KERO Wananchi Korogwe Mjini tuna Changamoto ya Maji

KERO Wananchi Korogwe Mjini tuna Changamoto ya Maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wakazi wa Bagamoyo na Kilole, Wilaya ya Korogwe Mjini, tunalalamikia changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yetu.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa hakuna ratiba maalumu ya mgao wa maji hali inayotusababishia usumbufu mkubwa katika maisha ya kila siku. Cha kushangaza ni kwamba hata katika kipindi hiki cha mvua, bado huduma ya maji ni duni sana.

Kuna taarifa kuwa Mamlaka ya maji korogwe (HTM) inashindwa kujiendesha kutokana na matumizi kuwa makubwa kuliko makusanyo husika.

Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka ili wananchi wa Korogwe tuweze kupata huduma ya maji kwa uhakika.
 
Mto pangani hapo umepita mjini kabisa, ila sirikali hawapo serious🤔
 
Huduma ya maji imekuwa ni Anasa korogwe.

Swala la maji limekuwa ni changamoto sana inafika mahali wananchi tunabembeleza Mamlaka ya Maji Korogwe (HTM) itufungulie maji.

Kwa Sasa tuna zaidi ya week tatu hatuna maji licha ya kuwepo kwa mvua za kutosha.
 
Back
Top Bottom