Tatizo si Kikwete na uelewa wake bali chuo kikuu alichosoma!

Papa D, Kwa kuliona hilo jitose kwenye sisiem uonyeshe the difference na Hadija Kopa atakutumbuiza siku ya uteuzi wako. Otherwise , Kusema bila kuonyesha utofauti wako huna maana
 
Nitavunjika mbavu hatimaye leo

hatimaye utapelekwa muhimbili .... badala ya kufanyiwa operesheni ya mbavu utafanyiwa operesheni ya kichwa .... hivi wale madoctor vilaza walisoma chuo gani
 
I was about to drop a nasty comment,but let me spare him.It is about mental and intellectual intergrity....nwei,let me ignore him
 


Katika mchanganuo wako zingatia haya:-
Nimesema wanakaririshwa na siyo kukuza uelewa wao. hii ni hata katika tasnia unayojaribu kusema [coordination-uratibu] mwisho wake wanaishia kuwa wana nadharia
Mlinganisho ninaozungumzia ni ule wa similar level of award [i.e chukua aliyemaliza digrii ya sheria mlimani na course ile ile pale mzumbe]
Bado utakuwa haiko sahihi kumtetea JK au Pinda kutokana na kwamba mtu aliye-elimishwa kwa kukaririshwa hawezi kusahau basics tofauti na mtu aliyekaririshwa. Hii nadharia huenda ikawa ngumu kuielewa mpaka ukikutana na watu wa aina hiyo wakifanya kazi katika eneo moja. you will see the difference between he who thinks and he who claims!!
 
Politics is the ability to foretell what is going to happen tomorrow, next week, next month and next year. And to have the ability afterwards to explain why it didn't happen...Winston churchill
 

THERE YOU ARE! Kazi kunung'unika nadharia kibao vitendo hamna, ndo walotufikisha tulipo...na hasa kizazi cha miaka 10 iliyopita , kuna tata somewhere. Kila mtu ni mwanasiasa pale
 
Papa D, Kwa kuliona hilo jitose kwenye sisiem uonyeshe the difference na Hadija Kopa atakutumbuiza siku ya uteuzi wako. Otherwise , Kusema bila kuonyesha utofauti wako huna maana

huu nao ni mpasho!
 

Hapo ndugu umechemka kidogo! Haiwezekani kwamba eti wanaokosa nafasi Mlimani ndo wanaenda vyuo vingine. Yaani unataka kusema hata yule anayeenda SUA alikosa nafasi Mlimani? Sahihisha hapo, naomba SUA muiondoe kwenye huu mchuano wenu ili kama mkiamua kuchapana makonde mchapane wenyewe.
 
..tatizo ni Kikwete mwenyewe siyo chuo kikuu alichosoma.

..Kikwete alishapata kusema yeye ni mchumi lakini hapendi mahesabu.

..nikimnukuu Majjid Mjengwa, huyo ni sawa na fundi makenika asiyetaka kushika spanner.
 
hapo ndugu umeenda isivyo naomba uangalie elimu ya SUA kama unabishi mpeleke mdogo wako au akasome MSc. au PhD uone mzikwake usichukulie vyuo UDSM ndio wako juu sana tunafanya nao kazi tunawaona majority hawana lolote ni jina tu


UDSM hawasomi kilimo, huo ulinganifu na SUA na UDSM unalinganisha kwenye fani gani?. Mnangángánia kukaa mjini kufanya kazi kwenye ma-bank,... Ebu nenda mkasaidie Kilimo kwanza huko ebo !!!!!.....
 
kuna tofauti kubwa sana kati ya kukaririshwa na kueleweshwa. si UD pekee, ni vyuo karibu vyote na shule karibu zote Tanzania. wanafunzi wanasoma ili kufaulu mtihani na si kuelewa kile walichofundishwa! matokeo yake, wakipata challenge kidogo kwenye kazi/maisha hawawezi ku apply kile walichofundishwa darasani kwasababu hawawezi kuoanisha walichofundishwa na changamoto zilizoko kwenye kazi au maisha ya kila siku. matokeo yake ni kulalama badala ya kutafuta solution ya changamoto wanazokutana nazo
 

Hizi thread za ki-teenager ndiyo zinafanya watu tuanze kuona kuwa JF siku hizi imepoteza great thinkers. Mtu yeyote mwenye akili timamu ataona kuwa kumuwakia huyu anayejiita Papa D ni sawa na kumfukuza kichaa aliyechukua nguo zako wakati wewe unaoga.

Thread pekee imeisha mueleza muanzilishi wake ni mtu wa aina gani katika ujuvi wa mambo, hasa ya kielimu maana kama angekuwa anabusara angefahamu lengo kuu la chuo kikuu na vyuo vingine, halafu aje kwenye umri wa chuo kikuu na vyuo vingine, halafu aende kwenye CV za walimu makini kwenye vyuo vingine na kuangalia walisoma wapi?, then atoe statistics za jinsi watu wa chuo kikuu na vyuo vingine jinsi wanavyo perform kwenye Private sector. Halafu aangalie je ni jinsi gani siasa inavyoweza ku-correlate na kiwango cha elimu ya mtu, then aangalie chuo alichosoma kina affect vipi hii correlation.

Otherwise nachelea kusema kuwa mwanzilishi wa hii thread amebugi step maana kaonesha wazi kabisa kuwa ana chuki na chuo kikuu kama taasisi (Huenda alitoswa kwenye kuomba nafasi kwa kutokuwa na sifa, ama alipigwa "disco" kwa kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri kama thread inavyoonesha). kumtumia JK kama graduate ilikuwa ni janja tu ya kuiweka thread hii kwenye jukwaa la siasa ambalo isingepaswa kuwepo. MODS Can you take this jukwaa la elimu?

Note: Chuo Kikuu = UDSM
 
UDSM is a mother University in Tanzania. Pole sana wewe uliekua na hamu sana ya kusoma UDSM lakini sababu ulifail (hukua na grades zinazoitajika pale the hill)...Ukachukuliwa na Tumaini, Ruco, Mzumbe etc. Hoja yako ni mfu. Naomba kuwasilisha.

Agreed hakuna ubishi
 
Hii topic tulishaijadili sana.mods naomba mui-merge na ile inayohusu UDOM kuwa chuo cha kata.
 
Kama ni chuo cha vilaza mbona huwa kinachukua cream yote, hafu mtu akikosa mlimani ndo anafikiria kwenda vyuo vingine, kwa nini?

Nimesema wanaohitimu pale sio wanaodahiliwa kusoma pale. Maana yake ni kwamba tatizo si wanafunzi bali wanaowafundisha!!!
 
wengi

Hakuna Ubishi kuwa wanafunzi wengi wanaojiunga SUA ndoto zao za Awali zilikuwa ni kusomea Udaktari Mhimbili au Uchumi na Uhasibu UDSM, na wao hujiunga SUA baada ya kupigwa panga UDSM (kumbuka Mhimbili lilikuwa Tawi la UD).Watu wengi waliomo humu JF wamepitia hizo procedure za enzi hizo kila chuo kina aaplication from zake.Mimi ninamifano ya watu wengi waliopata admission SUA na UDSM, waachana na SUA. Haina Ubishi wewe ni mhanga wa wale ambao hamjanusa UD
 
Wewe ukitaka kulinganisha hivi vyuo viwili na wahitimu wake, mchukue Samuel Sitta kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na utendaji wake akiwa spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano na Anne Makinda kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe (IDM) akiwa Spika pia wa Bunge hilo, then utapata chuo kipi na uelewa upi mtu aligraduate nao pia utendaji wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…