Tatizo la Waraka wa shehe Ponda ni zile takwimu hazina uhakika na ni kinyume na sheria

Anasema watu waseme kweli, je anamaanisha hilo? Ni vyema ukaijua tabia ya mtu. Huwa inasemwa tazama matendo na sio maneno. Mfano mrahisi ni jana, kuna mjumbe toka kanda ya kusini, alitoa malalamiko ya kuwa wapinzani wanatoka huko upinzani na kupewa nafasi. Majibu aliyopewa yalikuwa ni kebehi zaidi kuliko ilivyopaswa. Inaonekana unatetea jambo ambalo hujalifanyia utafiti.

Yote kwa yote ujumbe wa Ponda umefika, hata akichukuliwa hatua ni kwa mapungufu machache ya waraka wake, lakini ndani vya huo waraka kuna ukweli wa zaidi ya 80%. Na uzuri ukweli huwa unajitetea wenyewe. Ni watu wachache sana huwezi kusimamia hadharani ukweli ulio kinyume na watawala. Na hii ni toka zama za manabii.
kama mtu ana uhakika wa anachosema na anayo dhamira njema kwa mujibu wa imani yake, anaogopa nini kukisema?
Kama malalamiko haya ya waislamu ni ya kweli, kwanini Mufti hayasemi mbele ya Rais na hata hadharani?
Nakumbuka enzi za Mufti akiitwa Hemed bin Jumaa bin Hemed, kuna kijana wa kiislamu alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kusema 'Yesu siyo Mungu', Mufti alitoka hadharani na kusema kuwa waislamu wote ndivyo wanavyoamini kuwa Yesu siyo Mungu, kwahiyo kumshikilia kijana huyo ni kama kumdhulumu haki yake ya kukiri anachoamini. Kama nakumbuka vizuri kijana yule alishinda rufaa yake, na ushindi wake kwa mtazamo wangu hauthibitishi kuwa Yesu siyo Mungu bali unathibitisha uhuru wa mtanzania kuamini dini anayoitaka ilimradi hajavunja sheria.
Vivyohivyo kwa yanayolalamikiwa, kwanini Mufti asiyawakilishe serikalini aseme wazi kuwa hivi ndivyo waislamu wanavyotaka, pawepo mjadala na uchunguzi kuhusu haki iliyokiukwa kama ipo, muafaka upatikane.
 
Kwahiyo mkuu katika maboresho hapo UDOM ndio waondolewe waislam 11 waletwe wakristo 11? .Hakuna hata mkristo alikuwa na sifa sawa za waliondolewe achanganywe katika hao 11?

Kuna tatizo hapo nawala sibahati mbaya.
Bado kuna mambo ambayo huyu aliyeleta malalamiko hajaweka wazi. Maswali haya:
1. Jumla ya wote walioondolewa UDOM ni hao 11 tu au mwandishi amechambua hayo majina ya waislamu yakatimia 11? Hao wengine ni kina nani? Tupate ushahidi kutoka UDOM.
2. Jumla ya watu wote waliopelekwa UDOM kuziba nafasi wazi ni hao 11 tu, au mwandishi amechambua majina ya hao wakristo 11? Hili nalo lahitaji ushahidi kutoka UDOM
3. Kabla ya kuondolewa hao waislamu 11, wahadhiri wa kiislamu jumla yao ilikuwa wangapi na sasa wamebaki wangapi? Hali kadhalika kwa hao wahadhiri ambao ni wakristo walikuwa wangapi kabla ya mabadiliko na sasa ni wangapi?
4. UDOM wanasemaje kuhusu mabadilik haya, yalikusudiwa kufanikisha nini? Vigezo (criteria) vilivyotumika katika mabadiliko hayo ni vipi? Dini ni criterion mojawapo?

Tukishapata majibu ya maswali hayo ndipo tunaweza kusema kama kulikuwa na nia ovu ya ubaguzi au la.
 
Mkuu hukufatilita mjadala toka mwanzo, Yule Mama nafikiri mama Kabaka Kama sijasahau alijibu majibu ambayo hayana kichwa Wala miguu tafuta hio thread iko humu tangu mwaka Jana watu wakilalamika.
 
Acheni kujifungia kwenye misikiti nendeni mkasome,!

Huku mtaani unakuta toto liko busy msikini linakariri yale maandishi yenu ya kuandika toka kulia kwenda kushoto, mwisho wa siku linaishia kupata 0 shuleni. Alafu mnataka teuzi kwa kigezo cha dini?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
huku mtaani kwetu wapo wengi mno walio soma hayo maandishi yao na class walitusua kinyamaa!!!sawa na tusio soma yale maandishi na class tuka chemka mbaya!!!
 
Mkuu hukufatilita mjadala toka mwanzo, Yule Mama nafikiri mama Kabaka Kama sijasahau alijibu majibu ambayo hayana kichwa Wala miguu tafuta hio thread iko humu tangu mwaka Jana watu wakilalamika.
Samahani sikuiona hiyo thread. Kama una urahisi wa kuipata naomba uniwekee link
 
hii comment yako ni chonganishi , inafikirisha na ina ukweli nusu!! sasa ni ngumu waislam kufanya unavyotaka sababu waislam wamo ndani CCM juu kileleni Bashiru na Samia ila kwenye ajira na elimu ziiii! teuzi zote za Mkulu wakristo watupu!!! nadhani hilo liko njiani ngoja wazee wapukutike kwanza Allahu Aalam na kama ikitokea hivyo itapendeza sana, waislam waipigie kura ACT, hii ni fursa kwa ZZK kupandikiza hii dhana itauzika, yaani aseme chagua ACT mwislam uokolewe upate maendeleo, upate ajira upate elimu!!
Zitto is smarter than that, anajua akisema hivyo atakosa kura za wakristo ambao anawahitaji pia. Asimame katikati kwa neno la haki sawa, hapo atafanikiwa. Haki sawa kwa maana ya kwamba anataka kuondoa dhuluma zote zilizotendewa watu wa aina zote. Nina uhakika watu wa kila kundi wana malalamiko yao mbalimbali, ajikite kwenye haki na usawa.
 
Wana CCM kila atakae ongea "UKWELI" lazima apingwe. Tumewazoea.

Turudi kwenye "HOJA KUU" ya swala la "KUTENDA HAKI", dini zote zinalitilia mkazo hili swala. Na hata mungu amewaonya vikali na amewa ahidi kuwapa adhabu kali sana wale wote wanao "PINDISHA/KUNYIMA/KUDHULUMU/KUPUNJA" haki.

Hata kama utadhulumu "PIPI MOJA" katika kontena zima la 40FT basi jiandae na adhabu kali sana kwa mola wako.

Kuomba "TUME HURU" ni kwasababu "HAKI ITENDEKE". Sio swala la kichama hilo.
Pendekeza tume iwe na watu gani,maana inawezekana ni kelele tu kumbe tume huru ndiyo iliyopo
 
Ukweli hauhitaji sheria yoyote kusimama pahala pake.

Udini haufai, nchi hii ni yetu sote, tunahitaji kuwa fair kwa makundi yote ya kijamii.

80% kwa 20% ni too much, haijakaa sawasawa hata kidogo

Waislamu majority wanaunga mkono waraka
Sasa unasoma madrasa halafu upewe ukurugenzi?? Akili matope hiyo.

Waislamu wasipoishukuru serikali ya CCM hapo hata mungu ataendelea kuwapiga kofi,yaani Mzee Mkapa aliwapa chuo kikuu Morogoro pale na wanasoma waislamu tu,bado mnasema mnabaguliwa?

Taja chuo gani wakristo wamepewa zaidi ya vyuo vyao kwa kuthamini elimu dunia badala ya elimu ya tusikokujua.

Tuongee ya kweli,unajiita muislamu safi halafu unaongea uongo tu.

Kabla hujalaumu,tafuta idadi ya wasomi wakristo against waislamu watanzania. Kama umesoma utagundua hata bila kuzunguka.
 
pia tusi sahau ile MEMORANDUM OF UNDERSTANDING baina ya Serikali na Makanisa pengine ndiyo sababu ya makanisa kuwa na vyuo na mashule! ikiwa ni sababu basi niwazi kuna upendeleo wa imani fulani dhidi ya imani fulani unao fanywa na serikali.
 
Siku na sisi tusioamini katika hizo dini zenu zilizokuja na mashua tukiamua kutaka upendeleo kwenye vyeo na teuzi ndio mtajua sisi ni nani....hahahahah natania tu, miungu wetu hawana wivu kama wa kwenu; tunawaandika kwa herufi ndogo ya mwanzo hawagombi, tunaweza kuwachanganya wao na yule wa kwenu bila wao kuwa na wivu, wakati hao wa kwenu huwezi kuchanganya Allah na Yehova yaani ufahamike unasali kwenye madhehebu yote mawili uachwe hivi hivi! Huyo wa kwenu anataka dunia yote na sayari zingine wawe ni waumini wake tu....wa kwetu hana kiu na idadi ya waumini, hata watatu tu wanatosha, hata majina ya "ubatizo'' mungu wetu hana habari nayo hata uitwe Masoud au Yohana hawezi kukubagua!
 
Back
Top Bottom