A
Anonymous
Guest
Tatizo la maji kwa sisi wakazi wa Kibaha – Mfipa, mtaa wa Simbani limekuwa kubwa sana. Maji yanatoka mara moja au mbili tu kwa wiki tena usiku wa manane wakati tumelala , na wakati mwingine hayatoki kabisa. Hii inaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Maji ni hitaji la msingi kwa maisha ya kila siku—kupika, usafi, afya na matumizi mengine ya familia. Lakini kwa hali ilivyo sasa, wakazi wengi tunalazimika kutafuta maji mbali au kununua kwa gharama kubwa.
Kinachoumiza zaidi ni kwamba Eneo letu la Kwa Mfipa liko karibu sana na chanzo kikubwa cha maji cha Mto Ruvu, umbali wa kilomita chache tu. Inashangaza kuona kuwa karibu na chanzo kikubwa cha maji lakini bado tunapata shida kubwa ya maji.
Hali hii imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu na inaathiri maisha ya wananchi wengi. Tunahitaji suluhisho la kudumu, siyo maji kutoka mara chache bila ratiba ya uhakika.
Tunaomba kwa heshima mamlaka husika za maji kama DAWASA mkoa wa Pwani pamoja na viongozi wa eneo letu waliangalie kwa makini tatizo hili na kulifanyia kazi kwa upana.
🙏 Tunaomba mamlaka husika wachukue hatua haraka kutatua changamoto hii kwa manufaa ya wakazi wote wa eneo hili.
Naomba kuwasilisha.