Tatizo la Wanawake Kupata Maumivu Wakati na Baada ya Kujamiiana: Fahamu Sababu na Suluhisho la Tatizo

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,967
22,161


WADAU WANAOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU MATATIZO HAYA
Nisaidieni kuhusu hili: inakuaje mwanamke anadai anahisi maumivu wakati wa tendo la ndoa, ni kwamba uume mkubwa au namna ya kufanya nae, ila tatizo style zote anadai maumivu anayasikia.

Habari zenu wakuu.
Kupata maumvu ya tumbo au kitovu pia pindi mwanamke anapofanya tendo la ndoa au sex je tatizo ni nini kwa mtu huyo.
Na je nini hafanye ili aweze kujiondoa katika tatizo hili.


FAHAMU TATIZO LA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA KWA MWANAMKE (DYSPAREUNIA)

Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia.

Neno Dyspareunia tamka (dis-pa-roon-ia) linatokana na neno la kigiriki lenye maana ya shida katika kuingiliana wakati wa kufanya tendo la ndoa (difficulty mating au badly mated).

Utafiti unaonesha kwamba kati ya wanawake watatu, wawili wamewahi au hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Imefika kwamba baadhi ya ndoa, mwanamke anapata maumivu kiasi cha kutokuwa na hamu tena ya tendo la ndoa na matokeo yake wamekuwa na wakati mgumu linapokuja suala la kufanya mapenzi na pia kila wakirudia kufanya tendo la ndoa, mambo ni yamekuwa ni yaleyale kwa mwanamke kuumia zaidi kuliko mara ya kwanza.

Kawaida huwa haifurahishi kabisa na haina hata ladha kufanya tendo la ndoa huku mmoja kati yenu akiwa anapata maumivu makali au shida hiyo husababisha kutojishughulisha katika kuleta raha ya kweli na hatimaye kuridhishana kimapenzi wakati wa tendo la ndoa.

Tendo la ndoa halikuwekwa ili kukupa shida au maumivu bali kukupa raha, furaha na kuridhishwa.
Moja ya kanuni muhimu sana katika tendo la ndoa ni:

Kama unapata maumivu usifanye
Badala yake tafuta nini kimesababisha na tafuta jibu sahihi la kuondoa hiyo hali au muone daktari akusaidie.
Na baada ya kupata tiba na kupona ndiyo unaruhusiwa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kufurahia na kukupa raha zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuleta maangamizi.

Ni kweli kwamba kama moja wapo ya mahitaji ya msingi ya kihisia (emotions) kama hili la tendo la ndoa halipatikani katika ndoa linaweza kusababisha mmoja ya wanandoa kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake na kutoka nje kwenda kutafuta mtu wa kumridhisha zaidi, hata hivyo kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa huku anapata maumivu au kuumia kwa kuogopa kwamba asipompa Mume wake haki yake basi anaweza kutoka nje na kutokuwa mwaminifu hilo si sahihi kwani ni kutojiamini na kutojali si afya yako tu bali haki yako ya msingi ya kufanya tyendo la ndoa kwa kupata raha.

Mnahitaji kujulishana na kuelezana ukweli ili muweze kupata dawa na hatimaye kurudi kwenye raha upya badala ya kuumizana.

Kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke au hata mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na inaweza kuwa ni wakati mwanaume anapoingia (penetrate) au wakati wa kitendo chenyewe au baada ya kitendo chenyewe.

Inaweza kuwa ni maumivu makali sana au inaweza kuwa ni kuwashwa au inaweza kuwa ni maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida au inaweza kuwa ni maumivu ambayo unasikia kama moto unawaka vile ndani yako wakati wa tendo la ndoa.

Naamini kufika mwisho wa hili soma utakuwa umefahamu si nini kinasababisha bali utafahamu jibu la hili Tatizo.


Kichwani (brain & mind) ndiyo kiungo kikubwa cha tendo la ndoa, jinsi unavyojiweka kwenye akili zako inaweza kusababisha raha au maumivu ya tendo la ndoa.

Kwa nini ujisikie maumivu

Maumivu wakati wa tendo la ndoa husababishwa au hutokana na sababu za kihisia na za pia (physical and emotional)
Ili kujua kwa nini maumivu kutokea ni vizuri kujua nini hutokea kwa mwili wa mwanamke wakati wa tendo la ndoa (sex)
Mwili wa mwanamke hupitia hatua nne (4) muhimu kukamilisha tendo la ndoa.

HAMU (dedire)
Hapa mwanamke hujisikia anataka kufanya tendo la ndoa

KUSISIMKA (arousal)
Hapa mwili husisimka kwa sehemu zake za siri (vagina) hutanuka urefu na upana pia hutoa majimaji yanayorahisisha mwanaume kuingia (penis penetration), kisimi hudinda na kuongezeka ukubwa, chuchu husimama na kusisimka, uterus hupanda juu nk

KUFIKA KILELENI (orgasm)
Hapa ni kilele cha mwitikio wa tendo la ndoa, misuli hujikusanya (contradict) na kumpa hisia kubwa za raha na utamu wa tendo lenyewe.

SULUHISHO (resolution)
Viungo vyote vinavyohusika na tendo la ndoa hurudi kwenye hali ya kawaida

Aina za maumivu na sehemu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke zinaweza kutokea kwenye katika sehemu zifuatazoSehemu ya nje ya vagina, yaani vulva na huumia wakati inaguswa au kuwasha hata unapotumia baadhi ya sabuni na wakati mwingine kusababisha makovu au utando unaonesha kuna cheese.sehemu ya tundu la kuingia kwenye vagina na sehemu ya ndani ya Vagina unayoungan na uterus.

Je ni kawaida mwanamke kupata maumivu hata kama hajaambukizwa magonjwa ya zinaa?
Kawaida kila mwanamke ana aina ya chachu au hamila (yeast) kwenye sehemu za siri zake za siri, na hii yeast ikiongezeka sana inaweza kusababisha kuwasha au maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida na pia husababisha kutoa majimaji meupe mithili ya maziwa na hii hutokea kama mwanamke anatumia antibiotics au medication inayosababisha kuua bacteria wanaofanya hiyo yeast kutoleta madhala yoyote. Hivyo ni jambo la kawaida kwa mwanamke kujisikia maumivu mara chache wakati wa tendo la ndoa ingawa maumivu yakizidi inabidi uchukue hatua inayotakiwa ili kupata tiba kamili.

Vitu gani vinavyosababisha kuumia wakati wa tendo la ndoa?
Kukaza kwa misuli ya vagina (Vaginismus) (tamka vaj-uh-niz-muh s)Ni kukaza kwa misuli ya vagina bila hiari (involuntary) na kusababisha tendo la ndoa kuwa gumu au kutofanyika kabisa. Mwanamke mwenyewe anaweza asijue kwamba misuli inayozunguka vagina umekaza na kusababisha maumivu wakati mwanaume anaingiza penis.
Hii hali hutokana na hofu na mashaka aliyonayo mwanamke kuhusiana na suala la tendo la ndoa kwamba anaweza kuumia (kisaikolojia).

Pia wanawake wengi wenye vaginismus hawajawahi pata furaha ya tendo la ndoa maishani mwao na wengi ni waoga sana hata kwenda kwa madaktari kuhofia daktari anaweza kuchokonoa vagina zao hivyo kuongeza tatizo zaidi.

Ni nini husababisha hiyo hofu na mashaka?
Malezi aliyofundishwa kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya na dhambia na hata akiolewa anafahamu kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya. Malezi aliyolelewa kwa kuambiwa kwamba vagina ni nyembamba sana na hivyo tendo la ndoa husababisha mwanamke kuumia.

Kama amewahi kudhalilishwa kimapenzi kama kubakwa anaweza kuwa na hofu na tendo la ndoa kwa sababu aliumizwa.
Kama amewahi kupata magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yanamuumiza sana na kumpa shida pia anaweza kuwa anahisia za kuumia wakati wa tendo la ndoa.

Wanawake wengi wa aina hii hupata raha sana wakati wa foreplay na utamu wa mahaba huwaisha pale tu penetration ikianza. Kitu cha msingi ni kwamba ili tendo la ndoa liwe tamu na zuri hali ya akili na ubongo ni muhimu sana kwani hisia zote za utamu wa tendo hutafsiriwa kwenye ubongo na ubongo ukipata pollution ya mawazo mabaya basi kila kitu kitaenda kombo. Tutaendelea na somo kuangalia vitu vingine vinavyosababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.


MAJIBU NA MICHANGO YA WADAU KUHUSU TATIZO HILO
 
Somo zuri kaka. Saaana!! Maana hata mimi limenikuta hilo, kijana nahangaika mwisho wa siku ni kusumbuana tu na kukojolea mashavuni mwa "mma"! Mbaya zaidi maandalizi yalikua yanachukua muda wa kutosha, ila ukitaka tu kubisha hodi, kesi. Ila KY inasaidia.
 
Kaka hii kitu mpenzi wangu anayo. Wakati wa tendo yeye anasikia maumivu na wakati mwingine pana waka moto, kuna siku tulikutana kimwili na alipata hiyo hali lakin hakumia sana kivile, chakushangaza kesho yake alinipigia cmu nakudai anasikia maumivu makali na kumevimba! Kaka hii hali inatiba? Hebu nisaidie nisije nikapoteza kipenzi changu!
 
Nimechoka ila niwape kiprofessional kidogo. Maumivu haya kwa wanawake yanatokana na
i) STDs/STIs
ii) FUNGI
iii) Cancer.
 
Asante kwa elimu yako mkubwa kwani mpenzi wangu analo hili tatizo, bora nitafute tiba mapema!
 
Asante kwa Ujumbe Pidy, ila siku nyingine ukitaka kweli members tusome don't put picha inachkua kama more than five minutes kuingalia. lol
 
Baba erick,

Sisemi muongo ila hizo zinachangia maumivu. Binafsi nikiwa na google nimeona mtu akiwa anaumia kweli ingwa katikati anaita tamu huku mwanzoni kaumia na tukapima zote hapo juu -NIL

Tulichofanya nikuamini hayo ndio mapenzi tuliopewa na muumba mppaka akaja kuolewa, ila ukiona mtu anaumia pls nenda pima hayo juu ukikuta akuna kitu basi hilo neno yaani ndio mzigo wako.
 
Kila mwanamke kwenye uke wake kuna kiwango muhimu cha bacteria, fungus, yeast au protozoa na hawa viumbe hawana madhara yoyote katika mwili hadi hapo kiwango chake kikiathirika na mazingira yake kama matumizi ya antibiotics, kuwa na medication au madawa na uzazi wa mpango na ndipo matatizo hutokea na kupata haya matatizo si kuwa unaumwa magonjwa ya zinaa ni hali ya kawaida kitu muhimu lazima uhakikisha unapata dawa.

Leo tumalizie na mambo yanayosababisha kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke.

Maambukizo (vaginal infection)
Mwanamke anaweza kupata maambukizi kutokana na bacteria, fungus, yeast na amoeba. Kawaida kwenye sehemu za siri za mwanamke kuna kiasi kikubwa cha bacteria, fungus, yeast au amoeba ambao hawana madhara yoyote hadi pale uwiano ukiwa tofauti kutokana na sababu mbalimbali kama vile madawa nk. Maambukizi (infections) yanapotokea kawaida kunakuwa na mabadiliko yafuatayo:
  • Kubadilika rangi kwa majimaji yanayotoka sehemu za siri za mwanamke,
  • Pia kutoa harufu mbaya baada ya tendo la ndoa,
  • Kuvimba sehemu za siri,
  • Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo,
  • Kuumia wakati wa tendo la ndoa (maumivu ya kama kuchoma na kuwasha).
Menopause
Upo wakati mwanamke anafikia (miaka 48 - 52) muda ambao hawezi kuzalisha tena homoni za estrogen zinazosababisha kuzalishwa kwa yai kila mwezi. Kutokuwepo kwa hii homoni husababisha uke wake kuwa mkavu hata wakati wa tendo la ndoa. Uke kuwa mkavu husababisha kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa na hasa kama hakuandliwa vizuri.

Zipo sababu zingine kama vile hitilafu katika maumbile ya uke kutokana na operation au kubakwa n.k husababisha mwanamke kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Je, wanaume nao hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa?
Ni kweli inawezekana kwa mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa ikiwa:
  • Amepata maambukizi ya bacteria, fungus au yeast kutoka kwa partner wake
  • Kama ameambukizwa magonjwa ya zinaaa
  • Kama hajatahiriwa na hasa kama ndo anaanza kufanya tendo la ndoa atajisikia maumivu kwa sababu ya gozi (foreskin) kugoma kujivuta nyuma.
 
USHAURI WANGU
  1. Jichunguze wewe mume kwanza. Je, huna vimwana wasiojua kuoga na kusafisha nyeti zao kwa maji safi na salama?
  2. Uwe makini sana na utendaji kazi wako. Uzamishaji wa oil stick kwenye Engine sio sawa na urefu wa stick izame yote. Zamisha Stick kwa uangalifu na si lazoma uende mpaka Brake iwe ni Bulb zako.
  3. Uchanganyaji wa sera ya maandalizi ya mwenzi wako si mke tu anaye andaliwa bali hata mume huandaliwa sawa dada zangu. Mume huandaliwa ili ukali na vurugu ukiherehere wa kupanda gari wakati hujatiza maji yapo? oil imeshuka au lah? na je nyaya za betri ziko active?
  4. Dada zangu Ubinafsi wenu ndio unawafanya mnapata hayo maumivu makali maana nyie mnaona haki ni kwenu tu na wenzenu oooooh!
  5. Mwisho kama unayafanya haya yote na bado unasikia maumivu, Jaribu kumuona daktari mkiwa na mwenzi wako ili mpate ushauri kwani Conc. U.T.I inaweza kusababisha hayo muanza dozi wote.
ZINGATIENI SANA HAYO.
 
Leo nimefarijika na somo hili. Kesho nitakuja na maswali yangu. Ngoja niandae kwanza. Asanteni sana kwa muda wentu kutuelimisha.

CD
 
Ila hua watu wengi wanaumia sana alafu mi hua nashangaa wanaume hawaumii hata loh! Kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya Firauni, hebu mie napita tu hapa maaaaana.
 
Thanx kwa somo hii ndo faida ya JF jamani; burudani na somo juu be blessed wajameni.
 
Wana JF,

Mke wangu yupo mbali kikazi na kwa sasa ni mjamzito. Tumekuwa tukikaa hata miezi2 bila kuonana. Nikifika na 2kianza sex analalamika kuumia sana na vagina huwa imejirudi sana hata kupenetrate inakuwa kwashida.

Baada ya siku3 au 4 ndipo huanza kuingia kiurahisi. Pia anasema hasikii hamu yakusex tangu apate ujauzito. Wataalamu hebu fungukeni hapa sababu ya maumivu, vagina kujirudi na yeye kutosikia hamu ya sex.
 
Wewe unakuwa na hamu, mwenzio ameshapoteza hamu with time. Unatakiwa uende naye taratibu na Mazingira yawe mazuri.

Kuhusu kukosa hamu wakati wa ujauzito, itakuwa mimba imekukataa tu. Mimi pia ilinitokea, nilimchukia baba wa mtoto wangu, nilikuja kumpa mtoto ana miezi minne.

Wengine hupelekea kuwapenda waume zao na kuwataka 24/7.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…