pili, Hivi kweli mkuu wangu mtu anapata riziki zake Dar mjini unataka kumpeleka nje ya mji sii ndio vijiji vya Ujamaa hivyo lakini kwa lugha ya kistaabu? Kwa nini watu walikataa vijiji vya Ujamaa wakati vilikuwa bure?...
Mkuu wangu watu wanatazama mkono uendao kinywani na Dar au mijini ndipo riziki hupatikana, Nchi haina kazi zaidi ya asilimia 50 ya vijana hawana kazi, wazee wetu elimu hawana halafu unataka waende wapi?...
 
Nipo Tanzania na kama vipo over priced bado nauliza ni kwanini wakazi wa mabondeni walikataa viwanja vya buree. Kwahiyo tusitumie viwanja vya mauzo ya kawaida kufunika ukweli kuwa watu hawa walipewa viwanja vya bure. Hapo ndipo hoja yangu inaposimamia.

Sababu ya watu kuishi mabondeni siyo moja tu. Uwezo wa watu kiuchumi nayo ni sababu. Mtu atakayelikataa hili basi atakuwa na matatizo.

Na atakayekataa kuwa real estate properties Tanzania haziko overpriced basi sijui nisemeje. Lakini sishangai sana kwa sababu watu wengi hilo la overpricing hawalioni Tanzania.
 
Mkuu viwanja viko overpriced Tanzania tena naweza sema kila kitu ni over priced kutokana na kwamba vilivyopo havitoshelezi.. demand kubwa kuliko supply. Swala na nyumba ndio kabisaa labda tufikirie upya maneno ya Mwanakijiji hapo juu..

Pili, Hivi kweli mkuu wangu mtu anapata riziki zake Dar mjini unataka kumpeleka nje ya mji sii ndio vijiji vya Ujamaa hivyo lakini kwa lugha ya kistaabau? Kwa nini watu walikataa vijiji vya Ujama wakati vilikuwa bure?...Mkuu wangu watu wanatazama mkono uendao kinywani na Dar au mijini ndipo riziki hupatikana, Nchi haina kazi zaidi ya asilimia 50 ya vijana hawana kazi, wazee wetu elimu hawana halafu unataka waende wapi?...

Sema wewe Bob maana wengine ni kama hatuaminiki na tunayoyasema! Na tena cha kushangaza zaidi kuna maeneo ambayo hata price quote unapewa kwa US dollars.
 
Tushajadili tatizo,
Then what is the solution?
Wataalamu wanisaidie, hivi pale haiwezekana ukatafutwa mlima maeneo kama kimara au mbezi ukasawazishwa halafu kifusi chote kikaletwa pale!!
Kisha ukaachwa mto uliojengewa kingo labda za upana wa mita hata 20 ambao unaweza kua "nevigable" kwa ajili ya kupunguza foleni!!
Pili kifusi kikikolea na kujishindilia sawasawa panajengwa maghorofa kadhaa kwa ajili ya kupangisha walalahoi!!
Mradi kama huu unaweza kujengwa na bwana miradi (NSSF).
Imekaaje hii wadau?
Tujadilini solution sasa
 
Serikali haikuanza leo kuzuia watu kujenga mabondeni. Na hao wanaojenga Mabondeni wanajua fika kuwa wamekatazwa na kwa kweli wanavunja sheria. Suala la kuwa Serikali ilikuwa wapi siku zote, tangu Nyumba inaanza kujengwa mpaka watu wanahamia na kuanza kuishi, hili ni suala jingine. Sie,kama Wananchi tunatakiwa tubalike, tusiwe na majibu mepesi kwenye masuala mazito. Mathalan, utamkuta mtu anauliza, 'mnatufukuza hapa mabondeni, mnatutaka twende wapi?' Tunaoathirika leo hii ni sie tulio mabondeni na si vinginevyo. Tunajiuliza kama kweli jeuri yetu ni kwa manufaa/hasara ya nani? Baina yetu na Serikali imekuwa kama ka mchezo fulani ka kuku na yai je nani alianza? Mwisho wa siku ni nani anayeumia? Tutafakari.
 
Hayo mabonde yanaonekana kwa maskini tu nchi hii. Kumbuka mabonde yamekuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu na waungwana wameishi nayo kwa urafiki mkubwa. Walipoingia mafedhuli wenye fedha nyingi, wakabadilisha matumizi yake kwa kujenga ma-godown, viwanda, ma-garage na kuelekezea mikondo ya maji kwa mafukara wa dunia, hao ndio wanaolaumiwa kwa kutokimbia mafuriko. Wale waliowapelekea hali hiyo wanapongezwa na kulindwa na jamhuri hii hii kwa kuwa ni wawekezaji!
 
Tushajadili tatizo,
Then what is the solution?
Wataalamu wanisaidie, hivi pale haiwezekana ukatafutwa mlima maeneo kama kimara au mbezi ukasawazishwa halafu kifusi chote kikaletwa pale!!
Kisha ukaachwa mto uliojengewa kingo labda za upana wa mita hata 20 ambao unaweza kua "nevigable" kwa ajili ya kupunguza foleni!!
Pili kifusi kikikolea na kujishindilia sawasawa panajengwa maghorofa kadhaa kwa ajili ya kupangisha walalahoi!!
Mradi kama huu unaweza kujengwa na bwana miradi (NSSF).
Imekaaje hii wadau?
Tujadilini solution sasa
Hii solution tunatazama jinsi ya kuzuia maafa yasitokee tena au tunatazama hawa watu kwa makazi yao?..

Mimi ningesema tu ya kwamba JK amsikilize Magufuli na hizi nyumba zinazojengwa leo kinyume cha sheria zibomolewe tuache kabisa habari za Machinga na kugeuza kila Nyumba duka hivyo zinaongezwa vipande hadi barabarani kuua mifereji. Matatizo ya Dar yametokana na sehemu nyingi kutokuwa na mirefeji ya maji na vizuri zaidi tuwe na mifereji ya chini kwa chini ambayo inaunganishwa kabla ya ujenzi wa barabara ama nyumba. Mbona Mwanza jamani wameweza?..Itakuwaje Dar mji mkubwa tunashindwa kabisa kujenga mifereji ya maji nasikia Kariakoo watu walikuwa wakipishana na makimba mji mzima unanuka..

Swala la hawa waliokuwa wakiishi Bondeni itabidi watafutiwe makazi mapya sii lazima wakae mjini.. Hasara hii lazima waikubali na tuikubali sote maana watu wamekufa na hatuwezi kujaribu kuzipoza roho zao kwa ujenzi wa maghorofa ambayo tunajua fika kwamba hawataiweza kodi wala hawatapewa wao kuishi ktk majumba hayo. Nyumba Dar ni Almasi, hatuna nyumba za kutosha na pengine itolewe amri makazi fulani hairuhusiwi kubomoa na kujenga nyumba isiyokuwa na ghorofa kadhaa na kwa ajili ya makazi ya watu.

Pili, hamisheni makao makuu Dodoma kupunguza ghasia za mjini ili mji wetu upate kupumua na kuangaliwa kama manispaa maanake hivi sasa imekuwa kama Dar ni mji wa viongozi..

Tatu, bandari za Tanga na Mtwara zitumike zaidi ili ya Dar na ifungwe taratibu kupisha sehemu yote ya bandari itumike kuujenga mji mpya utakao ungana na Kigamboni...Kama wanataka kujenga bandari nyingine Bagamoyo wajenge lakini hiyo ya Dar kwani haifai tena kupokea mizigo ila itumike kama bandari ya meli za utalii - cruise ship, Yatch club na highrise Condominiums zijengwe eneo lote la bandari na shoredepot zake kusogeza wafanyakazi wa mjini wapate kupanga karibu na mjini..Ni sehemu kubwa sana ya mji imepotezwa bure wakati bandari haiwezi kumudu mizigo.

Mwisho, sisi walalahoi tusaidiwe tu usafiri wa Train najua subway hatuna uwezo basi hata train la nje baada ya hilo liendalo mikoani waanzishe transit route la kutoka Mbezi au Kimara hadi mjini kutwa mara matu tu na ile ya Tazara pia itumike kwa usafiri wa mjini toka sijui wapi huko mabondeni...Hii itasaidia watu kuhamia maneno ya nje ya mji ikiwa rahisi kwao kuja mjini na kuwahi kazi, kisha ktk mpango wa muda mrefu ifikiriwe rail line ya kwenda Bagamoyo na nyingine ya kusini wakati Mabus ya mjini yakifanya kazi kuunganisha. Usafiri unapokuwa rahisi kutoka na kuingia mjini kutoka vitongojini ni rahisi watu kuhamia makazi mapya. Nipeni U Meya muone kazi ya Mheshimiwa Mkandara!... mkhuu khuu!
 
Sababu ya watu kuishi mabondeni siyo moja tu. Uwezo wa watu kiuchumi nayo ni sababu. Mtu atakayelikataa hili basi atakuwa na matatizo.
Na atakayekataa kuwa real estate properties Tanzania haziko overpriced basi sijui nisemeje. Lakini sishangai sana kwa sababu watu wengi hilo la overpricing hawalioni Tanzania.
Nadhani aliye na matatizo ni mimi kwa lugha yako njema.
Ninachosema hapa ni kuwa hawa watu walipewa viwanja bure wakakataa! Overprice inatoka wapi ukipewa kitu bure!

Hilo ni tofauti na bei ya viwanja kwa ujumla wake. Tusichanganye hoja ili kukwepa ukweli. Ukweli unabaki pale pale walikataa kuhama.

Pili, hatuwezi kuachia sheria kwa visingizio. Ndiyo maana miji ipo hovyo. Sheria lazima simamiwe kikamilifu na si hapa tu ndivyo ilivyo dunia nzima kwenye mipango miji.

Kinachotukwamisha watanzania ni kukwepa uwajibikaji na usimamizi wa sheria. Tumekuwa wazuri kutetea hata uvunjaji wa sheria.
Kujenga mahali pasiporuhusiwa ni ukikuaji wa sheria, na kukataa kuhamia eneo walilopewa BURE ni uzembe.
Tuambizane ukweli Watanzania, tusijifiche vichwa kwenye ardhi viwili wili vikiwa nje.
 
Mkuu kama nimemwelewa Nyani Ngabu alichosema ni kwanza viwanja maeneo yanayokubalika havishikiki hawa watu waliojenga Jangwani na Kigogo kinyume cha sheria hawan uwezo wa kununua viwanja sehemu yoyote ktk mji wa Dar na viwanja hivyo walipojenga vilikuwa bure na pia karibu na mjini ambako hupatia riziki zao, hivyo tunazungumzia Dar Es Salaam na sio nje ya mji.

Ukitaka kuwandoka watu Dar kwa kuwapa viwanja nje ya mji lazima pia ufikirie hawa watu wataweza vipi kufikia sehemu za kupatia riziki zao yaani wataweza vipi kuja Dar na kuendelea na maisha yao jambo ambalo serikali imeshindwa kulitazma isipokuwa kufuta sheria inayotazama makazi tu. Na ndio maana nikasema unakumbuka zoezi la vijiji vya Ujamaa? watu walipewa ardhi bure tena kubwa kwa kilimo bado hawakutaka kuacha makazi yao na wakakataa SHERIA hii hii tunayoizungumzia leo..Na watu wanalaani kitendo kile hadi kesho haina maana kilikuwa kibaya lakini ndivyo binadamu tunavyofikiria..

Maafa haya ni matokeo ya safari ndefu toka tukatae vijiji vya ujamaa, ujenzi wa viwanda nje ya miji ili kupanua na kuzalisha ajira huko vitongojini na yote haya ni matokeo ya sera mbovu na mengine yameelezwa huko nyuma...Kupewa viwanja bure sio solution kabisa mkuu wangu kwani hata maskini ombaomba hupewa sehemu za kulala na chakula buree, kuwekwa ktk shelter lakini kwa sababu binadamu kaumbwa na kiburi anataka kuitafuta riziki yake mwenyewe hapendi kuishi ktk shelters kama mfungwa ni bora waingie mjini wakaombe wapate cash kisha waamue watazifanyia nini kuliko kulala na kula bure huku umefungiwa kama mnyama.
 
Sentensi hiyo yaweza kuwa kweli au si kweli; kama unafikiri ina ukweli jadili kwanini na kama unafikiri si ya kweli ina walakini tuelezee kwanini. Clue: watu wa "mabondeni" ni wale wote ambao ambao wamejikuta wakiathirika na mafuriko haya moja kwa moja na watu wa "magogoni" ni watawala wetu.

Mwanakijiji,
Ungeweka kura za maoni ziende sambamba na mjadala huu kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana ingekuwa vizuri zaidi!
 
Majibu yapo hapa kwenye Mwananchi:
Rais Kikwete kwa hili tuko pamoja
Thursday, 22 December 2011 20:02
mwananchilogo.jpg
UKURASA wa kwanza wa gazeti hili tumechapisha habari ya Rais Jakaya Kikwete akiwataka wakazi wanaoishi mabondeni kuhama ili kuondokana kukumbwa na maafa mengine yanayoweza kutokea katika siku zitajazo.
Rais Kikwete alisema inasikitisha kuona wakati Watanzania tunaomba usiku na mchana mvua inyeshe ili mazao yastawi, wapo wenzetu ambao wanaomba jua liwake mwaka mzima ili waendelee kuishi maeneo yasiyoruhusiwa ya mabondeni.Vilevile, Serikali imesema kwamba itatenga eneo la wakazi waishio mabondeni waweze kuhamia.

Agizo la Rais Kikwete linafuatia mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia Desemba 20 mwaka huu, na kusababisha vifo vya watu 30 na majeruhi 50.

Tunachukua nafasi hii kumpongeza Rais Kikwete kwa kuchukua uamuzi huu ambao utasaidia kunusuru maisha ya mamia ya watu ambao wanaishi katika maeneo hayo jijini Dar es Salaam.

Kutokana na wananchi kupoteza maisha, mali na miundombinu mingi kuharibika hili ni janga la kitaifa na kama tulivyosema katika tahariri yetu ya gazeti la jana kuwa Serikali ihakikishe inawahudumia wananchi wote walioathirika na mafuriko haya.

Pamoja na Serikali kutenga eneo la kuwahamishia wakazi, ikiwa ni pamoja na kuwapatia misaada wale wote waliokumbana na mafuriko hayo ambapo nyumba zao zilianguka na kisha kusombwa na maji, lakini sisi tunasisitiza kwamba agizo la Rais Kikwete kuwataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama lisimamiwe na kutekelezwa watendaji wa Serikali.

Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa Serikali kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaam kuhama mara mvua kubwa zinaponyesha na kuleta madhara.

Tunakumbuka vyema Serikali iliwahi kulitangaza eneo la Jangwani kuwa ni eneo la maafa na hivyo kuwataka wakazi wote wa eneo hilo kuhama, lakini, hakuna mtu ambaye alihama.

Kama hiyo haitoshi, Serikali iliwahi kuwavunjia nyumba wakazi wa eneo la Jangwani kuwalazimisha kuhama, lakini zoezi hili lilisitishwa baada ya wakazi wa eneo hilo kukimbilia kwa viongozi chama tawala na baadaye wakakingiwa kifua kuwa ni wapigakura wasibughudhiwe.

Kutokana na uzoefu huo, tunadhani sasa maafa haya yaliyotokea wiki hii, agizo la Rais litekelezwe kwa vitendo na mtendaji wa Serikali ambaye atashindwa kulisimamia awajibishwe.

Tutakuwa ni nchi pekee duniani ambayo wananchi wake wanaweza kuvunja sheria watakavyo, huku Serikali ambayo inatakiwa kuwawajibisha ikiwachekea na pengine kuwakingia kifua kwa kisingizio kuwa eti ni wapigakura.

Ili kuondokana na hali hii ya wananchi kuvamia maeneo ya mabondeni, ni vyema Serikali itunge sheria mpya ya ujenzi na kuweka viwango vya ujenzi vyenye hadhi ya kimataifa na hasa ujenzi wa kuta mbalimbali,majengo marefu ili kuhakikisha ujenzi holela haujitokezi kwenye miji na majiji.

Alama za nguzo kubwa ziwekwe katika mipaka ya maeneo ya makazi na mabonde ili maeneo hayo yabakie wazi.
Kitengo cha maafa kilichopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu nacho kinatakiwa kuimarishwa ili kiwe na uwezo wa kukabiliana na maafa yanapotokea.

Inavyoonekana kitengo hiki hakijaandaliwa vizuri kutokana na kushindwa kukabiliana na majukumu yanavyopaswa kufanywa wakati wa matatizo makubwa ya maafa.

Katika janga hili la mafuriko, inasikitisha kuona kwamba hata vifaa ya kujiokoa kwenye maji, Serikali haina hadi kufikia mahali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick atafute Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na mamlaka nyingine. Ni maoni yangu kwamba zoezi la kuwahamisha wakazi waishio mabondeni litafanywa kwa umakini ikiwa ni pamoja kuwapa msaada ya ujenzi watu hawa ambao wengi wao hawana kipato.

Souce: Rais Kikwete kwa hili tuko pamoja

Tatizo la kwanza ni aliowaachia watu wajenge na wasibughudhiwe, ni nani huyo? Mleta mada anamjuwa fika.

Hivi JK ameshatoka mapumzikoni Serengeti?
 
Mwanakijiji ;
Tatizo kubwa ni kushindwa kufuata misingi ya kisheria; na serikali yenyewe inaposhindwa kutofautisha sheria ilizoweka na siasa; yamepita maazimio mengi ya kuwahamisha wananchi waliojenga mabondeni je kuna kinachofanyika? Tusubiri hakuna kitakachofanyika zaidi ya maneno mengi; tatizo si maneno tatizo kutenda>

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Tushajadili tatizo,
Then what is the solution?
Wataalamu wanisaidie, hivi pale haiwezekana ukatafutwa mlima maeneo kama kimara au mbezi ukasawazishwa halafu kifusi chote kikaletwa pale!!
Kisha ukaachwa mto uliojengewa kingo labda za upana wa mita hata 20 ambao unaweza kua "nevigable" kwa ajili ya kupunguza foleni!!
Pili kifusi kikikolea na kujishindilia sawasawa panajengwa maghorofa kadhaa kwa ajili ya kupangisha walalahoi!!
Mradi kama huu unaweza kujengwa na bwana miradi (NSSF).
Imekaaje hii wadau?
Tujadilini solution sasa
Hili suala "linajadilika"
Ila sasa hicho kifusi cha kuweza kuijaza Jangwani yote utakata milima mingapi ya kimara au mbezi
 
Daima tumekuwa wa kulalamika badala ya kutimiza sheria za nchi.....kwanza naomba kutanguliza pole kwa wote waliokumbwa na janga hili kwani ndio kawaida ya ubinadamu.

Napenda kuweka wazi mtazamo wangu kuwa jamiiyetu kuwa waliojenga mabondeni ni wavunja sheria na ni sawa na mtu aliyefanya kosa lingine lolote . sasa kuna kundi la watu wamejenga mabondeni na kuvunja sheria bila ya kujua na wengine wamejua na kutenda wakiwa wanajua wazi wanachokifanya. kwa mujibu wa sheria za taifa letu ujenzi wowote lazima upewe kibali ya kujenga jengo hilo, hivyo basi yeyote aliyejenga bila kupewa kibali ni mvunja sheria.

lakini swali kubwa ni kujiuliza mamlaka zinazohusika na mipango miji zilikuwa wapi mpaka sheria za nchi zimevunjwa na kundi kubwa la watu mpaka kupelekea uvunjaji huu wa sheria kuwa haki zao za msingi? hivyo serikali haiwezi kukwepa ulegelege wake uliopelekea majanga haya na uvunjaji mkubwa wa sheria na hasara kubwa katika taifa letu..ni lazima timu kubwa sana inayohusika na mipango miji wafukuzwe kazi na kushitakiwa. lakini wananchi lazima tuanze kuheshimu sheria za mipango miji....na mbeleni tusijekutumia kigezo cha kutojua sheria za ujenzi na makazi eti ndio sababu ya sisi kuzivunja

​kazi kweli kweli
 
Nadhani aliye na matatizo ni mimi kwa lugha yako njema.
Ninachosema hapa ni kuwa hawa watu walipewa viwanja bure wakakataa! Overprice inatoka wapi ukipewa kitu bure!

Hilo ni tofauti na bei ya viwanja kwa ujumla wake. Tusichanganye hoja ili kukwepa ukweli. Ukweli unabaki pale pale walikataa kuhama.

Pili, hatuwezi kuachia sheria kwa visingizio. Ndiyo maana miji ipo hovyo. Sheria lazima simamiwe kikamilifu na si hapa tu ndivyo ilivyo dunia nzima kwenye mipango miji.

Kinachotukwamisha watanzania ni kukwepa uwajibikaji na usimamizi wa sheria. Tumekuwa wazuri kutetea hata uvunjaji wa sheria.
Kujenga mahali pasiporuhusiwa ni ukikuaji wa sheria, na kukataa kuhamia eneo walilopewa BURE ni uzembe.
Tuambizane ukweli Watanzania, tusijifiche vichwa kwenye ardhi viwili wili vikiwa nje.

Haya, hoja yako iko sahihi kaka.
 
Mkuu kama nimemwelewa Nyani Ngabu alichosema ni kwanza viwanja maeneo yanayokubalika havishikiki hawa watu waliojenga Jangwani na Kigogo kinyume cha sheria hawan uwezo wa kununua viwanja sehemu yoyote ktk mji wa Dar na viwanja hivyo walipojenga vilikuwa bure na pia karibu na mjini ambako hupatia riziki zao, hivyo tunazungumzia Dar Es Salaam na sio nje ya mji.

Ukitaka kuwandoka watu Dar kwa kuwapa viwanja nje ya mji lazima pia ufikirie hawa watu wataweza vipi kufikia sehemu za kupatia riziki zao yaani wataweza vipi kuja Dar na kuendelea na maisha yao jambo ambalo serikali imeshindwa kulitazma isipokuwa kufuta sheria inayotazama makazi tu. Na ndio maana nikasema unakumbuka zoezi la vijiji vya Ujamaa? watu walipewa ardhi bure tena kubwa kwa kilimo bado hawakutaka kuacha makazi yao na wakakataa SHERIA hii hii tunayoizungumzia leo..Na watu wanalaani kitendo kile hadi kesho haina maana kilikuwa kibaya lakini ndivyo binadamu tunavyofikiria..

Maafa haya ni matokeo ya safari ndefu toka tukatae vijiji vya ujamaa, ujenzi wa viwanda nje ya miji ili kupanua na kuzalisha ajira huko vitongojini na yote haya ni matokeo ya sera mbovu na mengine yameelezwa huko nyuma...Kupewa viwanja bure sio solution kabisa mkuu wangu kwani hata maskini ombaomba hupewa sehemu za kulala na chakula buree, kuwekwa ktk shelter lakini kwa sababu binadamu kaumbwa na kiburi anataka kuitafuta riziki yake mwenyewe hapendi kuishi ktk shelters kama mfungwa ni bora waingie mjini wakaombe wapate cash kisha waamue watazifanyia nini kuliko kulala na kula bure huku umefungiwa kama mnyama.

Umenielewa vyema kabisa. Sina hata la kuongeza.
 
Kama watu wanajenga kuanzia msingi mpaka nyumba inasimama bila kupewa maelekezo au kuzuhiwa,tatizo lipo kwa nani hapo? Tatizo ni vichwa vya watu wa magogoni.......
 
Back
Top Bottom