Mzalendo80
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 2,508
- 1,338
Sentensi hiyo yaweza kuwa kweli au si kweli; kama unafikiri ina ukweli jadili kwanini na kama unafikiri si ya kweli ina walakini tuelezee kwanini. Clue: watu wa "mabondeni" ni wale wote ambao ambao wamejikuta wakiathirika na mafuriko haya moja kwa moja na watu wa "magogoni" ni watawala wetu.
Nakubaliana na wewe Mwanakijiji, tatizo lipo kwa wapangaji wetu wa Magogoni. Ukitembelea nchi zilizoendelea utakuta viwanja kama vya watu wanaishi mabondeni ni bei ghali mno. Kwanza kipo karibu na mto, pili kuna kama mlima. Nchi zilizoendelea hizo sehemu ni bei ghali kama viwanja vilivyo karibu na Bahari.
Tatizo liliopo hapa kwetu ni kwamba serikali haijali wananchi, haitengenezi miundombinu ya kupitishia maji machafu na safi na mazingira mazuri ya kuwafanya watu wanoishi (mabondeni kama wanavyosema) kupata hizo huduma, ingawa kupata hizo huduma hapa Tanzania ni ndoto kama tukiendelea na wajinga hawa waliotufikisha hapa tulipo kwa upuuzi wa watu wachache, uvivu wao wa kufikiria umefika kikomo zaidi ya kukwapua kodi za Watanzania na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi bila ya kuwajali walipa kodi wenyewe.
Hebu angalieni Nyumba zilizo sehemu kama hizo za Mabondeni na hakuna mafuriko, tusiwalaumu wakazi wa sehemu hizo wakati tatizo lipo kwa wapangaji wetu wa magogoni wliofikia kikomo cha kufikiria na Wavivu ndani ya vichwa vyao