Tatizo Lilitokea Miaka kumi Iliyopita

Tatizo Lilitokea Miaka kumi Iliyopita

jrmlaurence

Member
Joined
Dec 2, 2010
Posts
80
Reaction score
57
Jamaa alivunjika mguu akaepelekwa hospitali;
DAKTARI: Imekuwaje mpaka ukavunjika mguu?
JAMAA: Miaka kumi iliyopita…
DAKTARI: Staki kujua hayo nataka kujua umevunjikaje mguu?
JAMAA: Dokta nisikilize kwanza, miaka kumi iliyopita nilikuwa nafanya kazi kwa bosi moja kule Uzunguni, siku moja binti yake mzuri sana akaja chumbani kwangu na kuniuliza kama nahitaji kitu chochote, nikamjibu sitaki, akarudia tena tena na kuniuliza tena kama sihitaji kitu chochote, mimi nikasema sihitaji kitu, akaondoka anacheka.
DAKTARI: Sasa hiyo inauhusiano gani na kuvunjika mguu?
JAMAA:Sasa leo nilipokuwa niko juu ya mnazi nagema, si ndio jibu likanijia kwanini yule mrembo alikuwa ananiuliza lile swali, ndio bahati mbaya nikajisahau nikaanguka na kuvunjika mguu
 
duh! memory ya jamaa kiboko. alikosa menyu kizembe kweli
 
Back
Top Bottom